Rais Magufuli awataka TRA kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo

Yeye anachojua ni kushughulikia watu tu hamna kingine
 
VAT siyo kodi inayotozwa kwa mfanyabiashara.
Mfanyabiashara yeye ni kama wakala anayetakiwa kuikusanya na kuiwasilisha TRA kwa wakati kwa mujibu wa sheria.

Sasa mnacholalamikia hapo ni nini hasa?
 


Kwa Kampuni na mauzo yanayozidi 20M kama sijakosea kwa sasa kuanzia 100M na wenye kuandaa hesabu hulipa kodi kwenye faida.

Hao wengine hulipia kwenye mauzo.

Hata hivyo huko kulipia kwenye mauzo mbona utaratibu wake uko vizuri wala haukandamizi mlipakodi?!

Jamani ifike mahali waTz tujivunie kutii sheria bila shuruti .

Tujivunie kulipa kodi kwa wakati.
 
Dada ni petrol station za wapi hazitoi receipt? Mana bora ungetoa mfano mwingine lakini sio petrol station wao pump zimeunganishwa na mashine ya receipt akiuza receipt inatoka
👍
 
Mimi nashauri kote tutengeneze mifumo ya kulinda tunachokikusanya.

Tunaweza kusanya kodi lakini kuna mahali pana vuja.

Tutaishia kulumbana kumbe kunauwezekano kuna mahali mfumo tulionao unapelekea kibubu kisijae.

Tuwekeze kwenye kutengeneza mifumo thabiti ya kulinda tunachokikusanya.
 


Kwa upande mmoja ni sawa ulichoandika lakini mimi naona yote yaende sambamba pamoja na swala kwa uhamasishaji , enforcements Na maximization of Tax collections .

Pia ubunifu wa tax bases ambazo hazitamuelemea mwananchi kwa sana.
 
Kuna watu wanajadili hili swala la kodi kisiasa !

Lakini mimi naona haifai kulifanyia mzaha sababu ni swala nyeti sana kwa manufaa ya kila mmoja wetu na ndugu zetu.

Ni kupitia kodi serikali huweza kuwalipa madaktari ambao mtu ukiumwa wanakutibu,

Kulipa walimu, wanajeshi wanaolinda mipaka yetu, maaskari wanaotulinda na mali zetu na watumishi wote wa Umma kila mmoja kwa umuhimu wake kwetu.

Zaidi kulipia gharama za miradi ya maendeleo yetu n.k

Tulipe kodi kwa hiyari na kuona fahari.
 


Hata swala la kununua magari ya gharama kubwa kila Mwaka linapaswa kuangaliwa.

Mfano upotevu wa pesa za Umma kwenye rasimu ya katiba ambapo mpaka leo lengo halijafikiwa.

N.k
 
Hahahahah you killed on dat 1!

Mkuu aisee anadeal na mambo madogo sana ambayo hayawez kuipush hii nchi mbele, hakyamungu nakwambia tuanze kuhesabu majanga, yan sijui hata what the future holds for us. Nashangaa sana Young people wanavyomshangilia, Mzee kashajizeekea kazi ipo kwetu surprisingly watu hawaoni hilo
 
Inakuja hiyoo, maji muite mma.
Kodi kulipa kawaida tu sio kesi.
 

Watu hawelew kwamba ni system ndio ipo fuwked up, na tuanze kuifi system ili iweze kumwajibisha kila mmoja kwa upande wake wenyewe wamekazana na kuziba tobo kwa kidole badala ya kutafuta permanent solution
 
Hizi kodi huwa hazipangwi na wizara kama unavyopanga matumizi ya familia yako, Bunge ndio lenye dhamana la kupanga na kupitisha sheria mbali mbali zinazotumika. Wasiliana na Mbunge wako.
Waziri ndiye anapeleka miswaada, na ana team na resouce zote za kuweza kufanikisha hilo.
 
Wafanya biashara hawatishiwi, ni kuongea nao, na kuweka mifumo inayozuia hali hiyo matatizo, hawa watu wanatumia akili sana kufikia kuitwa wafanya biashara, wakiingiwa na uwoga wanawekeza akili zao nying kwenye kujilinda na sio ubunifu wa kuongeza uzalishaji.
 
Hoteli ya Mt. Hotel Kilosa, Guest ya Leopard na Elephant Njia panda Moshi tunaomba TRA iwatembelee wajionee wanatoa huduma nzuri sana na risiti za efd
 
Yaan km kuna mwanya Serikali inapoteza mapato bc ni hapa.Unakuta umenunua bidhaa anakwambia machine ya EFD mbovu anakuandikia risit ya mkono , wengine ndo ivo thaman ya 200000 anakuandikia 50000.
 
Kuna kila dalili mambo sio mazuri. Mtashikana uchawi soon
 
Wamachinga ndio wanaokwamisha, wanachukua vitu kwa mali kauli kwa wahindi wanamwaga vitu mitaani alafu aje TRA eti anataka kodi alafu machinga anauza vitu nje bila risti hapo serikali itaendelea kupigwa tu
Hii post wale wanaompelekea taarifa wamlatie na hii. Hapa kariakoo tunachokifanya sisi wa maduka ya jumla ni kuwa na vijana wako kumi au ishirini. Kila siku unawapa mzigo kwa masharti wakauze kwa bei tunayowapa faida atajipangia mwenyewe auze kwa bei gani. Jioni analeta hela yangu na hanidai risiti kwanza nakua kama namsaidia maana yeye halazimiki kuwa na hela mkononi ili afanye biashara. Magu aliposema machinga waachwe kila kona ya mtaaa alitusaidia sana sisi wa maduka ya jumla maana sasa hivi hatukwepi kodi tu bali hatulipi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…