Rais Magufuli awaambia Waandishi wa Habari wawe makini, hawako huru kihivyo...

Hao wamiliki wa vyombo vya habari wamevunja sheria ipi?

Magufuli huwa hapendi kutafuta chanzo cha tatizo, yeye huwa anajikita kwenye matokeo.
 
Nasikitika rais na yeye anashinda mitandaoni, mara zote anasema kuna umbea na udaku.
Kama yupo makini awe anasoma report za World bank, UN na IMF kwa ajiri ya maendeleo ya nchi yetu.

Aache vyombo vya habari vifanye kazi zake
Lugha kaka
 
Kumbe huyu mjamaa wetu toka chaa tuu huwa anashinda humu jf kufuatilia wadau wanavomchana mubashara! Basi atapasuka na alivo na gubu kama ashangedere.
Umejuaje kuwa huwa anashinda humu, ametoa kauelekeo? Nitonye
 
Wazee wetu walipigania uhuru kutoka kwa wazungu,

Sisi tunapigania kutoka kwa weusi wenzetu.

Eti Rais anamtishia Kusaga na Mengi, kisa tu hawakubaliani na matendo maovu ya mpendwa wake BASHITE.
 
Mie nafikiri kabla habari hazijatoka wahariri wote wawe wanapanga foleni ikulu zikaguliwe kwanza.
 
Kuna dongo linamhusu mzee machache kwenye hii speech. Pale ilipoongelewa issue ya ugomvi wa wakulima na wafugaji kupewa muda mwingi wa hewani.

Kama hapendi jamii isikie kilio cha wafugaji na wakulima anajiitaje Raisi wa wanyonge?
 
'Magufuli rebukes Press' BBC News. Mwambieni asome sasa sijui huu nao ni udaku?!
 
Nzi, I can't access your thread, sijui mods wameifanya nini. Lakini napenda usikilize tena kauli ya raisi, tuponde na kupinga mabaya lakini sio kila kitu.

Naamini unaelewa, kuongea na kusikiliza kiswahili kwa ufasaha.
 
Ujinga wa waandishi wa habari na wapinzani nchi hii wanadhani wanamkomoa Magufuli hawajui wanarudisha nchi nyuma ndio màna watanzania tunaongoza kutokujitambua tunajipiga mishale hakika nchi hii haitawahi kuja kupata rais mzalendo kama Magufuli watanzania wanapenda kuishi leo tu wale washibe leo wavae leo maendeleo ni swala la muda mrefu linalohitaji uwekezaji na uaminifu wa muda mrefu chapa kazi Magufuli
 
watu bhana huna muda huku unasoma na kujbu acheni unafiki ndugu zangu....mnasoma na mnafatlia hamna game wala miereka mnachekesha sana.......MB mshamalza sana kwa upuuz na bado mtaendelea kumalza MB kwa kujadili mambo ambayo hayana faida kwenu.....
 
Kama hapendi jamii isikie kilio cha wafugaji na wakulima anajiitaje Raisi wa wanyonge?
Kuna mtindo wa ufikishaji habari....naweza kwa mfano nikakwambia ahhh we si mpuuzi tu na ukaishia kucheka...lakini naweza kukwambia wewe mpuuzi na unifanyi kitu na wewe ukaamka na kunitandika kibao cha shavuni...neno lile lakini mfikishaji analifikisha akiwa na sauti ya aina gani.
 
Nitashangaa kama waandishi wa habar watatishiwa kiasi hichi na wakakubali ku fall na ubabe huo
 
Kama maendeleo ya nchi yanakuja kwa kukandamiza wananchi wake then acha waendelee kumkosoa na kutompa airtime mpaka asimamie haki
 
walikubaliana habari za makonda sio za serikali we vp
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…