Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”

Mboga moto ugali moto
Mitano tena[emoji23][emoji23]
 
Mbona wanasiasa wanakula hela za serikali za kila siku mnawaacha. Si jana kasamehewa alonunua gari la anasa na zahanati hazina ambulance.
Ameongeza value serikalini kwa kuokoa hela za central government kwa kufanya investment muhimu zenye tija kwa wananchi kupitia mapato yao, amebuni njia za kuvutia uwekezaji, kupeleka ajira kahama na kukuza tax base ya serikali.

Boss baada ya kuona kazi kavutiwa nae kaona anastahili gari la kuchumpa na kiyoyozi kisichotoa kelele ndio maana kamsamehe.
 
Sasa ukifungia hospital na madaktari hao watanzania wagonjwa watatibiwa na nani considering huduma za afya kwenye hospital za serikali ni mbovu kupitiliza.
Sasa hapa haoni kama amejipinga mwenyewe kwenye kauli yake ya uzalendo?
Kufungia hospital na madaktari then hao wananchi watibiwe nani kama huduma za afya kwenye hospital za serikali ni mbovu.

Hapa ni kuingiza siasa kwenye maisha na afya za watu.
Pia hapo ni kuingilia maamuzi binafsi ya mwananchi
Utanilazimisha vipi mimi nifanye kazi hospital ya serikali kisa mkopo kwani mkopo ndivyo ulivyosema hivyo?
Mwananchi anachotakiwa ni kufuata sheria zilizopo na sio kufuata kauli haijarishi ametoa nani. sasa huyo daktari amevunja sheria?

Btw serikali ipo kwa ajili ya wananchi na sio wananchi wapo kwa ajili ya serikali hivyo ni wajibu wake serikali kufuata mapendekezo na haja za wananchi na sio vinginevyo.

btw Sikumbuki lini nilikanyaga hospital ya serikali.
hakuna uzalendo kwenye vitu vibovu na huduma mbovu.
 
Wakutosha kusambaza nchi nzima mpaka vijijini?
Wakutosha kusambaza kwenye hospitali zote zenye sifa ya kuwa na bingwa, huwezi kupelekwa bingwa mahali pasipo na vifaa tiba muhimu
 
Hivi ni Mwanasiasa gani yule aliyesema"Tuna Rais wa ajabu sana kuwahi kutokea"

Haya ni maajabu mengine ya dunia! Kwani huyo daktari aliyekimbila hospitali binafsi, huko aliko anatibu Tumbili au Watanzania walewale?

Hajisikii aibu kuona sekta binafsi inawalipa wafanyakazi wake malipo mazuri,huku yeye akiendelea kuwadhulumu tangu alipoingia madarakani?

Atapata faida gani kumfungia huyo daktari na hiyo hospitali kwa sababu tu ya ubinafsi wake na roho yake mbaya ya kuwadhulumu wafanyakazi stahiki zao kwa miaka zaidi ya sita sasa!!!

Huyu mzee mbona ana mihemko sana!!! Amalize tu muda wake tupumue!!
 
Sasa mkuu hospitali aliyoenda mnaifungia kwa lipi ? kwa roho zako mbaya kama hizi ndio maana watu wengi hawaamini kama wewe ni mtanzania .

Madaktari chungu mzima hawana kazi si wapeni hiyo nafasi muachane na huyo aliyehama , mbona ni rahisi tu !
Jana tu nimesoma habari kuhusu Bodi ya Ushauri kwa Hospitali Binafsi ambayo inafanya kazi kama mamlaka ya usajili/udhibiti wa huduma zitolewazo na hospitali zisizo za serikali.

Habari hiyo inaonesha kuwa Bodi imesajili zaidi ya vituo
Kwani akiwa huko hospitali binafsi, si anarejesha mkopo!? Ama mimi ndiye nimeingia kwenye uwanja wa mpira na shoka!!!
====
Kuna uwezekano mkubwa Rais amenukuliwa vibaya, ngoja nitafute chanzo halisi.
Bilashaka mwenzetu siku zote unaona Magufuli yuko sawa hata usiamini kuwa hayo yametoka kwenye kinywa chake. Endelea kutafuta chanzo cha kuaminika cha habari.
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
makato ya bodi pekee yanachukua 22%ya salary,bado 3%vyama vya wafanyakazi, 5% Pssr, Paye n. k. Umesoma kwa shida halafu, mazingira ya kazi ni hovyo, bora niende kwenye masilah.Tanzania hakuna mzalendo hata mmoja.JPM mwenyewe alipoona ualimu hauna masilahi aliacha kazi ya UALIMU NA KWENDA KUFANYA KAZ NYANZA HUKU AKIJUA AMESOMESHWA NA SERIKALI BURE NA NAULI NA MIKATE WALIPEWA BURE. NA ALIPOONA KAZI YA NYANZA HAINA MASILAHI ALIHAMIA KWENYE SIASA.UBABE HAUSAIDII TUKITAFUTA KWA STAILI HII, ITABID KILA MTU ARUDI KAZINI KWAKE.
 
Km huongezi mishahara watu wafanyaje sasa mzee?? Mambo n magumu on the ground.

Tumekutana na mkunga angali ni vigori
 
Hii thinking ya ajabu sana! Yaani kwa sababu mmempa mkopo 100% ndio haruhusiwi kutafuta kazi yenye maslahi zaidi? Kwani huo mkopo si analipa? Au mikopo wanalipa waliajiriwa serikalini tu?
Nilitaka kuwa upande wake hadi niliposoma maneno yako haya!

Nadhani ndyo maana kasema "...ikiwezekana." Kwa sababu sioni 'iwezekane' kumchukulia hatua mtu anayelipa mkopo wake bila ya matatizo yoyote.

Lakini najua akina 'YEHODA' hapa wanaopewa hiyo amri ya kuchunguza wao hawaoni neno hilo "ikiwezekana", wao wanachojua ni kutimiza amri kwa kutumia ujinga wao kuwa ndio ujuaji.

Hivi huku "private" huyo daktari hahudumii waTanzania?
 
Hakuna ambaye hatoguswa sababu walianziwa wapangaji kufukuzwa kuwa wanachelewesha maendeleo sasa nyumba imebaki familia moja bakora mtindo mmoja! Tano tena yani wapinzani walituchelewesha sana
 
Kwani mkuu kama ni hizo hela si bado anailipa serikali? Kwan amelikimbia deni? Na kama mnajua kumpata daktari tena ni kisanga, sasa kwanini hamyathamini maslahi yao? Kwann hamwathamini??? Alafu daktar alichokifanya amehamia kituo kingne tu ila jukumu atakalolifanya huko aliko n sawa na ambalo angelifanya akiwa serikalin!

Waswahili husema, huwezi kujua umhimu wa tako mpk upate majipu matakoni ndo utajua kumbe tako lina umhimu sana!
Alafu kwani wale walimu wanaofundisha st Francis girls wametoka Kenya?

Private institutions zishajua udhaifu wa serikali thus inatembea mle mle. Serikal ipandishe masilahi uone kama hawatatoka huko sekita binafs kuja serikalini.
Mnajifanya hamjui tatz et
Serikali ingekuwa haijui umuhimu wake ingemsomesha bure?

Nchi inatumia tsh 700 billion kwa mwezi kulipa mishahara tu ya wafanyakazi, serikali hiyo hiyo iwatafutie vifaa tiba na majengo; ni hivi karibuni tu ndio imekuja na bima kujitua baadhi ya mzigo.

Hizo hela mnazotaka watu waongezewe kila siku au ajira mpya zitengenezwe, mnataka funds zitoke wapi? Wakati huo huo amtaki watu wadaiwe kodi.

Kuna taaluma wakubali ni wito, kama unataka kufanya kazi private as M.D wajisomeshe wenyewe basi na waende huko huko private kutafuta practice experience. Lakini uitumie serikali kuvuka daraja ukishafika ulipokusudia uanze ngebe hilo hapana.

The government made them they need to show respect and be loyal..
 
Mitano tena!

Masikini sipati picha huyo doctor huko aliko ana hali gani muda huu... Pengine hii taarifa wameipata familia yake kabla yeye hajaipata
 
🇦𝖑𝖎𝖐𝖚𝖑𝖆 𝖇𝖔𝖔𝖒 𝖑𝖊𝖙𝖚 huyoo
 
Back
Top Bottom