Kwa sehemu kubwa sana tunakubaliana kati yako na mimi.
Mimi naamini kabisa kwamba bandari ya Bagamoyo ni muhimu sana kwa Tanzania, tatizo pekee lililopo ni, je, itajengwa vipi, na nani na kwa masharti gani.
Kenya wameanza ujenzi wa bandari yao ya Lamu, wao wenyewe. Tayari ghati tatu zitakuwepo pale. Hiyo ni bandari yao. Uwekezaji mwingine wa ziada katika eneo hilo wa miradi mbalimbali, huko wanaalika wawekezaji. Sisi hapa tumekomalia waChina wajenge, kwa masharti magumu wanayotupa sisi. Hapo ndipo penye tatizo.
Nilishauliza humu JF mara kadhaa, lakini sijawahi kujibiwa. Hivi haiwezekani mradi huo wa Bagamoyo ikawa 'Joint Venture' kati yetu na wawekezaji, huku mradi ukiwa bado ni wa Tanzania? Mbona bomba la mafuta ya Uganda tuna umiliki kule, kwa nini isiwezekane kwenye mradi huu wa Bagamoyo.
Niseme wazi, kama wewe ulivyo na wasiwasi na Mchina, nami nina wasiwasi mkubwa sana juu yake. Huyu ndiye anayekuja kuwa mkuu wa mabepari duniani kote, tena anakiu kubwa sana, ukichukulia na wingi wa wananchi wake. Mahusiano ya huyu na nchi atakazokuwa ameziingilia utakuwa ni tofauti sana na hawa mabepari tuliowazoea kwa miaka mingi.