Unadai kila siku huwa unasema humu ndani na kila siku huwa unakosea, bora uache kusema sasa.
Mbowe kuwa Mwenyekiti Chadema hakuna anayezuiwa kumpelekea mawazo ya kujenga chama, kuwa kiongozi hakumfanyi awe malaika wakujua kila kitu, hoja yako kwamba kiongozi akikaa madarakani miaka 15 uwezo wa kuongoza unapungua ni nyepesi sana, halafu inakuaje mtu km bado anakubalika aache tu kuongoza eti kwasababa miaka 15 imefika, huo uwezo unashuka vipi, anakuwa chizi au?!
Halafu unaonesha ulivyo muoga kwa kusema Mbowe na Chadema wamejiweka kwenye mazingira ya kushambuliwa kisiasa na wapinzani wao kwa sababu ya ule ujio wa Lowassa, km unaogopa kushambuliwa na wapinzani mjomba acha kufuatilia siasa, nenda kasapoti uchungaji; hao watu hawawezi kuacha kukushambulia na lazima uwe tayari kujibu mashambulizi yao perfectly, ambapo naamini mpk sasa CDM wako vizuri ndio maana Mbowe binafsi anashambuliwa na viongozi wa bunge na serikali, but still ametulia.
Yaani Mbowe aachie uenyekiti wakati ambapo maadui wake wa nje wote walikuwa wanataka aondoke?!
this is bullshit of the highest degree.
Kama hizo tuhuma unazoogopa wana ushahidi nazo waende mahakamani, you sound very weak, unaogopa maneno tu!.
In life you dont have to do anything to please anyone, just do what you believe is right for you.
Naheshimu mawazo yako, sina tatizo lolote na unaloamini na unayemuamini. Kwanza kabisa sina hofu yoyote na mashambulizi, bali mashambulizi ya makosa ya kibinadamu hayatoi picha nzuri. Huenda ww unaamini katika mtu, wakati mimi naamini katika taasisi, hilo sio kosa lako ni kosa langu.
Sasa twende pamoja na hapa sikulazimishi kuamini/kukubali bali ndio uhalisia. Viongozi wote wa kuchaguliwa hufanya vyema ndani ya miaka 10, au 15. Lakini ni nadra kiongozi kuzidi miaka 15 akiwa madarakani, tena nafasi moja ya uongozi akafanya vizuri. Wengi hujikuta ubora wao umepungua, au huongoza kwa ubora hafifu na mizengwe kibao. Mfano wa viongozi waliokaa madarakani zaidi ya miaka 15, matatizo na mizengwe kuanza,
- Nyerere
- Mugabe
- Ghaddafi
- Moi
- Paulo Biya
- Museveni
- Hosin Mubaraka
- Fidel Castro nk
Mifano hiyo michache hapo juu inabeba hoja zangu. Sasa tuje kwa Mbowe. Ubora wa Mbowe ukiangalia vizuri ulikuwa ni ndani ya miaka kumi ambapo cdm ilikuwa kwa kasi, na miaka mitano kabla ya uchaguzi wa 2015 ilikuwa bora kabisa,lakini ilipaswa kuwa kilele bila kujali kama cdm ingekamata dola au la. Kosa la kwanza dhahiri kabisa, unapokuwa na chama imara kisha ukachukua mgombea wa kuokoteza, miezi michache kabla ya uchaguzi tena kwa nafasi ya urais, utakuwa mwendawazimu wa hali ya juu kushabikia kiongozi wa aina hiyo. Halafu unaleta mgombea dhaifu, wala asiyejua itikadi ya chama, wala kuziishi falsafa za chama. Kisha mgombea huyo wa kuokoteza, anarudi huko anakoamini!
Sasa hivi chaguzi zote zinahujumiwa waziwazi wala hatuoni hatua zozote za maana, hata kwenda mahakamani tu. Viongozi wengi hasa waliookotezwa dakika za majeruhi uchaguzi wa 2015 ndio wamerejea ccm, kiongozi huoni kuwa ni sahihi kujiuzulu? Yaani lifanyike kosa gani ndio kiongozi awajibike? Isitoshe kama ni kukaa madarakani kashakaa miaka 15, anaongeza mingine ya nini wakati taasisi ina mivutano isiyo na afya kwa chama? Wengi wetu hatuamini kwenye viongozi wanaokaa madarakani muda mrefu, kwa hili la Mbowe kwanini tukwame? Hizo tuhuma dhidi ya Mbowe, huenda zote sio za kweli bali ni siasa chafu, ila utakuwa punguani kuamini kuwa zote ni za uongo. Sina shaka na ninachokisema, kama unaamini katika watu, mimi siamini kabisa katika mtu imara, bali naamini katika taasisi imara.