Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Mkuu Nikuulize swali, je umewahi kuuona huo mkataba? Mimi wote nawaona wehu tu si kikwete si ******** si samia mi nachotaka mkataba uwekwe wazi wananchi tuuone, tuusome na tuuelewe ili tujue kama unafaa ama la.
 
Mkuu Nikuulize swali, je umewahi kuuona huo mkataba? Mimi wote nawaona wehu tu si kikwete si ******** si samia mi nachotaka mkataba uwekwe wazi wananchi tuuone, tuusome na tuuelewe ili tujue kama unafaa ama la.
Huhitaji kuona mkataba ili ujue madhara ya kuipa nchi nyingine bandari (lango kuu) la nchi yako walimiliki. Huhitaji kuona mkataba ili ujue kuwa hiyo bandari siyo muhimu kwa sababu tayari tuna bandari ambazo tunaweza kuziendeleza kwa gharama ndogo, iliyo kwenye uwezo wetu, na zikakidhi mahitaji yetu.
 
Basi kwa maneno yako hayo niishie hapa maana nimeshakujua wewe ni mtu wa namna gani, uwe na jioni njema.
 
Huelewek unasimamia wapi
Unasema kweli, au unategemea niseme kwamba naunga mkono kila jambo alilokuwa akilisema Magufuli?
Kamwe siwezi kusema hivyo, kwa sababu mapungufu yake yalikuwa ni makubwa sana, kiasi cha kuharibu hata yale niliyoona ni mazuri akiyasimamia.
Na kama wewe upo upande wa 'Maza Mizinguo' na genge lake la wapigaji, akina Januari, Zitto na wengine, wanaofanya kila jitihada sasa za kunadisha kila mradi tunaotegemea utuletee manufaa kwa shibe zao, tambua kwamba hutanisikia nikifanya hivyo.

Unataka kujua ninaposimamia? Ninasimamia katika maslahi ya Tanzania na wananchi wake, basi.
 
Kwa sehemu kubwa sana tunakubaliana kati yako na mimi.
Mimi naamini kabisa kwamba bandari ya Bagamoyo ni muhimu sana kwa Tanzania, tatizo pekee lililopo ni, je, itajengwa vipi, na nani na kwa masharti gani.

Kenya wameanza ujenzi wa bandari yao ya Lamu, wao wenyewe. Tayari ghati tatu zitakuwepo pale. Hiyo ni bandari yao. Uwekezaji mwingine wa ziada katika eneo hilo wa miradi mbalimbali, huko wanaalika wawekezaji. Sisi hapa tumekomalia waChina wajenge, kwa masharti magumu wanayotupa sisi. Hapo ndipo penye tatizo.

Nilishauliza humu JF mara kadhaa, lakini sijawahi kujibiwa. Hivi haiwezekani mradi huo wa Bagamoyo ikawa 'Joint Venture' kati yetu na wawekezaji, huku mradi ukiwa bado ni wa Tanzania? Mbona bomba la mafuta ya Uganda tuna umiliki kule, kwa nini isiwezekane kwenye mradi huu wa Bagamoyo.

Niseme wazi, kama wewe ulivyo na wasiwasi na Mchina, nami nina wasiwasi mkubwa sana juu yake. Huyu ndiye anayekuja kuwa mkuu wa mabepari duniani kote, tena anakiu kubwa sana, ukichukulia na wingi wa wananchi wake. Mahusiano ya huyu na nchi atakazokuwa ameziingilia utakuwa ni tofauti sana na hawa mabepari tuliowazoea kwa miaka mingi.

Samia lazima awe makini sana, vinginevyo ninakubaliana na uliyoandika juu yake.
 
Mkuu Nikuulize swali, je umewahi kuuona huo mkataba? Mimi wote nawaona wehu tu si kikwete si ******** si samia mi nachotaka mkataba uwekwe wazi wananchi tuuone, tuusome na tuuelewe ili tujue kama unafaa ama la.

Na Ukiwekwa wazi Utaujuaje kama Ndio wenyewe?[emoji3516][emoji851][emoji851][emoji41]
 
Excellent! Wala sitakupinga. Ila nakuhakikishia (may be I am wrong) lakini wachina hawatakubali unacho-suggest. Wao lengo lau ni wamiliki hiyo bandari. Wanajua ikiwa yao hata kwa miaka 50 tu basi watakuwa wamefanya mengi. Hebu tuone mambo yatakavyokwenda.
 

Mchina Hajawahi Kuwa Mzuri Kamwe Kwa Vyovyote vile...Bora Mzungu Tuu...
Marekani,Germany,Nk nk!
Mkuu nakushauri Kwa moyo wa Dhati tuu.Muombe tuu MUNGU sababu Huna uwezo wa Kufanya/Kubadilisha Chochote,Mimi na Wewe hatujui kilichomo,
Mkuu Kama Hatuna Hela ya Uwekezaji je?
PPP.
Mi Nimemuachia MUNGU
 
Magufuli hakuwa muongo.
Mfumo wetu wa Nchi unavyoendeshwa umekaa kiuongo.
Mfano;
Vichwa vya tren kupatikana bandarini bila mwenyewe inaweza kukuingia akilini kweli.
Kuchepusha mafuta yasipite kwenye flow ni uongo huo siyo mfumo wetu mbovu.
Waziri anatoa tamko linalochonganisha na Rais huku usalama wapo,si mfumo mbovu.
 
Ume usoma mkataba? Mara nyingi kama huna taarifa za kutosha hakuna haja ya kupinga kitu
 
umuhumu wake ni Nini!??, miaka 100 hulambi kitu mapato yote yatakuwa Niya China,haya niambie kwa miaka yote hiyo miamoja ww utafaidika na nini,!?,labda faida ya kuona meli za kichina hapo nakubali!
 
Jiwe alikuwa na uwongo unaokaribiana na uchawi
pu......Basi ngoja ninyqmaze!! Bwawa la mwal.nyerere ambalo lilikuwa ndo mwalobaini wa umeme hapa nchini liko wapi ,nalo linasuasua ,juz wazyiri wenu akasema hakuna mtambo wa kuinulia mifuniko ya bwawa kuupachika mahala pake,si majibu ya kiwendawazimu haya,yaani wazyri mzma anaongea pumba utadhani kanywa mbege! hii nchi sijui ikoje ,imejaa mijitu ya hovyo na milafi Kama ww.mijitu inafikilia maisha ya miaka 2 au 3,haifikilia vizazi vijavyo vitakuwaje !! Kama sisi tusipojenga Sasa na kutengeneza Nani atafanya !?, wakati mwngine unaweza kumlaumu muumba ,anachukua viongozi wa maana anatuachia majanga !!daaah, halafu mijitu hii inaishi kweli
 
umuhumu wake ni Nini!??, miaka 100 hulambi kitu mapato yote yatakuwa Niya China,haya niambie kwa miaka yote hiyo miamoja ww utafaidika na nini,!?,labda faida ya kuona meli za kichina hapo nakubali!
Mkuu 'chazachaza', nisome unielewe. Naona hujaelewa ninachokieleza mimi.

Nasema hivi: Bandari ya Bagamoyo kwa Tanzania ni muhimu sana, tena sana. Sijaandika popote kwamba ni muhimu ijengwe na mchina kwa masharti anayotaka yeye.
Umuhimu wa hiyo bandari kwa Tanzania ni hapo inapokuwa na manufaa ya moja kwa moja kwa Tanzania na si vinginevyo.
 
umuhumu wake ni Nini!??, miaka 100 hulambi kitu mapato yote yatakuwa Niya China,haya niambie kwa miaka yote hiyo miamoja ww utafaidika na nini,!?,labda faida ya kuona meli za kichina hapo nakubali!
Umeyatoa wapi haya au kahawani. Huyu ni mmoja wa watanzania wanaochangaika Mada yeyote bila ya kuwa na uhakika wa anacho changia, Hatari kubwa sana
 
Hapo umenena mkuu! Asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…