Mkuu wa Mkoa ameomba wenye silaha wote mkoa wa Dar wazihakiki silaha zao. Raisi Magufuli ni mwenyeji wa Dar ni haki yake kufanya hivyo..
Lakini pia Kuna kanuni nyingi za kuzingatia ili mwananchi au asiye mwananchi kumiliki silaha. Raisi kama mwananchi yeyote yule najua fika ametimiza vigezo vyote.
Lakini pia sheria inaruhusu msajili mkuu wa silaha kumpa Mkuu wa nchi silaha ya dharura akiwa ndani ya mipaka ya Tanzania kama huyo mkuu wa nchi atakuwa hana hati ya kumiliki silaha.
Naomba utafute makala ya jinsi Raisi wa DRC Congo Mzee Kabila alivyouwawa na body guard wake halafu relate na kasi ya Raisi Magufuli serikalini na ndani ya CCM.
Kwa jinsi Raisi Magufuli anavyoyatumbua majipu ni haki na salama kwake kuwa na silaha binafsi.
Nimeona pia kwenye ITV alivyokuwa mwangalifu na silaha yake kuhakikisha kwenye chember hapakuwa na risasi. Raisi Magufuli anaonekana sio mgeni kwenye matumizi ya silaha.
BIG UP MAGUFULI. NI HAKI HAKO KIKATIBA NA KISHERIA.