Hapa inabidi kuangalia kipi ni kipi. Uzalendo ni kitu kizuri, lakini uzalendo ni kwa kila mtu, na si kwa watu wachache tu. Sis binadamu siku zote tunataka zaidi na bora, kwa hiyi daktari kuhama kwa ajili ya maslahi siyo kukosa uzalendo. Huyu daktari kahamia hospitali binafsi lakini anatibu Watanzania.
Katika hili la uzalendo pia inabidi tuangalie. Kama hakuna sheria inayowalazimisha waliyopata mikopo kuitumikia serkali, basi huyu daktari asilazimishwe, maana hata huo mkopo anaulipa. Sasa kama anaulipa kwa ni alazimishwe kutumikia hospitali ya serkali wakati huo mkataba haukuwepo?
Miaka ya nyumba 60s/70s kulikuwa na sheria ambayo mwanafunzi akisomeshwa anatakiwa aifanyie serkali miaka mitano. Kama serkali inataka hivyo, inatakiwa iiweke hii kama mojawapo ya masharti ya mkopo. Bila hii kuwepo, huwezi kumlazimisha mtu kuitumikia serkali. Tuepuke kutunga sheria kwa midomo yetu. Tuweke hivi vitu wazi na siyo kila kukicha matamko yanatoka ambayo ni sawa na sheria.