Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Big up mkuu, umenena ukweli mtupu, tunahitaji Sana vyama vya upinzani lakini ili upinzani uweze kukemea maovu ya chama tawala lazima wao Kwanza wawe mfano, mbowe aandae vijana kuwa viongozi na sio yeye tuu inatupa shida hii kitu
 
Enh ni sawa tu mbona Meko anafuja fedha za umma
Magufuli hajawai na wala haitotokea.
Ona midege yote ya Tanzania ianayopishana angani.
Ona mi interchange anavyojengwa kwa fujo.
Sgr na bwawa la kufua umeme zote hizo ni juhudi za Rais Magufuli.
 
Kubishana kusiko na maana maana yake unataka kukimbia hoja yako, km unaiamini ilinde mpk mwisho, halafu ulishakiri unaziogopa.

Umesikiliza propaganda za CCM zimekuingia kichwani ukaziamini.

Kupokezana madaraka kunatokana na uimara wa taasisi, najua unataka CDM wafanye km CCM wanavyofanya, lazima kukumbuka ukongwe wa hivyo vyama viwili, kinyume na hapo kutaka tu CDM wawaige CCM tena wakiwa wanapigiwa kelele na CCM wenyewe unajidanganya.

Zitto alitaka uenyekiti wa CDM akiwa anafanya vikao vya siri na JK, ulitaka apewe uenyekiti?

Huyo Mwambe wa juzi kuukosa huo uenyekiti akakimbilia CCM, ulitaka mtu wa aina hii apewe uenyekiti wa CDM inayowindwa na CCM kila siku?

Niambie, wewe ulitaka nani awe mwenyekiti wa CDM?
 
Usilazimishe tulia, sio chama hakiwezi kupata mwenyekiti mwingine, kitampata wakati wowote muda utakaporuhusu, sio kulazimisha mwenyekiti mpya ili kuwaliwaza wewe na CCM.
 
Naona umeshiba mkuu
 

Huyo unayemjibu kwa kejeli ni mfia chadema

Mjifunze ukiambiwa ukweli meza, na sio umfananishe na JPM. Aazungumzia chama unazungumzia serikali, umeishia darasa la ngapi? CCM ishabadili wenyeviti mara ngapi?


Tindo anaipenda CDM kuliko wewe
 

Nilikuambia kubishana kusikokuwa na maana kwani nimegundua unaoongozwa na mambo ya mahaba niue, lakini unaukwepa ukweli. Huenda unadhani mimi ni mwepesi kiasi naweza kutekwa na hizi propaganda mfu za ccm humu mitandaoni, au nje ya mitandao. Nimejiunga hapa jf 2011, na kama ni kutekwa na propaganda za ccm basi ningetekwa muda mrefu. Nilianza kuikubali cdm rasmi 2006. Muda wote huo hakukuwa na propaganda dhidi ya cdm, na huyo Mbowe ila zimeanza wiki iliyopita ndio maana sasa hivi zimenichanganya? Post zangu zote kuhusu cdm zimo humu ndani toka nilipojiunga, fuatilia uone kama nimewahi kuyumba kuhusu hiyo cdm.

Humu ndani kuna post kibao za kuiponda cdm na Mbowe respectively. Na wanaoanzisha hizo mada unawajua na mimi nawajua, na lengo la mada zao. Umeniona nikishabakia wasemacho kuhusu Mbowe zaidi ya kuitetea cdm kama taasisi. Kama wewe ni mtu makini fuatilia muanzisha mada kama ni mshabiki wa ccm kwa sasa, au mpiga propaganda wa ccm. Nimechangia kwenye uzi wake kuhusu huu udhaifu wa cdm, ili nisitoe maoni yangu kwenye uzi wa propaganda za ccm. Najua kwa uhakika nilichoongea, na nilipochangia.

Ukiwa na nafasi vuta post zangu kuhusu Zito huko nyuma kama niliwahi kuunga mkono yeye apewe nafasi ya mwenyekiti, au hizi taka ngumu toka ccm zilizokuja na mafuriko ya Lowassa. Unaposema cdm wangempa nani nafasi ya mwenyekiti, hivi kweli huoni aibu chama kina miaka 28 hakiwezi kutoa mwenyekiti zaidi ya aliyepo? Mkuu haya maoni yangu ni kama wali ulio na mawe, huna jinsi zaidi ya kuula kwani una njaa.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Shujaa tena wakati katepeta kama socks ya ngasa
 
Ukweli upi ninaoukwepa, una tatizo la kuona maneno yako ndio kama sheria, usijidanganye, kumhusu Mbowe nitaendelea kumtetea tu sijali unayoyaita mahaba niue au whatever, nimekwambia sema nani unataka awe mwenyekiti wa CDM husemi, unaleta habari ya aibu... mimi sio mwanamke, mtaje; but still unapiga kelele tu Mbowe aondoke, Mbowe aondoke... sasa km humjui wa kuchukua nafasi yake why unapiga tu kelele?!

Kuthibitisha zaidi ulivyo dikteta halafu unamsema Mbowe unaniambia maoni yako ni km wali wenye mawe, sina budi kuula kwani nina njaa, if you think so, then what about my idea, nayo ni pilau lazima ulile hata km lina mawe, coz una njaa pia, narudia tena, maneno yako sheria.

Nilishakwambia kule juu Mbowe hajajiweka, amewekwa, sasa kwanza uelewe pakuelekeza shutuma zako, nakuona unakurupuka tu kumshambulia asie stahili na wali wako wenye mawe.

Historia yako na jf has got nothing to do with me, ujifunze kutofautiana kimtazamo.
 

Ww ndio umesema mimi nataka kukimbia mada, I was here since 2011, sina chochote wala yoyote wa kumkimbia humu ndani. Sina popote ninapotaka neno langu kuwa sheria, ila nilikwambia sioni sababu yoyote ya mimi na ww kuingia kwenye mabishano yasiyo na tija, na hata hiki unachotaka kukileta ndio hicho nilichokuwa sikitaki. Sio kwamba siwezi kubishana, lakini kwangu mabishano hayana tija maana hayaleti suluhisho la tatizo husika.

Mimi sina mtu maalum huko ndani ya cdm kiasi kwamba utake nikutajie mtu specific. Sina maslahi yoyote na mtu binafsi huko ndani ya cdm. Isipokuwa najua cdm ina watu wa kutosha, hivyo sina shaka kuwa ndani ya watu hao, lazima awepo mwingine anayeweza kuwa mwenyekiti. Sio lazima awe kama Mbowe parsee, lakini sina shaka na uwepo wa mtu mwenye uwezo wa kuwa mwenyekiti. Tuchukulie leo Mbowe kafa, je hicho chama hakutakuwa na mwenyekiti? Ni vyema ukaona hoja yangu ilipo, na wala sikuzuii ww kuonyesha mahaba yako kwa Mbowe, isitoshe yeye ndio mwenyekiti hata sasa.
 
Sasa hao watu wakutosha unaoamini wapo ndio bado hawajajitokeza, siku wakijitoleza watakabidhiwa majukumu, sio kuendelea kumlaumu Mbowe, anachaguliwa na wengi na wengi siku zote lazima wapewe.

Personally ni supporter tu wa CDM, sio mdogo wake Mbowe, wala mjomba wake, so no mahaba niue on my part or anything.

The rest is history, I rest my case.
 

28yrs kweli chama hakina mtu mwingine wa kuweza kushika nafasi ya uenyekiti! Na wasomi wote hao ndani ya chama. It's a shame. Kwahiyo nijue kuanzia sasa iwapo Mbowe atafariki au kustaafu siasa cdm itakuwa haina mwenyekiti tena. Utani mwingine bana.
 
Hivi mbowe ananini cha zaidi ambacho ameshindwa kukitekeleza kwa miaka yote aliyokuwa madarakani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…