Rais Magufuli afungua mkutano Mkuu wa Chama cha Waalimu, Corona imeisha, Shule za Msingi kufunguliwa karibuni

Kuna watu tulishapanda madaraja kitambo tangu zaidi ya mara mbili enzi za JK! Hivyo hatutishiki kabisa. Na mwaka huu ameahidi muda huu atapandisha madaraja.

Hilo ndilo jambo tunalotaka. Siyo mambo ya kununua ndege kila siku.
amesema atapandisha kwa asilimia ngapi
 
Kampeni ya Kisiasa, JPM anapiga kampeni !
Anajishuku na kurudia zaidi ya mara tatu "sipigi kampeni"
 
Nikuulize wewe hukufundishwa na hawa wenye kazi ya kuzimu? Yawezekanaje huna watoto na siku ukipata watoto hutawapeleka wakafundishwe na hawa waalimu unaowadharau kiasi hili na kuona heri ya muuza maembe? Kwa vile umefundishwa Sasa unajiona mjanjaa. Waalimu hawana njaa Kama unavyofikiri. Waalimu wengi Wana maisha mazuri kuliko watu wengi mitaani, wengi wamejenga nyumba zao na wana usafiri binafsi wa magari ambapo huyo muuza maembe wako unayemsifia.
Acheni kudharau waalimu na kulinganisha na watu wa ajabu ambao hata wajikusanye vipi hawawezi kumualika rais awe mgeni rasmi kwenye shughuli yao
Acheni kupinga pinga kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umekosea sana asee
Wew unafanya kazi gani? Ungekuwa unajiamini wala usingetumia fake ID na watu wenye pesa zao wala hawana muda wa kubanana huku jf, wametulia zao kule twita.
Kwa hyo twitter ni patulivu kuliko jf siku hzi au

Punguza bangi bro!
 
Ukweli ni kuwa walimu hawajitambui,jiwe hakupaswa kualikwa ila Kwa sababu ni lazima aalikwe ndio mana yuko hapo,MTU kashindwa kuwaongezea mishahara,wastaafu hawajapara pension zao,unamwalika Wa nini?huyu ni kiongozi asiye na utu alipaswa kupuuzwa siku zote.
 
amesema atapandisha kwa asilimia ngapi

Hajataja ongezeko la mshahara! Ameongelea upandishwaji wa madaraja. Na hapa ndiyo wengi tunahitaji. Enzi za JK kila baada ya miaka 3 mfanyakazi alipandishwa daraja na hivyo mshahara wake kuongezeka.

Huyu wa sasa anatuweka mpaka miaka 5! Hapa ndipo penye tatizo. Kwa hiyo kama atapandisha tena madaraja mwaka huu, wafanyakazi tutapata unafuu. Kwenye mshahara anaweza kutudanganyia kwa hela ndogo tu, ila kwenye daraja kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake.
 
Mkuu unaongea as if wewe ndiyo msemaji wa rais ?
 
Kama kuna vyama ambavyo sioonagi ni jamboa hani la maana wanalifanya ni hiki CWT.hivi huwa wanapelekaga wapi michango kutoka kwa waalimu wote nchi nzima.naona ni chama kinachoongoza kwa kipato cha uhakika.Nadhani walitakiwa kuweka hadharani taarifa za mapato na matumizi iliyokaguliwa
 
sisi huku MAHAKAMANI na mawizarani huingii kama huna BARAKOA, nasema huingii
 
"Uongozi huu wa CWT ambao unamaliza muda wake umejenga uhusiano mzuri sana na Serikali nanayoiongoza. Na hili nasema kwa Dhati bila upendeleo" Mh. Magufuli.

Walimu bana
 

Ameahidi Wafanyakazi wenye sifa ya kupanda madaraja, watapandishwa mwaka huu, amegusia kuhusu CWT kuwaondolewa 2% ya ada ya makato kwa wanachama wake, amegusia matatizo ya Benki ya Walimu kurekebisha changamoto zake ili iwe na tija kwa wanachama wake, nk.

Kiufupi kuna matumaini.
 
Corona tushaishinda.
Hata kasahau mask inatamkwaje kiswahili
🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…