Rais Magufuli atekeleza agizo la Makonda la ukaguzi wa silaha, apeleka bunduki zake

Rais Magufuli atekeleza agizo la Makonda la ukaguzi wa silaha, apeleka bunduki zake

I don't get it that Rais anatembea na silaha wakati anao walinzi wanaomzunguka muda wote wakiwa na silaha za kumlinda?

Hakuna tatizo rais kuwa na silaha, ila mi naona tatizo ni uelewa wako kuwa mdogo na hapo ndipo uwezo wa akili yako kuchanganua mambo ulipofikia
 
I don't get it that Rais anatembea na silaha wakati anao walinzi wanaomzunguka muda wote wakiwa na silaha za kumlinda?
Unless kama heading ya post hii hujaielewa, maagizo ya Makonda wenye silaha waziwasilishe polisi zihakikiwe. ulitarajia afanyeje azitume kwenye Whasapp??
 
Ni mwendo wa maigizo ya bongo movies hata mimi nawasubiri waje ofisini kwangu kuhakiki wenyewe


Mkuu wana hakiki vitu gani maana hio manati kama wataanza kuhesabu risasi itakuwa ni shida!
 
luwasa-jpg.331157

MAPOVU IACHIE FOMA GOLD!
Kweli evolution ya ubongo kwa Africans bado inaendelea.....
 
Kuwa anamiliki silaha sio hoja, ila kulikuwa na umuhimu wa habari hii aitangaze hadharani? Huyu bwana nadhani zile mbwembwe za akiwa waziri anapaswa kuziacha sasa. Urais ni level nyingine na ndio maana kila ulifanyalo public lazima ushauriwe kuwa lina faa au laa. Isipokuwa kama ni mbishi sawa au washauri wanakuogopa kukuambia jambo utakalopinga kwa kuhofia kupoteza kazi. Jambo ambalo ni baya sana, ni borakutokuwa nao kuliko waoga.
Aache mara moja tabia hizo. Naagiza kama Raia mwajiri wake
 
sifa nyingine bwana
nashindwa kabisa kumwelewa huyu mzee ok ameenda kusajili ndio mpaka aonyeshe akitoa kiunoni
 
Hivi hili zoezi ni kwa mji wa Dar peke yake? Je kama mkazi wa Dar mwenye silaha amesafiri na silaha yake nje ya Dar atafanya nini?
 
Anaapenda sana kutumia media kwa kila kitu, why media?
ni kiongozi wa matendo na mifano na ndiye watanzania tuliyemtaka kiongozi namana hii safi kabisa. kama anapinga ufisadi apinge kwa mameno, sio unapinga ufisadi halafu wewe mwenyewe fisadi. Heko Magufuli kwa kuonyesha kuwa mtendaji wa vitendo
 
Pia sijajua ni kwa nini kuwepo huu ukaguzi wa kila mwaka wakati wenye silaha wote wanajulikana na kila mtu huenda kulipia ada kila mwaka!
 
ni kiongozi wa matendo na mifano na ndiye watanzania tuliyemtaka kiongozi namana hii safi kabisa. kama anapinga ufisadi apinge kwa mameno, sio unapinga ufisadi halafu wewe mwenyewe fisadi. Heko Magufuli kwa kuonyesha kuwa mtendaji wa vitendo
Umenikumbusha funguo Malaya.... Kila kufuli inafungua.....

Nikakukumbuka wewe kila awamu unaiimbia pambio... Upo kama audio cassette.... Ha ha ha ha ha!!!!
 
Hakutakiwa kuhakiki,alitakiwa kurudisha.Na alitakiwa kurudisha kabla hata ya kuingia Ikulu.Hivi akipata hasira yupo chumbani akammaliza mtu humo ndani inakuwaje??
Wewe umeathirikaje na silaha ya Magufuli? Hivi mbona mnakuwa watu wa ajabu namna hii, isitoshe pale ametii agizo la mkuu wake wa mkoa! Media kwa kiongozi ni muhimu kwani yeye ndie muongoza njia ktk harakati za nchi! Hivi nini hasa kinawauma hapo?

Hujaniconvince bado,inakuwaje RAIS amiliki silaha.
 
Sijaona sababu ya watu humu kukosoa kwa kila jambo huyu ndiye kwa sasa mtz namba moja kwa hiyo sioni sababu ya kumkosoa anaonyesha ni jinsi gani anatekeleza kwa vitendo maagizo ya viongozi wenzake bila kuwazalau big up jpm
 
Miss Chagga huyu anaenda kulindwa maisha yake yote yaliyobaki hakupaswa kuwa na silaha,vinginevyo aikabidhishe polisi mwanae akifika miaka kumi na nane airithi
mkuu binadamu hawaaminiki aisee ... ila nalo ni wazo jema
 
Kwa hali ilivyo sasa hapa nchini na maadui aliowatumbua majipu nadhani hata hiyo bastola na shotgun hazitoshi kuwa nazo. Ila kubwa tunapaswa kumuombea ulinzi wa Mungu na malaika zake.
 
Huyu wamnyan'ganye silaha maana haaminiki asije akauwa watu bule akidhani majipu
 
Back
Top Bottom