Rais Magufuli anahoji; Je, ninyi hamuamini kuwa yupo Mungu?

Wengi wana chuki binafsi tu ukishawaelewa hawakupi shida kabisa,,,,,wanatafutaga tu sababu za kutoa povu hata akifanya hayo wanayosema lazima watatafuta lingine la kulialia
 
Tatizo sio Mungu hayupo ila tunaomba atangaze hadharani kua C19 ipo ili tahadhari zianze kuchukuliwa.

😷 😷😷😷😷😷😷😷
We usichukue tahadhari jiachie tu kula maisha hadi rais akikwambia
 
Wewe unaweza kuchukua tahadhari zote.
Lakini Kama jirani yako hachukui tahadhari. Hata wewe unakuwa katika hatari ya kupata maambukizi.

Ndio Maana tunalia na viongozi, ili watu wote( asilimia kubwa) wachukue tahadhari.

Kuvaa barakoa
Kunawa mikono
Kuepuka misongamano, nk

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Mungu hajawahi msaadia mtu anayekaa kumlilia yeye bali huwasaidia wale wanaofanya bidiii kutatua shida zao.Tunajukumu la kumaliza Corona kwetu lakini nasi yatupasa kuusaidia ulimwengu kumaliza tatizo.Msimamo wako binfsi haupaswi kuwa ndio msimamo wa taifa.
 
Rais kwa nini anapata kigugumizi kizito hivi kutamka tu kuwa covid 19 ipo ili Watanzania hususan mashariki wake walione hilo na wote kwa ujumla wetu tuwe na mwelekeo mmoja wa kuchukua tahadhari. Anafika mahali anaquestion hata Imani ya viongozi wa dini wanaotuasa kuchukua tahadhari. This is pathetic.
 
Hiiiii.........This is Africa blaza penda usipende ndo imeshaenda hio
 
Tatizo sio Mungu hayupo ila tunaomba atangaze hadharani kua C19 ipo ili tahadhari zianze kuchukuliwa.

😷 😷😷😷😷😷😷😷
Utakufa wewe kwa kusubiri tangazo
 
Mimi ninasema tu. Mungu alitusikia kweli kabla ya uchaguzi mkuu lakini kwa tuliyoyafanya uchaguzi mkuu inawezekana Mungu kaondoa mkono wake ndiyo maana haya yanatupata. Tunatakiwa toba ya kweli kwa Mungu na kuomba msamaha kwa wapinzani. Biblia inasema kama humpendi jirani yako utawezaje kumpenda Mungu usiyemwona?. (Marko 12:21 " Na ya pili ndiyo hii. Mpemde jirani yako kama nafsi yako.") Tulichowatendea ndugu zetu wapinzani hakitatuacha salama kwa kweli. Mungu hawezi kutusikia hata tuombe vipi kama ndani yetu kumejaa chuki.
 
Huyu Mungu wa Magufuli ndiye anayeunga mkono wizi wa kura? Ndiye anayeruhusu anayemkosoa atandikwe risasi au apotezwe kama Saanane? Huyo Mungu wa Magufuli ndiye anayemwagiza awaambie wakurugenzi wasiwatangaze wapinzani washindi hata hama wananchi wamewachagua? Mungu wake Magufuli ni huyo anayesema wananchi wabambikiwe kesi za uhujumu uchumi?

Kama ningepewa na nafasi kuwa nipime kwa jicho la kibinadamu, na kishe nizipange awamu zote za Serikali katika ucha Mungu, hakika bila ya unafiki, hii ya awamu ya tano ni ya Kishetani. 80% inayoyatenda ni yale yaliyo kinyume na upendo wa Mungu.

Leo wakala wa shetani anatufundisha namna ya kumwabudu Mungu wa Kweli?
 
Tatizo sio Mungu hayupo ila tunaomba atangaze hadharani kua C19 ipo ili tahadhari zianze kuchukuliwa.

😷 😷😷😷😷😷😷😷
Kuchukua tahadhari kwa ajili ya afya yako, mpaka Rais akutangazie! Mna visa vingi ninyi watu!!
 
Hivi wewe ni lini umewahi mwamini Mungu wewe, Mungu ndio kila kitu.
 
Kumbe Mungu wa siku hiz yuko hivyo!!?? Yan uue, uumize, utese alafu iwe ni mkono wa Mungu wew kupata hiyo!?? Endelea kumpenda Magu kwa maana hujakutwa na mkono wa kishetani kutoka kwake
Hivi unadhani Ayubu alikuwa hamuamini Mungu!?
 
t
Kumbe Mungu wa siku hiz yuko hivyo!!?? Yan uue, uumize, utese alafu iwe ni mkono wa Mungu wew kupata hiyo!?? Endelea kumpenda Magu kwa maana hujakutwa na mkono wa kishetani kutoka kwake
tatizo sio wewe unayeandika bali ni pepo lililopo ndani yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…