Rais Magufuli alipendwa lakini sasa watu wamemkinai kwa itikadi yake

Kibinafsi nilimkubali sana huyu mzee, nilipenda amri zake nilipenda mabadiliko yake nilipenda uchapakazi wake na misimamo yake pia.

Japo kuwa katika utafiti wa mwaka 2015 asilimia kubwa ya watanzania walipenda apatikane raisi mkali lakini huyu msukuma kazidi sana.

Kila mtu anajionea matukio yote ya ziara zake anazodhalilisha viongozi na watendaji wengine kiasi kwamba hakuna wa kumfanya kitu.

Chuki yake dhidi ya jamii ya watu wa kaskazini ni mbaya sana. Kila anaetoka ukanda huo anamuona mwizi na haaminiki katika jamii.

Maneno yake na serikali yake yanathibitisha hilo. Akumbuke nae atakuwa na mwisho wa utawala vipi kama jamii yake ikijatengwa katika utawala wake?

Akiwa kama rais anapaswa kuwa na hekima, busara na heshima ili kuwa kama mfano kwa viongozi wengine.

Ni hayo tu mwenye nyongeza karibu
Umerashiarashia tu mkuu wangu 'kibosho'.

Hii ni uliyotoa hapa ni jumla jumla mno, kiasi kwamba haimpi msomaji sababu hasa kwa nini amekukinai.

Ukali tu..., mbona hilo wengi wasingejali kama ukali huo ungetenda haki. Hao wapuuzi na wazembe na manafiki hakuna yeyote anayewapenda, na sote tungeshangila ukali wake huo kwa hao watu wake.

Kuna mambo ya msingi zaidi kuliko hayo uliyoorodhesha kijumla jumla tu.

Mambo yanayoumiza wengine bila ya sababu za msingi wowote.

Tatizo lake la kwanza kabisa linalompa shida ni kupenda kusifiwa (kupenda sifa), aonekane yeye ndiye kabisa, na katika kutafuta hizi sifa matokeo yake ndiyo hayo ya kuumiza watu wengine hata bila ya sababu za maana.
Chukulia siku za mwanzo za utawala wake, jinsi watu walivyoanza kuingia matatani kwa sababu tu ya kumhusu yeye.

Unakumbuka jamaa aliyewekwa kifungoni miezi sita kwa kuropoka tu "Rais kitu gani?" au umesahau? Akina Lema na ndoto zao, unakumbuka?

Usiniambie yeye hakuyasababisha hayo, ni wapambe wake! Bila ya yeye kuyapa baraka hayawezi yakatokea.

Yote hayo, kwa bahati mbaya sana yakapelekea akina Ben Saanane kupotea hadi leo hii. Na watu wakawa wanatekwa bila sababu za maana.

Wengi wakaanza kujua tokea hapo kuwa huu ni utawala tofauti na nyingine zilizopita.

WaTanzania wengi, walikuwa mwanzo na ari kweli ya kuitikia ombi lake "Mniombee" na makamera kila sehemu makanisani, kila Jumapili na kwa wale wachungaji/mabishop Mwingira au Lusekero sikumbuki, na ahadiza kujengewa barabara hadi kanisani kwao.
Wengine malori ya simenti, yakionyeshwa kwenda kujenga makanisa!

Yote haya yalikuwa ya nini? Sifa

Lakini baadhi ya hayo sio taabu, binaadam yeyote hupenda kusifiwa kwa kiwango chake, hasa kama anastahiri sifa hizo.

Mstuko mkubwa kwa wengine ulianza alipoanza kujiona yeye yupo juu ya Katiba, sheria na kukiuka taratibu za kufanya mambo.
Ndiyo, yeye kama rais anao uwezo wa kubadili baadhi ya mambo anayoona hayamsaidii kufanya kazi. Lakini kuna taratibu za kuyabadili mambo haya. Sio tu kwa yeye kujiamria na kuwa hivyo.

Kama ni sheria kubadili sheria, kazi ya bunge ni nini, na huku chama chake ndio chenye wabunge wengi, anaogopa nini kufuata taratibu katika hilo.

Mara, bunge likawekwa gizani, mikutano na shughuli za vyama vya upinzani ikawa marufuku, huku yeye ndie akabaki kinara kila sehemu. Hata kwenye sehemu za shughuli za serikali, yeye anaingiza mambo ya chama chake TBC ikawa mali yake, ya kumtangaza kila sehemu.

"Wewe washughulikie huko (bungeni) wakija huku nje mimi nitawashughulikia," unayo kumbukumbu ya usemi huo, na ulielewa maana yake?

Kiongozi mchapa kazi, watu wanafurahia, au bado wanaona matumaini ya kazi zako, haya ya pembeni yanakuhusu nini!

Kazi nzuri itaonekana na watu watakupenda, haya marasharasha ya nini. Kuwatisha na kuwatia watu woga kunasaidia upendwe?

Sasa tena ni haya ya kukumbushana" Mimi nimejitoa maisha yangu....". Sawa, huna sababu yoyote ya kuhimiza watu wakumbuke.
Kazi zako zitajisemea zenyewe, lakini hata ufanye kazi nzuri kiasi gani huku mioyo ya watu ukiisononesha, ni kazi bure kukumbusha

Hizi barabara, reli, madege na makorokocho mbalimbali hayawezi kamwe kununua HAKI na UHURU wa watu.

Kulikuwa na biashara za watumwa enzi zile, baadhi ya wenye mali za watumwa hao walikuwa wanawapa mazingira mazuri katika utumwa wao. Nguo, malazi n.k. Haya yote hayakuweza kuwafanya watumwa wale wasahau hali yao duni ya kukosa haki na uhuru wa kuamua mambo yao.

Leo hii ukimnyima mTanzania HAKI ya kumchagua kiongozi anayemtaka yeye mwenyewe, kwa njia mbali mbali kama kutumia mabavu ya polisi au Tume ya uchaguzi, mTanzania huyu anayo tofauti gani na wale watumwa.

Ndio, barabara ni nzuri, zitawawezesha wananchi kufanya shughuli zao mbalimbali kwa ufanisi zaidi, lakini hapo hapo unawakandamiza eti uwaletee hizo barabara, kwa hiyo wanyamaze wakubali tu hizo barabara zije?

Sijapata taarifa za wale watu wa Jimbo la Singida Mashariki walionyang'anywa mbunge wao kwa nguvu kwa ahadi ya kuletewa huduma ya maji. Sijui kama waTanzania wale wanayo furaha kubwa kwa kuletewa huduma hiyo kwa bei ya uhuru wao wa kumpata kiongozi wanayetaka awaongoze jimboni kwao.

Hili nalo kweli linastahiri Rais kupewa sifa za uongozi bora kwa kufanya vile?

Rais Magufuli angeweza kuwa Rais mzuri sana kwa juhudi za kazi zake anazozifanya. Laiti kama angekazia sana kwenye hizi kazi zake na haya mambo ya pembeni yasiyokuwa ya lazima, hata kama yangetokea kiasi, kazi hizo zingezungumza kwa nguvu zaidi kuliko njia nyingine yoyote.

Sasa angalia, tunu yetu ya taifa mhimu kabisa, "Umoja wa Taifa letu" imo mashakani kabisa. Kwa nini? Inatusaidia nini enzi hii kwenda kwenye mikutano ya hadhara na kuanza kuzungumza kilugha! Ni wapi sehemu yoyote ya nchii pasipoeleweka lugha yetu adhimu ya kiswahili.?
Tunazunguza kilugha ili iweje? Tumwone mwenzetu yupo kwenye madaraka makubwa? Yatatusaidia nini hayo madaraka yake makubwa.
Nasi tunataka kuwaiga Kenya? Kuna kitu gani cha kufurahisha hapo, au cha kukumbukiwa nacho ukiwa kiongozi wa nchi iliyopiga hatua nzuri kabisa katika eneo la kuondokana na mambo ya kutenganisha watu wako ndani ya taifa lako!

Ngoja nimalize kwa kukumbushia kazi ambayo wengi tungedhani ni kazi nzuri ameifanya, hata kama kaifanya kwa njia za vurugu ambazo hazikustahiri iwe hivyo.
Mali za taifa letu hili kwa kweli zilistahiri kupewa ulinzi imara. Accacia na Barrick tumewaona. Mabadiliko yale pamoja na kuwa na vurugu zake, na hata akina Lissu kuwa vile, lengo lilikuwa ni zuri na mategemeo ni kwamba tutaambulia kitu huko, tukizingatia na sheria zilzobadilishwa

Mahusiano ya kimataifa, ni jambo mhimu kwa kiongozi mkuu kutolitilia maanani...,

Nilisema nimalizie
 
Huwez kuleta utani kwenye mambo halisi,heb wazia ww una udhaifu fulani kwa mwili wako afu mtu autumie kukutania utajisikiaje? (Heb nenda kamtanie Manara kuwa yeye ni Zeru Zeru ngozi yake ni dili) tuone hapo atajiskiaje.

Utani mwingine unaenda na uhalisia
Utani tu hule do not take it seriously!
Mchagga mpe mke wako amsindikize atamfikisha mpaka nyumbani ila sio hela mama mamaaa ,mfano wazee wa Rombo hawana time na mademu wala wanawake wao ni kusaka pesa kula tungi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mngoni mpe hela atazifikisha ila sio mke babaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ila utani huu una ukweli 95% kwa hiyo wachagga mtulie kwny utani wa kikabila msilete ukabila.
Wengi najua ni watoto wa 1990's hamjui km kuna mambo ya utani.
Wahenga walisema linalotoka mdomoni ndilo lililokuwa moyoni mwake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
U
Kibinafsi nilimkubali sana huyu mzee, nilipenda amri zake nilipenda mabadiliko yake nilipenda uchapakazi wake na misimamo yake pia.

Japo kuwa katika utafiti wa mwaka 2015 asilimia kubwa ya watanzania walipenda apatikane raisi mkali lakini huyu msukuma kazidi sana.

Kila mtu anajionea matukio yote ya ziara zake anazodhalilisha viongozi na watendaji wengine kiasi kwamba hakuna wa kumfanya kitu.

Chuki yake dhidi ya jamii ya watu wa kaskazini ni mbaya sana. Kila anaetoka ukanda huo anamuona mwizi na haaminiki katika jamii.

Maneno yake na serikali yake yanathibitisha hilo. Akumbuke nae atakuwa na mwisho wa utawala vipi kama jamii yake ikijatengwa katika utawala wake?

Akiwa kama rais anapaswa kuwa na hekima, busara na heshima ili kuwa kama mfano kwa viongozi wengine.

Ni hayo tu mwenye nyongeza karibu
UNAMCHUKIA PEKEE YAKO NA WENZAKO.SISI HATUKUWA NA BARABARA YA LAMI, UMEME NA SASA TUNAO TUTAMCHUKIA KWANINI.MMETUIBIA SANA NYIE NGOJA AWANYOOSHE KWANZA
 
[emoji122][emoji122][emoji122] asante mkuu kwa kumaliza kona kabisa. Ndio mana niligusia kijuu juu juu ya hisia za watz wengi saiv kwanzia watumishi hadi wananchi wanavyomchoka huyu mzee

Mwingine anaweza kuendeleza yaliyosahaulika
Umerashiarashia tu mkuu wangu 'kibosho'.

Hii ni uliyotoa hapa ni jumla jumla mno, kiasi kwamba haimpi msomaji sababu hasa kwa nini amekukinai.

Ukali tu..., mbona hilo wengi wasingejali kama ukali huo ungetenda haki. Hao wapuuzi na wazembe na manafiki hakuna yeyote anayewapenda, na sote tungeshangila ukali wake huo kwa hao watu wake.

Kuna mambo ya msingi zaidi kuliko hayo uliyoorodhesha kijumla jumla tu.

Mambo yanayoumiza wengine bila ya sababu za msingi wowote.

Tatizo lake la kwanza kabisa linalompa shida ni kupenda kusifiwa (kupenda sifa), aonekane yeye ndiye kabisa, na katika kutafuta hizi sifa matokeo yake ndiyo hayo ya kuumiza watu wengine hata bila ya sababu za maana.
Chukulia siku za mwanzo za utawala wake, jinsi watu walivyoanza kuingia matatani kwa sababu tu ya kumhusu yeye.

Unakumbuka jamaa aliyewekwa kifungoni miezi sita kwa kuropoka tu "Rais kitu gani?" au umesahau? Akina Lema na ndoto zao, unakumbuka?

Usiniambie yeye hakuyasababisha hayo, ni wapambe wake! Bila ya yeye kuyapa baraka hayawezi yakatokea.

Yote hayo, kwa bahati mbaya sana yakapelekea akina Ben Saanane kupotea hadi leo hii. Na watu wakawa wanatekwa bila sababu za maana.

Wengi wakaanza kujua tokea hapo kuwa huu ni utawala tofauti na nyingine zilizopita.

WaTanzania wengi, walikuwa mwanzo na ari kweli ya kuitikia ombi lake "Mniombee" na makamera kila sehemu makanisani, kila Jumapili na kwa wale wachungaji/mabishop Mwingira au Lusekero sikumbuki, na ahadiza kujengewa barabara hadi kanisani kwao.
Wengine malori ya simenti, yakionyeshwa kwenda kujenga makanisa!

Yote haya yalikuwa ya nini? Sifa

Lakini baadhi ya hayo sio taabu, binaadam yeyote hupenda kusifiwa kwa kiwango chake, hasa kama anastahiri sifa hizo.

Mstuko mkubwa kwa wengine ulianza alipoanza kujiona yeye yupo juu ya Katiba, sheria na kukiuka taratibu za kufanya mambo.
Ndiyo, yeye kama rais anao uwezo wa kubadili baadhi ya mambo anayoona hayamsaidii kufanya kazi. Lakini kuna taratibu za kuyabadili mambo haya. Sio tu kwa yeye kujiamria na kuwa hivyo.

Kama ni sheria kubadili sheria, kazi ya bunge ni nini, na huku chama chake ndio chenye wabunge wengi, anaogopa nini kufuata taratibu katika hilo.

Mara, bunge likawekwa gizani, mikutano na shughuli za vyama vya upinzani ikawa marufuku, huku yeye ndie akabaki kinara kila sehemu. Hata kwenye sehemu za shughuli za serikali, yeye anaingiza mambo ya chama chake TBC ikawa mali yake, ya kumtangaza kila sehemu.

"Wewe washughulikie huko (bungeni) wakija huku nje mimi nitawashughulikia," unayo kumbukumbu ya usemi huo, na ulielewa maana yake?

Kiongozi mchapa kazi, watu wanafurahia, au bado wanaona matumaini ya kazi zako, haya ya pembeni yanakuhusu nini!

Kazi nzuri itaonekana na watu watakupenda, haya marasharasha ya nini. Kuwatisha na kuwatia watu woga kunasaidia upendwe?

Sasa tena ni haya ya kukumbushana" Mimi nimejitoa maisha yangu....". Sawa, huna sababu yoyote ya kuhimiza watu wakumbuke.
Kazi zako zitajisemea zenyewe, lakini hata ufanye kazi nzuri kiasi gani huku mioyo ya watu ukiisononesha, ni kazi bure kukumbusha

Hizi barabara, reli, madege na makorokocho mbalimbali hayawezi kamwe kununua HAKI na UHURU wa watu.

Kulikuwa na biashara za watumwa enzi zile, baadhi ya wenye mali za watumwa hao walikuwa wanawapa mazingira mazuri katika utumwa wao. Nguo, malazi n.k. Haya yote hayakuweza kuwafanya watumwa wale wasahau hali yao duni ya kukosa haki na uhuru wa kuamua mambo yao.

Leo hii ukimnyima mTanzania HAKI ya kumchagua kiongozi anayemtaka yeye mwenyewe, kwa njia mbali mbali kama kutumia mabavu ya polisi au Tume ya uchaguzi, mTanzania huyu anayo tofauti gani na wale watumwa.

Ndio, barabara ni nzuri, zitawawezesha wananchi kufanya shughuli zao mbalimbali kwa ufanisi zaidi, lakini hapo hapo unawakandamiza eti uwaletee hizo barabara, kwa hiyo wanyamaze wakubali tu hizo barabara zije?

Sijapata taarifa za wale watu wa Jimbo la Singida Mashariki walionyang'anywa mbunge wao kwa nguvu kwa ahadi ya kuletewa huduma ya maji. Sijui kama waTanzania wale wanayo furaha kubwa kwa kuletewa huduma hiyo kwa bei ya uhuru wao wa kumpata kiongozi wanayetaka awaongoze jimboni kwao.

Hili nalo kweli linastahiri Rais kupewa sifa za uongozi bora kwa kufanya vile?

Rais Magufuli angeweza kuwa Rais mzuri sana kwa juhudi za kazi zake anazozifanya. Laiti kama angekazia sana kwenye hizi kazi zake na haya mambo ya pembeni yasiyokuwa ya lazima, hata kama yangetokea kiasi, kazi hizo zingezungumza kwa nguvu zaidi kuliko njia nyingine yoyote.

Sasa angalia, tunu yetu ya taifa mhimu kabisa, "Umoja wa Taifa letu" imo mashakani kabisa. Kwa nini? Inatusaidia nini enzi hii kwenda kwenye mikutano ya hadhara na kuanza kuzungumza kilugha! Ni wapi sehemu yoyote ya nchii pasipoeleweka lugha yetu adhimu ya kiswahili.?
Tunazunguza kilugha ili iweje? Tumwone mwenzetu yupo kwenye madaraka makubwa? Yatatusaidia nini hayo madaraka yake makubwa.
Nasi tunataka kuwaiga Kenya? Kuna kitu gani cha kufurahisha hapo, au cha kukumbukiwa nacho ukiwa kiongozi wa nchi iliyopiga hatua nzuri kabisa katika eneo la kuondokana na mambo ya kutenganisha watu wako ndani ya taifa lako!

Ngoja nimalize kwa kukumbushia kazi ambayo wengi tungedhani ni kazi nzuri ameifanya, hata kama kaifanya kwa njia za vurugu ambazo hazikustahiri iwe hivyo.
Mali za taifa letu hili kwa kweli zilistahiri kupewa ulinzi imara. Accacia na Barrick tumewaona. Mabadiliko yale pamoja na kuwa na vurugu zake, na hata akina Lissu kuwa vile, lengo lilikuwa ni zuri na mategemeo ni kwamba tutaambulia kitu huko, tukizingatia na sheria zilzobadilishwa

Mahusiano ya kimataifa, ni jambo mhimu kwa kiongozi mkuu kutolitilia maanani...,

Nilisema nimalizie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba niongee kitu ambacho kipo mitaani na mtazamo wa watu wengi ikiwemo Mimi, Rais Magufuli anapendea na anakubalika sana. Hapa nimetoa mtazamo, maoni na matarajio ya wengi lakini maoni ya wachache kama yako yaheshimiwe.
Huo ni mtazamo wako finyu
 
tindo
Hebu tujiulize swali moja jepesi, hivi kuna mantiki yoyote kwa kiongozi anayependwa na wananchi wake, kuwa na ulinzi wa "kufuru" alio nao Rais wetu?

Hilo haliwezekani, kimsingi hapendwi ila angependa sana apendwe. Hivyo wapambe na watu mbalimbali wanaimbisha watu kuwa anapendwa ili itokee watu kumpenda kweli.
 
magu anakubalika sana acha porojo aisee, nimekatiza mikoa mingi kila kona nikidadisi naambiwa jamaa amekaza ila yupo freshi anapiga kazi. wanasema kweli amekaza ila wanamkubali, kwa ujumla anakubarika sana, amini usiamini ndio hivyo
watu wanataka hata Corona ifanye yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afu kusema rais anachuki na wachaga ni kumkosea heshima na kukosa shukran na mawazo hayo ni theoretical tu hakuna practical case instead kawapelekea tren

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom