Salaam Wakuu,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania-CWT.
Mkutano huo utafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, huku watu wote wakitakiwa kuzingatia na kuchukua tahadhari za kujikinga na Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.
Tayari, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-Takukuru, Mkoa wa Dodoma, imetangaza kuwa itashughulika na watu watakaojihusisha na vitendo vya rushwa katika Uchaguzi huo.
Nitawaletea Updates kwa kila kitakachojiri.
Karibuni.
===
UPDATES:
Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako, Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa mingine na viongozi wengine wengi.
Tayari M.h Rais Magufuli ameshawasili katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambaye tayari kwa ajili ya kuja kufungua Mkutano huu wa Chama cha Waalimu Tanzania ambapo amefika na kuwasalimia na kuwapungia mkono Waalimu wote waliohudhuria.
Wimbo wa Taifa unaimbwa kabla ya Rais kuketi na kufungua mkutano huu.
Kabla ya kukaribishwa Mh. Rais kuzungumza Mkutano huu umeanza kwa maombi kutoka kwa Sheikh na Mchungaji Davidi kalinga ambao wameanza kwa maombi kwa kumshukuru Mungu kisha kuomba amani na furaha katika mkutano huu pamoja na kumuombea Rais na viongozi wengine.
Katibu Mkuu wa chama cha Waalimu ameanza kwa kuzingatia itifaki na kuwatambulisha viongozi mbalimbali waliohudhuria katika Mkutano huu na kisha ameanza kusoma risala iliyoandaliwa.
Risala hii imeanza kwa kumshukuru Rais kwa kukubali kuwa Mgeni Rasmi mkutano huo kisha kumpongeza rais kwa miradi mbalimbali ambayo Rais ameitekeleza katika kipindi hiki cha miaka mitano, Katika sekta ya elimu Rais amepongezwa kwa kuongeza miundo pamoja na samani.
Aidha, katika suala la upandishaji wa mishahara na urekebishaji wa mishahara kwa Waalimu Mh. Rais amepongezwa kwa kuruhusu zoezi la upandishaji mishahara na vyeo kwa zoezi ambalo lilikwama kuanzia mwaka 2014 ambapo inaelezwa kuwa hadi kufikia tarahe moja June 2020 serikali ilikuwa imeongeza mishahara na kuwapandisha vyeo Waalimu wapatao 121, 534.
Aidha kuhusu malimbikozo ya madeni yasiyo ya mishahara Mh. Rais amepongezwa kuwa hadi kufikia December 2019 serikali anayoiongoza ilikuwa imelipa kiasi cha Tsh Bilioni 12.05. Huku malimbikizo ya mishahara yakilipwa.
Aidha, risala hiyo imebainisha changamoto ambazo waalimu wanakumbana nazo ikiwamo ukosefu wa nyumba za waalimu na pia rasala hiyo imemuomba rais kuwapandisha cheo waalimu kundi la waalimu walioajiriwa mwaka 2013/ 2014 wapandishwe cheo katika bajeti ya ya mwaka 2020/2021.
Sambamba na hilo, risala hiyo imemuomba Rais kuongeza ajira kwa waalimu ili kukabiliana na idadi kubwa ya Wanafunzi iliyotokana na kuwa elimu bure.
Zaidi ya hayo, waalimu wamemshukuru kwa tamko lake la kutia moyo ambapo aliwambia watumishi nchini wakiwamo waalimu kuwa ataendelea kulipa mishahara hata kama waalimu watakaa nyumbani kutokana na janga la Corona. Pia, Waalimu wamempongeza Raisi pamoja na Wizara ya Afya kutokana na hatua walizozichukua kupambana na Corona na kuwafanya Wananchi kuondokana na hofu ambayo ni mbaya kuliko Corona yenyewe.
Hotuba ya Rais wa Chama cha Waalimu (Bi. Leah Ulaya)
Ameanza kwa Kumshukuru Rais kutenga muda wake kuhudhuria tukio hilo kama Mgeni Rasmi pamoja na kumpongeza Rais kwa kuendelea kufanikisha na kuendeleza Sekta mbalimbali za kimaendeleo nchini.
Sambamba na hilo, Rais wa Chama cha Waalimu amempongeza Rais kuwa na uthubutu na kuweza kufanya mambo mengi makubwa ambayo wengine yanaonekana ni magumu.
Amekazia kwa kumshukuru Rais kwa upendo wake mkubwa kufuatia Rais kuruhusu Watumishi na Waalimu kuendelea kuwalipwa mishahara japokuwa zaidi ya miezi miwili hawakwenda kazini kutokana na janga la Corona.
Ameongeza kwa kumsifia Rais kwakuwa na Muadilifu, Mtu mwenye Upendo, jasiri, Mtu mwenye utashi, mvumilivu, Mchapakazi na mcha Mungu
HOTUBA YA RAIS MAGUFULI
Rais ameanza kuwashukuru Vingozi wote kwa kuhudhuria Mkutano huu. Kisha ameanza kwa kutoa Nukuu ya za wanafalsafa ili kuonesha namna ambavyo waalimu wana umuhimu katika maisha ya Wanaadamu.
Sambamba na hilo, amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kuwakutanisha katika viwanja hivyo. Vilevile RaisMagufuli amemshukuru Rais wa chama cha Waalimu kwa kumpa heshima na kumualika katika Mkutano huu. Raisi amesema kuwa "Hii inadhihiriwa kuwa bado Waalimu wenzangu wanamkumbuka". Raisi ameeleza kuwa anatambua kuwa mkutano huo ni muhimu sana katika kufanya uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Waalimu Taifa.
Aidha, katika suala hili Rais Magufuli amesema "kusema ukweli nisingependa hata kidogo nionekane kuwa napiga Chapuo kwa Mgombea yoyote, hata hivyo nukweli lazima usemwe".
"Uongozi huu wa CWT ambao unamaliza muda wake umejenga uhusiano mzuri sana na Serikali nanayoiongoza. Na hili nasema kwa Dhati bila upendeleo"