4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 8,406
- 9,619
Mkuu umeuliza swali zuri, but omba mungu huku pia ikitumika mahalifa aliyokupa kujua hema na baya, mfano umepimwa umekutwa, typhoid, dawa zipo , na hutaki kunywa, alafu sema mungu tuone Kama hautazikwa,Mhe. Rais naona ameumaliza mzizi wa fitina leo katika mazishi ya Balozi Kijazi na kusema kuwa magonjwa yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, na sisi si pekee ndiyo tunaotaabika na matatizo haya ya magonjwa ya milipuko hata nchi zingine wamekufa wengi sana. Na tatizo linapokuwa kubwa kuzidi uwezo wa binadamu tulisogeze kwa Mungu.
Rais anasema mwaka jana tulimuona Mungu akitusaidia lakini sasa naona wengine hawana imani tena wanatengeneza taharuki na kutishana mimi sifanyi lokudauni tuchape kazi Mungu yupo. Kwanini au amwamini kuwa Mungu anaweza kuishinda Korona?
Mimi mtoto wa mchungaji nahoji hivi hawa baadhi ya viongozi wa dini ambao nao pia wanaogopa Corona kiasi cha kwamba wanatushauri tuwasikilize watu wa afya na wamitandaoni hivyi hawa watumishi wa Mungu si wangeacha hiyo kazi na kuja huku mchangani ijulikane moja.
Nawauliza na ninyi wana janvi Mungu yupo au, maana babuzetu waliomba mvua zilinyesha, waliomba nzige waondoke asubui waliwakuta chali kificha mende, magonjwa ya mlipuko hayakuwagusa, hivi na yule Mungu wa babu zetu yupo wapi siku hizi na huyu wa kanisani na msikitini yupo wapi.
Hoja hapa serikali pitia wizara ya afya , KWA kushirikiana na Tamisemi, lazima kuja na sheria ya mpito KWA ajili ya kujikinga na CORONA, maji tiririka kila mahali kila kaya , barakoa iwe lazima huna na unatembea mjini piga fain, mikusanyiko isiyo ya lazima piga chini,
Tutaweza vuka, ila kusema kwamba corona ya kwanza wenzetu walikufa Sana , ni sawa ila sio kigezo tusichukue hatua ,mpaka nasi yatukute, mdudu , huyu ana mutate kila wakati, hakuna sababu ya kusubili,
I wish , ningekua katibu mkuu, waziri or naibu , Ningeamuka hasubuhi natangaza mikakati tajwa hapo juu, wakati huo nikiwa na barua ya kujiuzuru , au kutumbuliwa mda huohuo!