Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Unaifungia hospitali binafsi, hujiulizi imeajiri watu wangapi?, je ukishaifungia hao waajiriwa wa hiyo hospitali utawalipa mshahara wewe!?

Serikali yenyewe haina uwezo wakuajiri watu, sekta binafsi zinapojitahidi kuboresha huduma na kutoa ajira kwa waTz mnaziwekea vikwazo kibao.
 
Jamaa anachoweza ni usimamizi tuu , Ila Sera za uchumi jamaaa ni wa hovyo mnoo, na watanzania wasitegemee lolote Kwa huyu jamaaa...wataendelea kuwa maskini wa kutupwa kadri atakavyoendelea kuwa madarakan....

Kuajiri hatak, kuongeza mishahara hatak , wanaojaribu kujinasua anawagonga nyundo ...., Kwenye kujiajiri huko sasa utitiri wa Kodi mpaka unavuja jasho....

Na still anawatukana wahisani hadharani

Kuna watu wanatamani wengine wawe kama mbuzi zizini kwao, wakupangie nini ule uvae unywe na uende wapi! Sema basi tu!
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”

Mawazo ya kipumbavu, kwani huko alipo anahudumia mawe?
 
Siyo tunakoelekea bali tangu awali ndivyo ilivyokuwa. Unasomeshwa na serikali; ukihitimu unafanya kazi serikalini au kwenye shirika la umma kufuatana na utakavyopangiwa, kwa miaka mitano kipindi ambacho kinachukuliwa kinatosha kufidia gharama za kukusomesha. Ukitaka kwenda kwinginepo kabla ya utumishi wa miaka mitano ulikopangiwa, ruksa lakini ulipe gharama za kukusomesha. Mtu 'objective' hawezi kukosoa hilo. Agizo la JPM katika bandiko hili linafuata kanuni hii.
Wewe nawe huna lolote! Bla bla tu nyingi na usukuma wako tu ndiyo unao kusumbua. Unatetea ujinga! Mnapata faida gani nyinyi washamba wa mjini na mlio na mawazo ya kimaskini kwa hizi nguvu nyingi mnazoumia kuwaonea na kuwaumiza raia wema na wasio na hatia?

Halafu unajinasibu eti umesomeshwa na Umoja wa Mataifa! Sasa mbona hujaenda kufanya kazi kwa hao watu wako wa Umoja wa Mataifa walio kusomesha?
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
Kwani wanaenda kusaidia raia wa nchi jirani?
 
Kwanini private isichukue hao?
Hilo swali lako lina majibu ndani yake lakini kumbuka hatukuzaliwa kwa ajili ya kutesena uzalendo siyo kumridhisha mkuu wa nchi,uzalendo ni kulitumikia taifa lako kwa moyo wako wote bila kinyongo chochote au maumivu kutoka taasisi yoyote iwe serikali au private sector.
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
He also left teaching and joined NCU just after university graduation!
 
JPM bado ni mtumishi wa umma, amehama idara tuu hajaenda ACT 😂😂😂
Mtumishi namba1 wa serikali

Kwani huyo daktari amekimbia fani ya udaktari, au amehama tu toka kutibu kwenye sekta ya umma, na kwenda kutibu kutibu watanzania kupitia sekta binafsi? Ingekuwa kahama nchi na hataki kutibu watanzania hapo wangalau. Ulevi wa madaraka ni tatizo.
 
Wapinzani wametuchelewesha sana.

Kuna haja ya kufunga hospitali zote na shule zoote za binafsi.
 
Wala usihamgaike mkuu mleta mada. Wabunge wote wamechoka toka kwenye ajira zao za awali
 
JPM bado ni mtumishi wa umma, amehama idara tuu hajaenda ACT 😂😂😂
Mtumishi namba1 wa serikali
wakati wa ukaguzi wa vyeti feki serikali kupitia waziri Kairuki ilisema wabunge, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri na wote wa nyazifa za kisiasa sio watumishi wa umma hivyo wao hawakuhakikiwa,
halafu huyo daktari hana kosa basi tu ni roho mbaya za binadamu
 
Kule hawatibu watu ?

Wanadaiwa ?, Wamelipa hawajalipa ?, kuliko kufungia hospital / mtu anayetibu watu pia ni rahisi sana kwenye mkataba wa mkopo waseme kwa miaka kadhaa lazima ufanye kazi ya serikali sehemu yoyote utakayopelekwa (hapo mtu anakuwa anabanwa kwa mkataba) sio aina hii ya sheria / maamuzi kutoka kwenye kinywa cha mtu
Kuna tofauti kubwa kati ya kiongozi na mtawala.....
 
Hao madaktari sasa hivi wanatakiwa kujiandaa kupatiwa kesi pendwa ya "UHUJUMU UCHUMI NA UOSHAJI PESA"

Jitu halitaki kuwaongeza watu mishahara huku alitaki pia waame,hii ni roho yabkishetani kabisa
 
Back
Top Bottom