Rais John Magufuli amekwenda kuhakiki silaha zake kwa Jeshi LA Polisi. Akiwa mbele ya Kamanda Simon Siro alichomoa bastola yake kiunoni na kuweka mezani.
Hiki ni kituko cha mwaka, Rais ambaye ni raia namba moja mwenye ulinzi mkali kuliko wananchi wote bado anatembea na bastola kiunoni!?
Je, hawaamini walinzi wake? Sasa sisi wananchi wa chini huku tunahakikishiwaje usalama wetu ikiwa rais wetu hana uhakika?
Inawezekana alitaka kutoa mfano kwa watu wengine, lakini hii imemharibia.
Issue hiyo angewapa wasaidizi wake tu wakamsaidia kuhakiki.
Ndio tabia za vijana siku hizi wakinunua bastola wanaringishiana wakiwa bar. Ni ushamba tu.
Inadhihirisha pia tabia ya watawala was CCM kuamini katika mabavu tu. Hata kule bungeni wapinzani wakitoa hoja na kutaka majibu ya serikali, Spika anaita Polisi ndani kuwapiga. Kwenye uchaguzi wanategemea nguvu zabkijeshi tu, sio mapenzi ya wananchi.
Mwisho sasa nchi inageuka kuwa ya kibabe tu.
Ile nchi tuliyokuwa tukiita kisiwa cha amani haipo tena, watu waliishi kwa kuaminiana na kupendana.
Sasa ni mwendo was bastola tu.