Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?

Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?

Mhe. Rais naona ameumaliza mzizi wa fitina leo katika mazishi ya Balozi Kijazi na kusema kuwa magonjwa yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, na sisi si pekee ndiyo tunaotaabika na matatizo haya ya magonjwa ya milipuko hata nchi zingine wamekufa wengi sana. Na tatizo linapokuwa kubwa kuzidi uwezo wa binadamu tulisogeze kwa Mungu.

Rais anasema mwaka jana tulimuona Mungu akitusaidia lakini sasa naona wengine hawana imani tena wanatengeneza taharuki na kutishana mimi sifanyi lokudauni tuchape kazi Mungu yupo. Kwanini au amwamini kuwa Mungu anaweza kuishinda Korona?

Mimi mtoto wa mchungaji nahoji hivi hawa baadhi ya viongozi wa dini ambao nao pia wanaogopa Corona kiasi cha kwamba wanatushauri tuwasikilize watu wa afya na wamitandaoni hivyi hawa watumishi wa Mungu si wangeacha hiyo kazi na kuja huku mchangani ijulikane moja.

Nawauliza na ninyi wana janvi Mungu yupo au, maana babuzetu waliomba mvua zilinyesha, waliomba nzige waondoke asubui waliwakuta chali kificha mende, magonjwa ya mlipuko hayakuwagusa, hivi na yule Mungu wa babu zetu yupo wapi siku hizi na huyu wa kanisani na msikitini yupo wapi.
Corona ipo haipo
 
Mambo mengine ni kutumia akili kidogo tu....
Wakatoliki OG wamekuja na tamko kama hili, sasa we endelea kumsikiliza mtu mmoja anaejifanya ana imani kuliko watu wote ulimwenguni.
 
Mmh kwamba yeye kashakuwa injected?
Nimesema "si ajabu", Inawezekana maana uwezo wa kuwa injected anao na ni mkubwa. kama alituma ndege Madagascar, kutuma ndege China/ Uingereza/USA anashindwa? walituma ndege wakanywa wao peke yao, kwanini hili nalo asifanye?
 
Mbona mnachagua maneno machache na kuacha mengine?

Wakati anasema hayo unayoyataja, kasema pia yeye hawezi kuleta lockdown kwani mwaka jana “tuliomba na maombi yakapokelewa”

Yaani hujaelewa tu?
 
Lazimaa tutubu ili kuwee na toba ya kweli!!!soon watarudhisha majeshi nyuma kujipanga upya....nivigumu baba kukiri nimekosea Ila wenye,je unaweza kula matapishi yako?nimechanganya changanya mwenye kuelewa aelewee
 
Nimeona leo kwenye mitindao muheshimiwa Sana ,mtukigu Rais anatuamasiha waumini wa dini za kikristo,kiislamu na kisabato tusali na kufunga na kwamba tumtegemee MUNGU tu

Je ,ana hofu na Nini?

Tuko uchumi wa Kati kwani shida iko wapi?

Mbona kila siku tunaenda kwenye nyumba zaidi iweje leo kwenye kuaga mwili wa kijazi asisitize Sana hivyo ana hofu gani?

Tuendelee kupiga nyonga[emoji1]
View attachment 1706217
Nyonga tena🤣🤣
 
Tatizo sio Mungu hayupo ila tunaomba atangaze hadharani kua C19 ipo ili tahadhari zianze kuchukuliwa.

😷 😷😷😷😷😷😷😷
Umezuiwa na nani kuchukua tahadhari?Akitangaza tuu hofu itatamalaki na mgonjwa hata anaumwa na ugonjwa mwigine watu watamnyanyapaa.Mwenye akili keshaelewa Corona ipo coz awamu ya 1 tuliishinda sasa ipo CORONA phrase ya pili.
 
Mwambie jiwe ni kweli Mungu yupo na ndiye aliyemuokoa LISU na marisasi 32 ya shetani ambaye leo amegeuka Muomba MUNGU! Haa Tena mwambie jiwe MUNGU wa kweli hajaribiwi na mwaka huu hauishi lazima ampende uchwara zaidi 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😁
 
Inategemea ana maana ya mungu au Mungu! Yule mungu wanayemtumikia wao na akina makonda na Diwani msuya anayewaruhusu kuua hovyo. Yule mungu wanayemtumikia anayewaruhusu kutesa na kuteka binadamu wenzao, yule aliyewaruhusu kudhulumu haki katika uchaguzi uliopita huyo siye tunayemwamini au kumtumikia. Magu mungu wako anayeruhusu ufedhuli siyo Mungu wetu wa Haki samahani endelea naye.
 
Umezuiwa na nani kuchukua tahadhari?Akitangaza tuu hofu itatamalaki na mgonjwa hata anaumwa na ugonjwa mwigine watu watamnyanyapaa.Mwenye akili keshaelewa Corona ipo coz awamu ya 1 tuliishinda sasa ipo CORONA phrase ya pili.
Wewe unaweza kua umechukua tahadhari sawa vipi kuhusu wenzetu wa kijijini mbao hawana elimu ya kutosha juu ya huu ugonjwa na huduma duni za afya?
 
Mhe. Rais naona ameumaliza mzizi wa fitina leo katika mazishi ya Balozi Kijazi na kusema kuwa magonjwa yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, na sisi si pekee ndiyo tunaotaabika na matatizo haya ya magonjwa ya milipuko hata nchi zingine wamekufa wengi sana. Na tatizo linapokuwa kubwa kuzidi uwezo wa binadamu tulisogeze kwa Mungu.

Rais anasema mwaka jana tulimuona Mungu akitusaidia lakini sasa naona wengine hawana imani tena wanatengeneza taharuki na kutishana mimi sifanyi lokudauni tuchape kazi Mungu yupo. Kwanini au amwamini kuwa Mungu anaweza kuishinda Korona?

Mimi mtoto wa mchungaji nahoji hivi hawa baadhi ya viongozi wa dini ambao nao pia wanaogopa Corona kiasi cha kwamba wanatushauri tuwasikilize watu wa afya na wamitandaoni hivyi hawa watumishi wa Mungu si wangeacha hiyo kazi na kuja huku mchangani ijulikane moja.

Nawauliza na ninyi wana janvi Mungu yupo au, maana babuzetu waliomba mvua zilinyesha, waliomba nzige waondoke asubui waliwakuta chali kificha mende, magonjwa ya mlipuko hayakuwagusa, hivi na yule Mungu wa babu zetu yupo wapi siku hizi na huyu wa kanisani na msikitini yupo wapi.
Hizi ni kauli za ovyo za kijinga,Mungu hadhiakiwi,uwezi kupambana na magonjwa kwa kupiga magoti na kuomba wakati Mungu huyo huyo ametoa watu ambao ni madakitari,wamegoma vzr,kwa uwezo waliopewa na Mungu,Ili waisadie jamii,sasa utawala huu,badala ya kusikiliza wataalamu,utawala hautaki wataalamu wawaambie wananchi jinsi ya kujikinga,
Mwaka jana Mungu hakutusaidia,Kama alitusaidia jana,mbona leo hatusaidii na watu wanakufa?

Mungu hawezi kushusha miujiza korona,ipotee,ameishatupa wataalamu ,tuwape nafasi wafanye kazi yao,sio hizi porojo za kisiasa,
 
Huyu jiwe aaache unafiki Kama Mungu huwa anasaidia watu kwa kuomba tu,mbona tunajenga mahospitari,tunasomesha madakitari,si tuache tu,Ili tukiumwa,tupige dua,tupate uponyaji wa miujiza.
 
Back
Top Bottom