Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Nakuunga mkono kwa 10%
 
28yrs kweli chama hakina mtu mwingine wa kuweza kushika nafasi ya uenyekiti! Na wasomi wote hao ndani ya chama. It's a shame. Kwahiyo nijue kuanzia sasa iwapo Mbowe atafariki au kustaafu siasa cdm itakuwa haina mwenyekiti tena. Utani mwingine bana.
Hahaaa kuna jambo nikwambie. tatizo unalinganisha CCM na CDM ndio maana unaona 28 yrs ni mingi sana.

CCM ni chama kikongwe zaidi, kina rasilimali na taasisi wanazoweza kuzitumia kuidhoofisha CDM, tumeona bunge na mahakama zinavyoendeahwa. Sasa kwny mazingira haya CDM lazima wawe makini sn kwa yule watakayempa chama, mbinu za CCM ni nyingi, wanaweza honga mgombea huko nje mumpe chama halafu CDM ndio ibaki historia, na siku CCM wakiipata CDM kwny amgle yao, wataipoteza mazima, siku zote wanataka vyama vyote vya upinzani viwe dhaifu.

Kama siasa za hii nchi zingekuwa za kistaarabu nakuhakikishia Mbowe leo tungekuwa tumeshamsahau, tatizo wengi wa wanasiasa wa nchi hii ni njaa, wana bei, tunaona kila siku uthibitisho wa hili, ni hili sio tatizo la CDM kama chama, ni tatizo la watu binafsi, wapo sehemu kwa maslahi yao, ni wabinafsi japo wana tudanganya vinginevyo.

Sasa niambie, leo CDM waamue kumtoa Mbowe halafu chukulia mfano wampe mtu kama Mwambe kwasababu ndie aliekuwa mgombea pinzani wa Mbowe, mtu aliyeshindwa kuvumilia kukosa ushindi wa uenyekiti, angeweza kuvumilia hila na mbinu chafu za CCM?!

Wengi wa wanaompinga Mbowe ni CCM ukiachilia wachache wenye msimamo kama wako ndani ya chama, sasa huoni kumuondoa Mbowe madarakani hasa kwa wakati huu na awamu hii ni kukaribisha majanga kwa chama? unadhani Magu anataka kiongozi wa upinzani mwenye msimamo km Mbowe? na km asingekuwa Mbowe m/kiti wa CDM leo hii nina hakika hizi vurugu za watu kukimbilia NCCR na CCM mpk CUF leo hii zisingekuwepo, coz km wameshaona wanawamudu kwanini wahangaike na nyie?

Mbowe kawasababisha CCM watenge pesa maalum kwa ajili ya kununua watu toka CDM, wakifika kule wanapewa mpk uwaziri!

Sometimes I blv if you cant defeat them kwa hila zao, basi atlist wakere, ndicho kinachotokea sasa, wacha wapoteze pesa kununua watu ambao naamini watasababisha mgogoro huko kwao mbele ya safari.

Halafu kuna msimamo wako mwingine huwa siuelewi, "no tume huru no uchaguzi" is it practicable on your part? and if the answer is yes, unadhani likitokea litamnufaisha nani? ukumbuke CDM wasiposhiriki watashiriki kina NCCR na wenzie, sijui why unaamini kwenye kumsusia fisi bucha!.
 
28yrs kweli chama hakina mtu mwingine wa kuweza kushika nafasi ya uenyekiti! Na wasomi wote hao ndani ya chama. It's a shame. Kwahiyo nijue kuanzia sasa iwapo Mbowe atafariki au kustaafu siasa cdm itakuwa haina mwenyekiti tena. Utani mwingine bana.
Ww kwa maoni yako nani kati ya mwambe , sumaye nani anasifa za kumfanya awe M'kiti wa chadema...nakuomba sana hili swali jibu
 
Hivi mbowe ananini cha zaidi ambacho ameshindwa kukitekeleza kwa miaka yote aliyokuwa madarakani
Nikuulize, mwl akifundisha darasa la mtihani na wanafunzi wake wakafaulu vyema, mwl huyo hutakiwa kuiacha kazi yake?
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Shujaa tena wakati katepeta kama socks ya ngasa
Si ni Bora Bora yeye kwa mtepeto wa soksi kuliko wenu mlenda? Pamoja na advantages nyingi alizo nazo bado anaweweseka kwa kushindwa kuiua cdm Kama alivyoahidi! Yaani mtakufa ninyi na kuiacha cdm na Mbowe wakidunda!
 
Huyo unayemjibu kwa kejeli ni mfia chadema

Mjifunze ukiambiwa ukweli meza, na sio umfananishe na JPM. Aazungumzia chama unazungumzia serikali, umeishia darasa la ngapi? CCM ishabadili wenyeviti mara ngapi?


Tindo anaipenda CDM kuliko wewe
Nimeishia darasa uliloanzia! Una lingine?
Unanifundisha jinsi ya kuwakubali wanafiki? Yu wapi Dr Slaa. Walikwenda wapi kina Dr Kaborou? Hawakuwa wapenzi na wafia cdm? Nini kiliwatokea na kuyabadili mapenzi yao? Wasaliti wapo na kila chama kwa ufafanuzi muulize Zitto!
 
Nikuulize, mwl akifundisha darasa la mtihani na wanafunzi wake wakafaulu vyema, mwl huyo hutakiwa kuiacha kazi yake?
Mwalimu anayemfundisha mwanafunzi shule ya msingi hawezi kumfunsisha mwanafunzi huyo huyo akifika chuo, siyo kila mwafunzi uwezo wake wa kuelewa ni mdogo kuliko mwalimu wake
 
Nikuulize, mwl akifundisha darasa la mtihani na wanafunzi wake wakafaulu vyema, mwl huyo hutakiwa kuiacha kazi yake?
Mwalimu anaweza pia kuwa mwanafunzi wa mwanafunzi wake akihitaji kuongeza elimu
 
Kama kumpata tu mrithi wake inakuwa shida atawezaje kuunda serikali
 
Mwalimu anayemfundisha mwanafunzi shule ya msingi hawezi kumfunsisha mwanafunzi huyo huyo akifika chuo, siyo kila mwafunzi uwezo wake wa kuelewa ni mdogo kuliko mwalimu wake
Unaona ulivyo kiazi? Soma Tena nilichokiandika ulinganishe na hoja yako ya mwanzo!
 
Daah, Watanzania ni wapi tunakwama??

Mkuu, alichoandika mkuu Tindo ni ukweli 1000%

Ndugu yangu, hata wewe mwenyewe ukikaa Sana kwe nafasi Fulani ya kiuongozi huwepo kitu kinaitwa mazoea ya kazi na matokeo yake akiri hulala, heshima ya Mbowe ipo kubwa Sana Tu,Ila Kwa sasa hawezi kabisa kuleta kipya ndani ya chama
 
Baba kumsomesha au kumfungulia biashara mwanae haimfanyi mwanae ampe Pesa yote babake kwa kisingizio cha kumpatia mahitaji yamsingi, haiwezi kuingia akilini hata siku moja kuwa mbowe anawazidi uwezo wa kuongoza wanachadema wote
 
Mwl. Nyerere aliiongoza TANU na Ccm kwa miaka mingapi? Ukilipata jibu njoo Tena!
Unajua maana ya uzoevu? Unajua kuwa uzoevu huujenga umahiri? Yawezekana huelewi lolote juu ya uzoevu usiojengwa kwa mwaka mmoja Bali kwa miaka mingi utakayoishi! Au wewe huujengi umahiri wowote kupitia uzoevu?
Hauawahusu ya mwenyekiti wa cdm na najua mmetumwa kuziimba nyimbo za kebehi hapa! Kwa Sasa Mbowe ndiye mwenyekiti wa cdm na akiutaka Tena atapewa, tuombe uhai!
 
Nilisoma kwa haraka haraka na kudhani kuwa "Mh. Rais Magufuri anatengeneza upinzani pure utasumbua sana 2020" kumbe ni kinyume chake.
Binafsi naona upinzani imara hautengenezwi na Rais,unatengenezwa na wapinzani wenyewe kujipanga kukabiliana na Chama tawala chini ya Magufuri.
Upinzani imara Tanzania utapatikana 2035 kutokana na upinzania wa Leo na matunda ya wenye uadilifu kutoka Chama tawala.
 
Kiukweli mbowe alitakiwa aache uenyekiti kwa kosa tu alilofanya kwa uchaguzi wa mwaka 2015
 
Baba kumsomesha au kumfungulia biashara mwanae haimfanyi mwanae ampe Pesa yote babake kwa kisingizio cha kumpatia mahitaji yamsingi, haiwezi kuingia akilini hata siku moja kuwa mbowe anawazidi uwezo wa kuongoza wanachadema wote
Wewe kiini Cha mbegu cotyledon, usinilishe maneno! Nimesema nyumba na sio biashara! Jifunze kuja na mifano yenye uhalisia na sio huu urojo wako!
 
Mkuu, acha kupoteza muda. Upinzani 2020 hauna nafasi kabisa upande wa urais, hata ubungeni ni changamoto!
 
Ndugu mleta mada, hicho Chama cha CCM unachokitaja, ni Chama moja matata mno, ni Chama kilicho na majasusi waliobobea kisiasa za Kisayansi, ni Chama kinachofanya tathimini na kuona makosa na Kisha hujilidhisha endapo makosa hayo yatakigharimu Chama kwa kiasi gani ama kitapata faida Kwa kiasi gani na Kwa namna gani, ndipo hufanya maamuzi Kutokea hapo

Kina watu ambao hata wewe huwagshamu lakini wakipewa nafasi ndipo unawatambua nguvu zao

Kile Chama mpaka kinafanya maamzi Fulani, wenzio walishaona Hadi mwisho wa maamuzi hayo, wewe endelea kujidanganya mkuu

Kuna watu hupelekwa kwenda Kusoma kinyume na unachowaza wewe au mpinzani, wanauwezo wa Kufanya Impossible kuwa it is possible
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…