Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?


Labda tufanye hivi bro, wewe ulitaka sentensi yake aiwekeje?
 
Tunaamini MUNGU wa mbinguni yupo sana na ndiye mkuu Bwana wa majeshi yote ulimwenguni.

Lakini "mungu" mwenye sifa hizi hapa chini.....

  • Anayeruhusu wafuasi wake wamimine risasi 30 ndani ya mwili wa binadamu mwenzao - NAH!
  • Anayeruhusu watu watekwe na kupotezwa - MM!
  • Anayeruhusu watu baadhi wafe chini ya Corona Herd Immunity - a big NO!
  • Anayeruhusu miungu watu wanaopendwa kutukuzwa na kujitukuza - huyo siyo kabisa!
  • Anayeruhusu watu wabake demokrasia na kulazimisha kutawala kwa udhalimu - NEMMA!
 
Mungu ambariki mweshimiwa rais John pombe magufuli Kuna siku tutamwelewa tu ni mtu mwenye maono ya mbali
 
Mkuu mkuu mkuu tafadhali usimziaki Wala kumkufulu Mungu Kuna siku utamwitaji
 
..angewauliza hili swala masista waliokuwa wamevaa barakoa....yani MTU uache kutumia condom umtie demu mwenye Ngoma uone Kama hutaipata Kwa kuwa kuna Mungu!....hii akili mbovu inatumika kwenye Corona Kwa lengo gani?...mfano mwingine..wote hapo mawaziri wanalala na net kujikinga na malaria...wawaambie basi raia wasitumie net Kwa kuwa Mungu yupo...
 
Kuna siku Mungu atakuwa na umuhimu mkubwa Sana kwako.
Mkuu usimkufulu Mungu Kuna siku utamwitaji
Iko hivi... Huwezi lala mlango wazi kila siku kisa unamwabudu Mungu. Kila kitu kina kanuni.
Hatukatai uweza wa Mungu ila ukisema upuuzie mambo muhimu kwa kichaka cha Mungu ...unafeli. huyo Mungu unayemwabudu utampa kazi kubwa sana na utakuwa unamjaribu
 
β€œMwamini Mungu, lakini mfunge vizuri Ngamia wako”-Mtume Muhammad SAW.

Mungu huwa halipi maombi bali hulipa jitihada!Kupiga maombi wakati hakuna mipango pamoja na vitendo(Actions) madhubuti vya kupambana na Corona ni kumkejeli Mungu.
 
Of course by FAAAR!

Huwezi nifananisha na mtu anae deny corona haipo wakati anazika vichaa wenzie kila siku

Mtu anae amini eti kirusi kinaondolewa kwa kula malimao...these are lunatics kabisa!

I'm way better than these clowns!

Sawa Wyatt Mathewson ila naamini unakosea sana kusema kuzika vichaa wenzie sasa hiyo akili yako kubwa iko wapi? Kama hata lugha ya staha heshima na Adabu huna!

Rais ni kiongozi wetu amesema tuchukue tahadhari zote na tusali hapo shida ipo wapi? Leo hapo msibani umeona kuna watu wamevaa barakoa wengine hawakuvaa uliona kawaambia walovaa wazivue? Sasa hapo si swala tu la utashi wa Mtu tu au na hilo hadi Rais aliseme?

Haya watu atangaze atangaze sasa atangaze vipi ilihali kasema tuchukue tahadhari si ina maana anajua uwepo wa hiyo changamoto! Pia akitangaza vifo ndio vitaisha sasa? Haya basi sawa aseme tujifungie ndio hamtaongea? Mtasema alichelewa angefanya toka mda pia hajafunga bado tunalaumu au yeye ndio anawaua watu wote?

Nilichokuja kujifunza Binadamu hashukuru na hana moyo wa kuridhika hata umfanyie nini ni wachache sana Mungu aliowachagua.

Binafsi naungana na Mheshimiwa Rais kwa 100% hata kama na mimi ikiwa ni zamu yangu kufa au Ndugu kwa changamoto yeyote nitaungana na Mheshimiwa Rais Till the end kwa maono aliyonayo.

At the end everyone will stand to face his/ her Judgement with God and not Magufuli. Endeleeni kulaani na kutukana mnavyoweza lakini mwisho wa siku ni maisha ya Mtu mmoja mmoja na si serikali wala Magufuli.

Kila mtu na Imani yake na akili yake na ufahamu wake pia. Mimi ufahamu wangu unanambia kusimama na Mungu na kuchukua tahadhari na ama hakika sijajuta. Kazi nafanya nasonga mbele na natembea kwa imani.
 
Tatizo la sasa ni imani watu wengi hawana imani hata hao wachungji wakijaribiwa kidogo chali na neno linatimia kwamba kama msipohubiri Bwana anaweza amsha jiwe likqhubiri kwa hyo ona ajabu rais anatangaza uzima na imani kwa Mungu hao wachungaji wanatangaza kujifungia namuombeq kwa Mungu rais wetu imani yake isimame milele
 
Tamkeni wazi kwamba Covid-19 ipo. Sasa hayo maombi tutakuwa tunamwomba MUNGU afanye nini kwa kitu ambacho hakipo? Utamwombaje Mungu akuponye kama huumwi?

Tamkeni wazi kwamba kuna Corona na hapo tuanze kumlilia MUNGU atuponye na UGONJWA HUO. Na Mungu ana njia nyingi za kutuponya, tusimwekee mipaka. Anaweza kutuponya kwa kumpa mwanadamu maarifa ya kugundua chanjo. Tusiwe watu wa kutegemea miujiza kwenya mambo yanayohitaji utaalamu.
 
S
So whats the conclusion
 
Tatizo sio Mungu hayupo ila tunaomba atangaze hadharani kua C19 ipo ili tahadhari zianze kuchukuliwa.

😷 😷😷😷😷😷😷😷
Tatizo lipo hapo. Hadi uambiwe ndio ujue cha kufanya?
 
Kama ni Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo basi alielekeza wana wa Israeli kuchukua tahadhari ya kiafya na alianzisha karantini ya kwanza duniani kwa kuwaelekeza wenye ukoma watengwe kwa siku saba mpaka 14 ili wasiambukize watu wengine. Hao miungu wengine siwafahamu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…