Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Jakaya alisema Daktari anaeona maslahi madogo Serikalini atafute sehemu nyingine kwa roho safi tu akazodolewa,sasa kinekuja chuma ukihama Serikalini tunakufata huko huko ulipo tunakufutia leseni na ki hospitali hicho tunakitia Kufuli
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
Ila jpm ,pesa si hukopeshwa ,na hata akiwa private anaendelea na kulipa deni Kama kawa japo kulimaliza ni mbinde Wana bill kubwa Sana,ili jpm awabane vizuri ,Basi nifyema kuwafutia maden yao huko ,walipokopa wakati wa masomo maana fani yao hugusa maisha yetu moja KWA moja ,then wabane ,vinginevyo tuwaachie uhuru
 
Jakaya alisema Daktari anaeona maslahi madogo Serikalini atafute sehemu nyingine kwa roho safi tu akazodolewa,sasa kinekuja chuma ukihama Serikalini tunakufata huko huko ulipo tunakufutia leseni na ki hospitali hicho tunakitia Kufuli
Mkuu unaafikiana na hiki chuma kwa hili? [emoji30]
 
Tunakoelekea mikopo itawekwa masharti ya "lazima kufanya kazi serikali"
Siyo tunakoelekea bali tangu awali ndivyo ilivyokuwa. Unasomeshwa na serikali; ukihitimu unafanya kazi serikalini au kwenye shirika la umma kufuatana na utakavyopangiwa, kwa miaka mitano kipindi ambacho kinachukuliwa kinatosha kufidia gharama za kukusomesha. Ukitaka kwenda kwinginepo kabla ya utumishi wa miaka mitano ulikopangiwa, ruksa lakini ulipe gharama za kukusomesha. Mtu 'objective' hawezi kukosoa hilo. Agizo la JPM katika bandiko hili linafuata kanuni hii.
 
Jamaa anachoweza ni usimamizi tuu , Ila Sera za uchumi jamaaa ni wa hovyo mnoo, na watanzania wasitegemee lolote Kwa huyu jamaaa...wataendelea kuwa maskini wa kutupwa kadri atakavyoendelea kuwa madarakan....

Kuajiri hatak, kuongeza mishahara hatak , wanaojaribu kujinasua anawagonga nyundo ...., Kwenye kujiajiri huko sasa utitiri wa Kodi mpaka unavuja jasho....

Na still anawatukana wahisani hadharani
 
Anatafuta Dr. aliyekimbia hospital kufuata masilah na mazingira bora ya kazi,anayetoa maagizo yeye pia alikimbia ualimu na kwenda kuwa mkemia kwa kufuata masilah Mazur, licha ya kusomeshwa na serikali buree bila hata kurejesha sh. huku hata nauli na MIKATE wakipewa buree.Mtoa maagizo hajaridhika hapo akaacha ukemia akaingia kwenye siasa kula kwa mrija Sasa, amesahau alipotoka. HAPO NANI NI MZALENDO?
Tangu tuingie "uchumi wa kati" maajabu hayaishi nchini mwetu!! Yeye mwenyewe kakimbia 'njaa' halafu anapata ujasiri wa kuwatafuta wenzake warudi kwenye dhiki na taabu!

Hatushangai kumuona yeye mwenyewe akiishi kama yuko peponi, huku wafanyakazi wakitaabika kwa mshahara ule ule tangu alipoingia madarakani!

Ubinafsi siyo kabisa.
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
Kwani akiajiliwa private huo mkopo hawaukani!?

Kwani kwenye mkataba wa mkopo kunakipengere kimtaka mkopaji lazima aitumikie serikali punde amalizapo chuo?

Huyu mzee huyu jamani.....mbona anatuona watz hatuna tunachokijua!

Watu tupo kimya tu......kwa nini?
 
Mfano.. narudia huu ni mfano..

Wewe ni dokta bingwa wa moyo.

Seriaklini unalipwa 2mil alafu private unaambiwa utalipwa 8mil!

Je utakubali kazi ya private ya 8mil au utaendelea serikalini ambapo unalipwa 2mil?
Hakuna mtu asiyependa hela, udaktari unasoma miaka mitano tena kwa shida, halafu uongezee mwaka wa kukaa kama intern, halafu uende ukasomee uwe mbobezi, sio chini ya miaka miwili.

Jumla miaka 8 unahangaika na elimu ya juu, halafu aje mwanasiasa ambaye anatembelea vieite, posho na kiinua mgongo cha kutosha anihubirie uzalendo 🤬🤬🤬
 
JPM bado ni mtumishi wa umma, amehama idara tuu hajaenda ACT [emoji23][emoji23][emoji23]
Mtumishi namba1 wa serikali
Nadhani kwa mara ya kwanza, leo umegundua mzee wako kuna wakati mihemko inamzidia kiasi cha kushindwa kuidhibiti!!

Yeye mwenyewe kaukimbia ualimu baada ya kuona hauna maslahi! Na hakuna aliyemtafuta, wala kumchukulia hatua. Amefanya daktari wa watu, roho inamuuma!

Kama yeye ni mwamba si aongeze mishahara! Halafu aone kama kuna mtu atakimbilia sekta binafsi! Au anafikiri ni yeye tu na watu wake wa karibu ndiyo wenye haki ya kuishi maisha mazuri!!
 
Back
Top Bottom