Rais Magufuli amteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi nchini Uingereza

Rais Magufuli amteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi nchini Uingereza

Mama yetu huyu anapenda sana nafasi za kuteuliwa mweee jamani, yaani yeye kusema ajaribu angalao hata kugombea ubunge wa jimbo wapi, anasubiri dezo tu jamani
Na sikia tu dezo lkn gharama yake usipime!
 
Huna lolote
Mjipange kuzungusha viouno 2020
Maana ndio mjualo
Wewe unawaza 2020 wakati wenzio wanawaza foleni zilizoanza za kununua sukari kwa mgawo?
Nchi ya viwanda sukari kwa foleni? Miezi sita tuu chali! Kila ukiuliza kitu ni eti majipu kwanza! watu watakula majipu? bilalifulu
 
Wewe unawaza 2020 wakati wenzio wanawaza foleni zilizoanza za kununua sukari kwa mgawo?
Nchi ya viwanda sukari kwa foleni? Miezi sita tuu chali! Kila ukiuliza kitu ni eti majipu kwanza! watu watakula majipu? bilalifulu
Mkuu huyo Mzuka hajitambui
 
Kutoka naibu Katibu Mkuu UN hadi kuwa balozi ni free fall. Kama sio ni kwa ajili ya njaa sidhani kama kuna motivation nyingine kwa huyo mama kukubali hiyo post. Wazo la kustaafu kwa heshima ni gumu sana kueleweka kwa hawa jamaa
Watu kama hao kustaafu sahau, hapo hata kama angepewa ukuu wa wilaya au mkoa angekimbia haraka sana kwenda huko, muda mwingine njaa.
 
ASHA Rose Migiro, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), muda wowote kuanzia sasa, atatangazwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,anaandika Faki Sosi.

Taarifa za ndani kutoka katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa zinaeleza kuwa, jina la Dk. Migiro ambaye aliwahi kutumikia nafasi mbalimba ndani na nje tayari limefikishwa Uingereza kwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Februari mwaka huu Rais John Magufuli kutangaza kwamba, Dk. Migoro atateuliwa kuwa balozi bila kutaja nchi atakayokwenda kuiwakilisha Tanzania.

Uteuzi wa Dk. Migoro uliibua mjadala kutokana na kushika kwake nafasi mbalimbali za kidiplomasia ambapo mjadala huo ulijielekeza kuwa ‘ameshuka ama amepanda?’

Miongoni mwa nafasi za juu za kidiplomasia alizowahi kushika Dk. Migiro ni pamona na kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).

Aliteuliwa tarehe 5 Januari 2007. Dk. Migiro aliteuliwa na Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) kushika nafasi hiyo akiwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo baada ya Louise Fréchette, mwanadiplomasia wa Canada aliyeongoza kuanzia Aprili 1997 hadi Aprili 2006.

Dk. Migiro alichukua nafasi hiyo iliyoachwa na George Mark Malloch Brown wa Uingereza. Dk. Migiro alishikilia wadhifa huo kwa miaka mitano. Julai 2012 nafasi yake ilichukuliwa na mwanadiplomasia wa Sweden, Jan Elliason.

Mapito ya Dk. Migiro

Dk. Migiro alizaliwa tarehe 9 Julai 1956 katika Wilaya ya Songea, Ruvuma. Alisoma Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, Dar es Salaam mwaka 1963 hadi mwaka 1966.

Dk. Migiro alihamia Shule ya Msingi Korogwe, Tanga ambapo aliendela na elimu ya msingi mwaka 1967–1969.

Baadaye akajiunga kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Weruweru, Kilimanjaro mwaka 1970 hadi 1973 na Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari Korogwe mwaka 1974 -1975.

Dk. Migiro alikuwa mmoja wa wasichana waliofaulu vizuri Korogwe Sekondari na alipojiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1977, alichukua masomo ya sheria na kuhitimu Shahada yake (LLB) mwaka 1980.

Baadaye aliajiriwa UDSM kufundisha masomo ya sheria kama Mhadhiri Msaidizi. Alifanya kazi hiyo kwa miaka miwili kabla ya kuendelea tena na masomo ya juu ya sheria mwaka 1982–1984 hapohapo UDSM na kutunukiwa shahada ya uzamili (LLM).

Kati ya mwaka 1985–1988, alifundisha UDSM. Mwaka 1988 alikwenda Chuo Kikuu cha Konstanz, Ujerumani ambako alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika masuala ya Sheria mwaka 1992.

Dk. Migiro alirejea Tanzania akiwa Mhadhiri Mwandamizi na aliendelea kufundisha katika Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi mwaka 2000 alipoingia kwenye siasa.

Akiwa UDSM kati ya mwaka 1992 – 1994 Dk. Migiro alikuwa Mkuu wa Idara ya Sheria za Katiba na Utawala.

Kati ya mwaka 1994 – 1997 aliongoza Idara ya Sheria za Makosa ya Jinai (Idara zote zipo katika Kitivo cha Sheria UDSM).

Dk Migiro ni mzungumzaji mzuri katika lugha ya Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani. Ni mke wa Profesa Cleophas Migiro na wana watoto wawili wa kike.

Dk Migiro alianza na siasa za kujijenga akitokea katika taaluma. Mwaka 2000, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alimteua kuwa waziri kwenye Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.

Alitumikia wadhifa huo hadi mwaka 2005 bila kubadilishwa akisimamia mambo mengi ya kisera na kimiundombinu, bila kusahau utekelezaji na upiganiaji wa haki za wanawake na watoto.

Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005, alimteua kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje, Januari 2006 na kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia wadhifa huo. Katika kipindi cha mwaka mmoja tu, alifanya kazi nyingi za kimataifa zilizomweka katika anga nyingine kisiasa.

Januari 5, 2007, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu (UN) mpaka 2012 alipomaliza muda wake. Januari mwaka 2013, Dk Migiro aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Desemba 2013 aliteuliwa kuwa mbunge katika Bunge la Tanzania.

Januari 2014 aliteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Katiba, nafasi ambayo alidumu nayo mpaka Rais Kikwete alipomaliza muda wake mwaka jana.
Mbona hiyo nafasi ya naibu katibu mkuu wa un,hakukaa sana?je ni kitu gani kilimtoa mapema?au aliamua mwenyewe kuachia ngazi?
 
The best option was to go and lecture as UDSM....let this political ego fade. Ni muda wa kuelimisha kuliko kua balozi.
 
Kutoka naibu Katibu Mkuu UN hadi kuwa balozi ni free fall. Kama sio ni kwa ajili ya njaa sidhani kama kuna motivation nyingine kwa huyo mama kukubali hiyo post. Wazo la kustaafu kwa heshima ni gumu sana kueleweka kwa hawa jamaa
Kuna habari kuwa huyo mama hajawahi kuchaguliwa na wananchi kwenye cheo chochote, hata mjumbe wa nyumba kumi na hii inanyesha kuwa anaishi maisha ya kuvizia kama mshambuliaji
 
Mama yetu huyu anapenda sana nafasi za kuteuliwa mweee jamani, yaani yeye kusema ajaribu angalao hata kugombea ubunge wa jimbo wapi, anasubiri dezo tu jamani
Mkuu hiyo nafasi ya ubunge ni ya juu sana kwake ungesema labda ujumbe wa nyumba kumi tu au mkuu wa sungu sungu
 
It is only in africa where a person can walk 100 steps ahead and go back 150 steps and praises him/herself that he/she is improving
Mkuu mwenye njaa hachagui aina ya chakula
 
Kwasasa hamueleweki mnasimamia hoja ipi
Kama matukio ndio hakuna
Kuropoka Bungeni hakuna

Mnajirekodi !!!
Kweli waliopo Chamanzi na kinokia cha tochi atajua nini[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Kama mlivyo Fanya kwenye Sera ya CDM
Itapatikana mitandaoni
Mmerudia tena na bunge

Mnahali Mbaya sana
Tatizo kutegemea MAZERO kuongoza chama[emoji12] [emoji12] [emoji12]
Wasaliti wenzako wanasubiri kuburuzwa kwa pilato kwa kushawishi kupewa kitu kidogo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom