Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Kama kuna ushindani hakuna cha kushangaza akiwa mbunge, lakini kama uchaguzi ni huu Magufuli anaamua nani atangazwe mshindi, basi Mbowe hatatangazwa mshindi hata ashinde.
Tanzania ilipo unafikiri CCM inastahili Kuongoza nchi?
 
Watasubiri sana Chadema haiwezi kufa!!
 
Hakuna upinzani PURE ndugu, huu mchezo mwepesi kwa mtu mwenye dola hasa palipo na umasikini. Kila mtu ana bei yake, hao unaowaita pure hawajapewa nafasi ya ku bargain tu.
 
Wana cdm bado tuna imani na mh Mbowe, hakuna kiongozi wa upinzani ambaye ameamua kiukweli kuwa kiongozi wa upinzani.

Mbowe kafanyiwa kila aina ya vitimbi vya kummaliza kiakili na pia kiuchumi.
Katengenezewa kila aina ya kesi kisa msimamo wake thabiti juu ya cdm lkn bado yupo imara.

Bado tupo naye sana
Ambavyo mbowe hafai ndiyo hivyo ivyo na CCM haifai mkuu kuongoza nchi
 

Naheshimu mawazo yako, sina tatizo lolote na unaloamini na unayemuamini. Kwanza kabisa sina hofu yoyote na mashambulizi, bali mashambulizi ya makosa ya kibinadamu hayatoi picha nzuri. Huenda ww unaamini katika mtu, wakati mimi naamini katika taasisi, hilo sio kosa lako ni kosa langu.

Sasa twende pamoja na hapa sikulazimishi kuamini/kukubali bali ndio uhalisia. Viongozi wote wa kuchaguliwa hufanya vyema ndani ya miaka 10, au 15. Lakini ni nadra kiongozi kuzidi miaka 15 akiwa madarakani, tena nafasi moja ya uongozi akafanya vizuri. Wengi hujikuta ubora wao umepungua, au huongoza kwa ubora hafifu na mizengwe kibao. Mfano wa viongozi waliokaa madarakani zaidi ya miaka 15, matatizo na mizengwe kuanza,
  1. Nyerere
  2. Mugabe
  3. Ghaddafi
  4. Moi
  5. Paulo Biya
  6. Museveni
  7. Hosin Mubaraka
  8. Fidel Castro nk
Mifano hiyo michache hapo juu inabeba hoja zangu. Sasa tuje kwa Mbowe. Ubora wa Mbowe ukiangalia vizuri ulikuwa ni ndani ya miaka kumi ambapo cdm ilikuwa kwa kasi, na miaka mitano kabla ya uchaguzi wa 2015 ilikuwa bora kabisa,lakini ilipaswa kuwa kilele bila kujali kama cdm ingekamata dola au la. Kosa la kwanza dhahiri kabisa, unapokuwa na chama imara kisha ukachukua mgombea wa kuokoteza, miezi michache kabla ya uchaguzi tena kwa nafasi ya urais, utakuwa mwendawazimu wa hali ya juu kushabikia kiongozi wa aina hiyo. Halafu unaleta mgombea dhaifu, wala asiyejua itikadi ya chama, wala kuziishi falsafa za chama. Kisha mgombea huyo wa kuokoteza, anarudi huko anakoamini!

Sasa hivi chaguzi zote zinahujumiwa waziwazi wala hatuoni hatua zozote za maana, hata kwenda mahakamani tu. Viongozi wengi hasa waliookotezwa dakika za majeruhi uchaguzi wa 2015 ndio wamerejea ccm, kiongozi huoni kuwa ni sahihi kujiuzulu? Yaani lifanyike kosa gani ndio kiongozi awajibike? Isitoshe kama ni kukaa madarakani kashakaa miaka 15, anaongeza mingine ya nini wakati taasisi ina mivutano isiyo na afya kwa chama? Wengi wetu hatuamini kwenye viongozi wanaokaa madarakani muda mrefu, kwa hili la Mbowe kwanini tukwame? Hizo tuhuma dhidi ya Mbowe, huenda zote sio za kweli bali ni siasa chafu, ila utakuwa punguani kuamini kuwa zote ni za uongo. Sina shaka na ninachokisema, kama unaamini katika watu, mimi siamini kabisa katika mtu imara, bali naamini katika taasisi imara.
 
Ccm chini ya JPM hakuna makundi. Hivyo mtu akipita kwenye kura za maoni tambua anakubalika.
Mliobaki Chadema ni vibaraka mnaoishi kwa kulipwa na Mbowe huku yeye akikwapua bil 8.
Dr molel Naibu waziri [emoji23]
 

Sina chuki yoyote dhidi ya Mbowe kama Mbowe, nina tatizo na nafasi ya mwenyekiti kukaliwa na mtu mmoja kwa muda mrefu, huku kukiwa na sababu za wazi nafasi hiyo kukaliwa na mtu mwingine. Na wala sio kukaliwa na mtu mwingine tu, bali kukaliwa na mtu sahihi . Katika watu wasiomini hizo taka ngumi toka ccm kupewa nafasi ya uongozi ndani ya cdm, basi mimi ni mmojawapo. Hivyo usinitajie viongozi waliotoka ccm, kama sehemu ya Utetezi wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti tena.

Halafu unaposema wanachama mlimchagua, sina tatizo la yeye kuchaguliwa na watu wengi, ila ni ngumu kuamini chaguzi zetu waafrika hasa zinapokuwa chini ya viongozi waliokaa muda mrefu madarakani. Na kwa kukiongezea hata akina Mugabe, Moi nk walikuwa na watu waliowataka waendelee kuwa madarakani kwa kisingizio cha kuwa hakuna anayeweza kama wao. Na wengi wa huu Utetezi hujikuta ni wale wenye maslahi binafsi na kiongozi husika.
 
Umejenga hoja vzr mwishowe ukaalibu. Unaposema fisadi Luwassa, hiyo kisheria ni statement of conviction! Je ni mahakama ipi ndan ya jamuhuri yetu iliyomtia hatiani Lowassa ufisadi. Thread zenu zifanye za kuelimisha watu sio hivyp. Nafikili mwongozo mpya JF aliyotoa Melo unakuhusu. Tumia hekima ya umri wako kujenga hoja non partisan ulifae jukwaa.
 

Hicho kifungu cha kuendelea kukaa madarakani zaidi ya miaka 10, nacho kina utata. Sio mara moja au 2, kifungu hicho kimekuwa kikizua minong'ono na malalamiko ya wazi. Tukitaka tutembee kifua mbele tuwe wakweli tu. Penye shida ni lazima pafanyiwe kazi kwa afya ya taasisi. Sisi wengine cdm iko mioyoni mwetu na hilo liko wazi. Tukikubali udhaifu wa kibinadamu ukawa ndio udhaifu wa taasisi, tunajua tutaishia kusikofaa. Mimi kama mimi naamini ukomo wa miaka 10 no matter what. Ila kama katiba inataka zaidi ya hivyo, naheshimu katiba hiyo kwa shingo upande. Lakini kukaa tena madarakani zaidi ya miaka 15, huku ukiokoteza wagombea wa urais, na kuwa na misuguano isiyo na tija, hapo sioni afya ya taasisi.
 
Hilo swali unalomuuliza Tindo sio gumu kiviile!; Mbowe angekuwa naye ni muumini wa demokrasia anayeruhusu kupingwa ungeona wengi. Tatizo uko mtu ukionyesha nia tu, ujue unanyang’anywa sahani na mlo ndio basi. Na kwenye siasa watu wapo ili pia wale sio kutufurahisha sisi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…