Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Hapa inabidi kuangalia kipi ni kipi. Uzalendo ni kitu kizuri, lakini uzalendo ni kwa kila mtu, na si kwa watu wachache tu. Sis binadamu siku zote tunataka zaidi na bora, kwa hiyi daktari kuhama kwa ajili ya maslahi siyo kukosa uzalendo. Huyu daktari kahamia hospitali binafsi lakini anatibu Watanzania.

Katika hili la uzalendo pia inabidi tuangalie. Kama hakuna sheria inayowalazimisha waliyopata mikopo kuitumikia serkali, basi huyu daktari asilazimishwe, maana hata huo mkopo anaulipa. Sasa kama anaulipa kwa ni alazimishwe kutumikia hospitali ya serkali wakati huo mkataba haukuwepo?

Miaka ya nyumba 60s/70s kulikuwa na sheria ambayo mwanafunzi akisomeshwa anatakiwa aifanyie serkali miaka mitano. Kama serkali inataka hivyo, inatakiwa iiweke hii kama mojawapo ya masharti ya mkopo. Bila hii kuwepo, huwezi kumlazimisha mtu kuitumikia serkali. Tuepuke kutunga sheria kwa midomo yetu. Tuweke hivi vitu wazi na siyo kila kukicha matamko yanatoka ambayo ni sawa na sheria.
Sasa kutumikia miaka mitano hizo ajira zenyewe ili atumikie miaka 5 zipo??
 
Wafanye kama Cuba wanaingia nao mkataba mapema ni waajiriwa wa serikali wanapopokea mkopo wa masomo tu.

Ukienda kufanya kazi private hiyo hospitali inabidi iingie mkataba na serikali yao na kuwalipa asilimia kadhaa ya mshahara wako kila mwaka. Brazil na Venezuela wanaotegemea madaktari wa Cuba ndio wanavyofanyiwa.

Ikitokea daktari bingwa ndio kabisa yaani wakusomeshe, wakupe na experience mpaka uitwe bingwa mtu anaemtaka lazima alipe dau kubwa zaidi; that’s how Cuba manages to keep their highly skilled Drs wanaopokea mishahara midogo compared to the world.
Sasa hivi wahitimu wengi wapo mtaan na wamesomeshwa na mkopo je hapo utawakataza wasiajiriwe private?
Kuna wanafunzi zaidi ya 50,000 kila mwaka wanasomeshwa kwa mkopo je utawasaijisha mikataba lazima waajiriwe serekalini?
 
Kwanini sasa private isichukue hao?
Umekazana na swali lako la ajabu as if private hospitals madaktari wake wote wametoka government. Private inaajiri madaktari waliotoka moja kwa moja masomoni, inaajiri hata waliotoka kufanya kazi hospitali zingine za private, stupid question. Unaongea as if serikali yako inaajiri kila anayetoka shule na kumpa uzoefu, Grow up!
 
Kumbe unastahili kuporomoshewa matusi.
Kwanini mnataka kuongea nyie tuu? Kwani ule uhuru mnaoulilia kila siku ni wa kwenu tuu?

Kama matusi ndio ubingwa Poromosha tuu maana ndio haramu yako, ila ujue yatakuhusu mpromoshaji zaidi ya mporomoshewaji
 
Natamani siku mojaa akutane na kichwa kibovu.....jamaa amjibu nimesomeshwa na jasho la wazazi wangu,sijachukua mkopo kwani kutafta masilahi Ni kuujumu uchumi,nalipa Kodi zotee.....Kuna madaktari kibao ajirini wengine
Mwenye nguvu mpishe...
 
Hakika kuna tatizo
Hii ni thinking ya ajabu sana! Yaani kwa sababu mmempa mkopo 100% ndio haruhusiwi kutafuta kazi yenye maslahi zaidi? Kwani huo mkopo si analipa? Au mikopo wanalipa waliojiriwa serikalini tu?
 
Duh hii sasa ni balaa....mambo kumbe magumu kuliko ninavyoyaona.
Huyo daktari kaumia.

Huyo daktari hana kosa lolote! Serikali haitoi mikopo kwa wanachuo kwa masharti kuwa watafanya kazi kwenye sekta ya umma tu. kwa mara nyingine mkulu ametema mhemuko tu.

Naomba kuelimishwa, hasa na wanaojua sheria kuliko mimi! Ni sheria gani inayomzuia kuacha kazi kwenye sector ya umma na kujiunga na sekta binafsi? Ni kwa sheria ipi Rais anaweza kuifunga shughuli halali na binafsi, eti sababu mtumishi wa umma amejiunga nayo?

Anyways, kuifugia hiyo hospital binafsi anaweza kwa sababu anaweza kutumia wakaguzi wa wizara husika kutafuta sababu za kuifungia na bila shaka wataipata. Wanaweza hata kutumia TRA
 

Kwakuwa tunapenda kuiga mabeberu nimeweka standard framework ya mkataba wa ajira NHS uchukue mfanyakazi wao bila ya ruhusa yao au kuwalipa compensation halafu uone watakachokufanya.

Kwa haraka wale wabishi wapitie page 6 or 8 waone madhara ya kuongea na mtaalamu wao bila ya ruhusa yao au kuchukua mfanyakazi mwenye mkataba nae bila ya idhini yao au kuwalipa fidia.

It costs lots of money to train medical professionals and giving them experience; that’s why they are valuable to any employer.

Sisi watanzania tunatabia ya kuchukulia vitu rahisi sana, serikali yetu imekuwa ya kibepari zaidi kuliko wananchi wanaopiga kelele kudai free market.
 
Back
Top Bottom