Rais Magufuli awaambia Waandishi wa Habari wawe makini, hawako huru kihivyo...

Rais Magufuli awaambia Waandishi wa Habari wawe makini, hawako huru kihivyo...

Mkuu jiulize kwanini Bashite hajatumbuliwa mpaka leo hii.

Issue yake msingi wake ni vita dhidi ya madawa ya kulevya. Vyeti vya jamaa vimekuwa ni headlines baada ya watu kadhaa kuguswa.
Wauzaji wa ile kitu mbaya kwa afya wanazo nguvu nyingi sana za kiuchumi. Bahati mbaya ni rahisi sana kucheza na akili za mtanzania, kwa sababu mtanzania anadanganywa na kile anachokiona machoni pasipo kujiuliza kilichomo ndani.

Issue ya Bashite inatumiwa na jamii chafu haswa ile ya kwenye majiji yetu makubwa, jamii ambayo imezoea kula maisha mema kwa gharama za vijana kuwa mateja na kuwa useless kwenye familia zao.

Mkuu JPM hajamtumbua Bashite na haoni yote yanayoendelea kana kwamba yanasababishwa na yeye, kwa sababu anaelewa umafia upo vipi na nani anayefaidika nao.
Mbona hakanushi chochote? Wewe ndo msemaji wake? Kama umesoma utajua vyeti vina umuhimu gani huwez kudharaulika wakat vyeti vipo angetoa na tena anastahili kuwa jela kwa kughushi nyaraka za serikali
 
anataka habari za kumtukuza yeye tu. kwani gazeti Uhuru na habari Leo hayamtoshi
 
The true and solid peace of nations consists not in equality of arms, but in mutual trust alone. ~ Pope John XXIII
 
Mbona hakanushi chochote? Wewe ndo msemaji wake? Kama umesoma utajua vyeti vina umuhimu gani huwez kudharaulika wakat vyeti vipo angetoa na tena anastahili kuwa jela kwa kughushi nyaraka za serikali
Aliyemteua kasema yote mnayoyaandika kwake hayana tija, anachojali ni uwezo wa kuchapa kazi.

Dedication yake ni muhimu zaidi kuliko kelele za watu kama nyinyi ambao most of the time ni wafanya kazi wa watu wanaochangia katika kuiharibu Tanzania. Nchi imejaa umafia halafu watetezi wa umafia huo wala hamuoni haya kuutetea.

Makonda alikuwa DC na kabla ya hapo kapita kwingi tu, mbona kote huko hamkuhoji vyeti vyake?, baada ya mabosi wenu kuguswa na kutakiwa kupeleka haja ndogo zao zikapimwe pale kwa mkemia mkuu ndipo mnaanzisha maneno ambayo hata hamyaelewi vyema.
 
Nã Dotto Bulendu

Mh Rais John Magufuli,nakusalimia,pole na hongera kwa kazi unayoifanya katika nchi yetu kama amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama!

Baada ya salama hizo,Mh Rais leo nimekusikia ukionesha masikitiko na hisia zako juu ya utendaji wa vyombo vya habari nchini Tanzania!.

Sononeko lako kuu ni jinsi vyombo vya habari nchini vilivyoandika habari kuhusu matukio ya jana na siku za nyuma,Mh Rais umeongea kwa hasira na hisia huku ukivionya vyombo vya habari kuwa visidhani kama vipo huru!.

Mh Rais baada ya kukusikia nilijiuliza maswali mengi sana,kwa nini unaonesha hasira zako wazi kwa vyombo vya habari kutokana na vyombo vingi labda kumpa nafasi kubwa Nape Mnauye na si tukio la jana la wewe kukamata makontena!.

Mh Rais vyombo vya habari vimegawanyika katika makundi matatu(Print media,electronics media and new/social media),vyombo vya habari hivi vinasimamiwa na mamlaka yaliyo chini yako!.

Print media(magazeti na majarida) yanafanya kazi chini ya idara ya habari maelezo ambayo wewe Mh Rais ndiyo unamchagua mkurugenzi wake,electronics and social media zenyewe zinafanya kazi chini ya TCRA ambayo mkuu wake yupo chini ya uteuzi wako!.

Mh Rais kabla hujaonesha hasira zako kwa waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari,fahamu vyombo hivi vina leseni tofauti!.
1.Vyombo vya habari vya dola(state media)
2.Vyombo vya umma(public media)
3.Vyombo vya taasisi(dini,elimu) Institution media
4.Vyombo vya kijamii(community media)
5.Vyombo vya biashara(commercial media)
6.Vyombo vya kiburudani(Entertainment media)

Mh Rais vyombo hivi vina sera na malengo tofauti ambayo kwa namna moja ama nyingine ndiyo huamua aina ya maudhui ya kuwalisha walaji(wasikilizaji,wasomaji,watazamaji na wachangiaji).

Mh Rais maudhui ya vyombo vya habari huamuliwa na mambo mengi sana.

1.Umiliki(ownership),maudhui ya chombo hutegemea na nani anamiliki?Mh Rais maudhui ya Radio Imani na Radio Maria katu hayatakuja kufanana,huo ni msingi na katu hutaweza kuubadilisha,maudhui ya Gazeti la uhuru hayatafanana na maudhui ya gazeti la Tanzania Daima!.

2.Sera ya chombo(media policy),Mh Rais,chombo kabla hakijasajiliwa hupeleka kwenye mamlaka husika(idara ya habari ama TCRA),na huwasilisha andiko la sera ya chombo(dira,mwelekeo na malengo),hili nalo huamua aina ta maudhui!.

3.Hitaji na takwa la walaji(audience needs and wants),hii huamua maudhui ya chombo.wahariri,wazalishaji huangalia umri,imani za dini,itikadi za kisiasa,jinsia,shughuli za kiuchumi,kipato.chombo kisichozingatia hili kitakosa walaji.

4.Asili ya walaji(nature of the audience),Mh Rais ,walaji kiasili ni heterogeneous by nature,wanatofautiana kwa kila kitu,Mh Rais hata siku moja walaji wa habari hawatakuja kuwa homogeneous,kilio chako hicho kingekuwa na mashiko kama walaji wangekuwa homegenous,kitu ambacho sicho!.

5.Mh Rais vyombo vya habari pia vinaongozwa na wapi vita pesa,kila wafanyacho wanalenga wapi watapata pesa za kujiendesha,Tanzania haina sera ya kuvisaidia vyombo ,vinajiendesha kwa ubunifu wao,chochote wanachofanya lazima kiwape manufaa ya kiuchumi,je watapata pesa wasiooandika masuala yenye takwa na hitaji la walaji?

6.Maslahi ya umma(Public Interest),Mh Rais kama unavyojua ,maslahi ya umma yameshindwa kutafsiriwa hata na katiba,unachoona wewe ni maslahi ya umma kwa mwingine siyo!.Maslahi ya umma huamliwa na tafsiri ya mtu mwenyewe!.

7.Sera na sheria za nchi,Mh Rais vyombo vya habari katika kila wafanyacho huakikisha wanazingatia sheria za nchi na sera zake,waandishi hawaweza pigia debe ushoga,usagaji kwa sababu ni kinyume na sheria,sasa sijui sononeko lako kwa waandishi kuhusu story ya leo,msingi wake ni nini?


Mh Rais,walichofanya waandishi leo kwanza wamekifanya kama "I Hard news",waandishi huangalia mambo mengi,je kipi ni hitaji la watazamaji,wasomaji na wachangajiaji,?

Audience ya Tanzania jana mpaka leo hitaji na takwa lao lilikuwa ni kujua hatma ya Nape,Mh Rais Nape ni news!,kwa sababu.

1.Yeye ni mbunge,alikuwa waziri,alikuwa katibu wa itikadi,(Prominent)aliyekuwa mstari wa mbele kuhakikisha katu CCM haipitishi baadhi ya wagombea,chumba cha habari hakiwezi mpuuza kikimpuunza ni kutokujua "audience needs and wants"

2.Nape kaondoshwa wakati ana shughulikia mgogoro kati ya waandishi na mkuu wa mkoa,Alilofanya makonda lina sifa mbili tu(unusual and impact),kitendo cha Makonda kwenda kwenye TV na askari tena wengine yadaiwa ni walinzi wa kikosi maalum,ni story kubwa ,media haiwezi kuipuuza!.
3.Mh Rais Nape alishikiwa silaha ya moto mchana kweupe,Nape anashikiwa silaha ya moto?!!hiyo ni story kubwa,huwezi ipuuzaaa,audinence itakushangaa!.

Mh Rais usivichukie vyombo vya habari,fuatilia suala la Sera ndiyo lililosababisha Gazeti la Uhuru na Habari leo hawajaiweka ukurasa wa mbele habari kuhusu Nape,kama wewe unavyolaumu waliiandika story ya Nape,kuna watu huku nje nao wanavilaumu vyombo ambavyo havijaandika story ya Nape,na hii ndiyo maana ya dhana ya "Heterogeneous by nature" .

Mheshimiwa Rais,vyombo vya habari vilivyoiacha story ya Nape,havijaicha kwa sababu eti si hitaji na takwa la walaji wao,ni sababu ya sera na umiliki!.

Uhuru na habari leo wameiacha hui story si kwa sababu eti haina mashiko,nooo wamezingatia dhana ya umiliki,ila hata walaji wao nao wanataka habari ya Nape,yaaji Mh Rais kabisa unadhani story kama ya Nape ilivyo kuna chombo kinaweza iachaa?nooo,Mh Rais audience "needs and wants"

Mh Rais ni kweli sasa media zinatakiwa kwenda kwenye dhana ya "media for development"ila havitaondoka kwenye msingi wake wa kuandika matukio na unachokitaka kwa mazingira na msingi wa uandishi wa habari ,ikitaka viende kwa matakwa ya dola itakuwa ni kuongilia uhuru wa waandishi!.

Wasalaam.
 
KUNA KITU cha hovyo sana kinaendelea IKULU; SASA hata matibabu watu wanatumwa?
WTF?

Come on now...I think he just tripped over his words.

He probably didn't mean it that way [the way it came out].

We already know he doesn't have the gift of gab.

I cut him some slack for that.
 
Come on now...I think he just tripped over his words.

He probably didn't mean it that way [the way it came out].

We already know he doesn't have the gift of gab.

I cut him some slack for that.
He is the damn president.., am sorry this is just too much slack for one day of effn slacks..,
 
Mkuu jiulize kwanini Bashite hajatumbuliwa mpaka leo hii.

Issue yake msingi wake ni vita dhidi ya madawa ya kulevya. Vyeti vya jamaa vimekuwa ni headlines baada ya watu kadhaa kuguswa.
Wauzaji wa ile kitu mbaya kwa afya wanazo nguvu nyingi sana za kiuchumi. Bahati mbaya ni rahisi sana kucheza na akili za mtanzania, kwa sababu mtanzania anadanganywa na kile anachokiona machoni pasipo kujiuliza kilichomo ndani.

Issue ya Bashite inatumiwa na jamii chafu haswa ile ya kwenye majiji yetu makubwa, jamii ambayo imezoea kula maisha mema kwa gharama za vijana kuwa mateja na kuwa useless kwenye familia zao.

Mkuu JPM hajamtumbua Bashite na haoni yote yanayoendelea kana kwamba yanasababishwa na yeye, kwa sababu anaelewa umafia upo vipi na nani anayefaidika nao.

Hapo ndipo tulipoumizwa wengi kwa double standard. tuwe fair tufuate utawala wa sheria na kanuni mkuu. Bashite anakingiwa kifua asitumbuliwe kwa kua amepambana na vita ya madawa ya kulevya. Walimu wetu walikua wanafaulisha vizuri kabisa na watoto waliofaulu kwa sasa ni watu wenye nyadhfa mbalimbali na wanalitumikia Taifa. Madaktari na manesi wameokoa vifo vya mamilion ya watu na walikua msaada hasa kule vijijini. Hawa wametumbuliwa bila huruma tena mpaka magazetini kwakua walitumia vyeti vya watu vya form 4 kwenda kusomea taaluma zao na hivi sasa wapo mtaani wanapigika na Maisha. Juhudi zao zote walizozifanya imegeuka mateso kwao. Bashite kapambana na madawa ya kulevya sio kwamba kamaliza vita bado inaendelea, lakini hakupambana kwa kujitolea alikua analipwa mshahara na marupurupu mengine tu kwa kupitia kodi za Watanzania. Lets be fair tuwarudishe kazini na hawa wanataaluma wengine ambao nao walikua ni msaada kwa Taifa kwa kujitolea maisha yao kuokoa Maisha ya Watanzania na kuwaelimisha Watanzania.
 
Aliyemteua kasema yote mnayoyaandika kwake hayana tija, anachojali ni uwezo wa kuchapa kazi.

Dedication yake ni muhimu zaidi kuliko kelele za watu kama nyinyi ambao most of the time ni wafanya kazi wa watu wanaochangia katika kuiharibu Tanzania. Nchi imejaa umafia halafu watetezi wa umafia huo wala hamuoni haya kuutetea.

Makonda alikuwa DC na kabla ya hapo kapita kwingi tu, mbona kote huko hamkuhoji vyeti vyake?, baada ya mabosi wenu kuguswa na kutakiwa kupeleka haja ndogo zao zikapimwe pale kwa mkemia mkuu ndipo mnaanzisha maneno ambayo hata hamyaelewi vyema.
Hujajibu swali hata kama imegundulika sasa hivi kuwa alifoji hana vyeti aachwe kisa madawa? Wangapi wamefukuzwa hawana vyeti? ?basi kama ni hvyo waliofukuzwa warudishwe tuachane na habari ya vyeti
 
Nyerere mwenyewe ambae siku siyo nyingi atatangazwa mtakatifu hajawahi kutishia wamiliki wala vyombo vya habari. When an empire wants to come to end it becomes adamant and assume absolute powers which in the long ran become inefficient

​

Habari waungwana, leo Rais John Magufuli anaapisha watu kadhaa na miongoni ni teuzi iliyozua rapsha ya wizara ya habari, sanaa, utamaduni na michezo ambayo ilimuondoa Nape Nnauye kwenye nafasi yake huku timing ikileta mjadala. Nafasi hio inachukuliwa na aliyekuwa waziri wa katiba na sheria, Dkt Harisson Mwakyembe huku Palamaganda Kabudi akiiziba nafasi yake anapotoka.

Pia Leo anaapishwa katibu mkuu wa Ikulu ila kwa sasa wanaoapishwa ni mabalozi mbalimbali wanaowakisha nchi zao.
===========

Mawaziri Dkt Harisson Mwakyembe na Palamaganda Kabudi wameshaapa, wanaoapa kwa sasa ni mabalozi wanaonda kuwakilisha katika nchi mbalimbali.
======

Anaeongea kwa sasa ni Rais Magufuli na kuwapongeza wote walioteuliwa. Amewaambia wasitegemee mazuri sana kwa kazi huwa zina lawama hasa kwa Tanzania ambapo kuna grupu la watu wao siku zote ni kulalamika.

Amedai Mwakyembe mitandao ilisema asingekuja kuapishwa pia wapo walioposti kuwa Kinana angeongea leo ilhali yeye kamtuma India kwa matibabu.



====​
 
Anatamani afungie mpaka mitandao ya kijamii..!! Hata madikteta huwa wanapiga sana vitaa Vyombo vya habari kwa kuwa wanataka Vitangaze tu mema yao hata kama kuna utumboo na upuuzi wanafanya...! Hizi ni dalili mbaya kwa nchi ya kidemokrasia kama hii...
 
Hapo ndipo tulipoumizwa wengi kwa double standard. tuwe fair tufuate utawala wa sheria na kanuni mkuu. Bashite anakingiwa kifua asitumbuliwe kwa kua amepambana na vita ya madawa ya kulevya. Walimu wetu walikua wanafaulisha vizuri kabisa na watoto waliofaulu kwa sasa ni watu wenye nyadhfa mbalimbali na wanalitumikia Taifa. Madaktari na manesi wameokoa vifo vya mamilion ya watu na walikua msaada hasa kule vijijini. Hawa wametumbuliwa bila huruma tena mpaka magazetini kwakua walitumia vyeti vya watu vya form 4 kwenda kusomea taaluma zao na hivi sasa wapo mtaani wanapigika na Maisha. Juhudi zao zote walizozifanya imegeuka mateso kwao. Bashite kapambana na madawa ya kulevya sio kwamba kamaliza vita bado inaendelea, lakini hakupambana kwa kujitolea alikua analipwa mshahara na marupurupu mengine tu kwa kupitia kodi za Watanzania. Lets be fair tuwarudishe kazini na hawa wanataaluma wengine ambao nao walikua ni msaada kwa Taifa kwa kujitolea maisha yao kuokoa Maisha ya Watanzania na kuwaelimisha Watanzania.
Umeandika mengi lakini kama ni tuhuma basi sasa hivi Mbowe angeshakuwa anaitwa mwenyekiti mstaafu wa CDM. Kwani analo rundo la tuhuma tena chafu zaidi ya hizi anazotuhumiwa RC makonda.
Mti wenye matunda mazuri ndio unaopigwa mawe, Makonda chapa kazi....
 
Raisi wangu Dr John Joseph Pombe Magufuli unajua kuwa kunatofauti kubwa kati ya " TAARIFA" na "HABARI" .

Fuatilia huu mfano,

Ikitokea Nyoka ameng`atwa na Binadamu hii huitwa HABARI
( Hili si jambo la kawaida machoni na hivyo huitwa habari)
Ikitokea Binadamu ameng`atwa na Nyoka hii huitwa TAARIFA
( Hili si jambo geni machoni na hivyo huitwa taarifa tu)

Waandishi na vyombo vya habari wako sahihi kabisa kuandika habari juu ya afisa mmoja wa polisi kutoa bunduki hadharani tena mbele yao kutaka kum-shoot waziri.
(Hii huitwa Habari na waandishi wa habari huipa kipaumbele zaidi).

Msema kweli Mpenzi wa Mungu

Lets give a time time
​
 
Back
Top Bottom