Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Siyo michezo. Ni waziri wizara nyeti. Michezo atapewa Mnyeti.

Wewe kiasi fulani tunashabihiana kimawazo, Mimi nikimuona ndugu Polepole naona mbali sana, mbali mno, watu wasimchukulie Poa ndugu Polepole.

Napata fununu nyingi tu za CCM kuwekeza vilivyo kwa Ndugu Polepole, kwamba watu wengi wanam- underrate sana ndugu Polepole.

Binafsi nilitegemea uteuzi wake kama mbunge wa JMT, hilo limeisha, Bado namuona kwenye nafasi nyeti zaidi ya hapo.

Na kama nilimsikia vizuri jaji mkuu siku ya kuapishwa waziri mkuu, nanukuu (we are still looking for a PERFECT UNION) Hisia tu zinaniambia kipindi hiki tunaandika katiba mpya ya JMT na tunaenda kua na serikari moja.

Japo anayeteu hatabiliki na wala hapangiwi ila binafsi nahisi ndugu Polepole ndio waziri wa ULINZI, na baada ya hapo hisia tu zinazidi kuniambia ndugu Polepole ndio Rais wa JMT anaefata kwa JPM

Ni hisia tu wakuu na namna ya uunganishaji wa dots kama nilivyo uhisi uteuzi wa ubunge wa ndugu Polepole.
 
Sasa anajenga hoja kutetea huu upande alipo. Majority wanamkubali.

Kujenga hoja ni pale kunapokuwa na logic watu washawishike. Ukiona unajenga hoja kutetea dhuluma na uzandiki, hiyo sio kujenga hoja bali ni kuhubiri ghiliba. Unapimaje ujengaji hoja huku chama kikitumia nguvu ya madaraka ya urais kutangazwa washindi? Toka Polepole amekuwa kwenye nafsi hiyo chini ya Magufuli, ni uchaguzi upi umeemdeshwa kihalali useme ushindi wao ni wa ushawishi wa hoja? Ama unatuona tuna uwezo mdogo wa kupima mambo?
 
ila siasa ikikukubali unakula shumbwela sana..ndani ya miaka mitano pole pole katoka kuwa Dc bukoba,kaenda kuwa Dc Ubungo nadhani,, kaenda uenezi,,sasa ni mbunge na kesho atakua waziri..ni ndani ya miaka mitano haya yanatokea
Alikuwa Dc Musoma na sio Bukoba
 
View attachment 1637307

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Wabunge 2 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Humphrey Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

View attachment 1637284
Uteuzi huu unakishindo let keep silence
 
Mungu aitwe Mungu....! Kwa kutuletea Raisi muafaka kwa wakati muafaka. Huyu tulikuwa tunamuhitaji siku nyingi lakini Mungu kamleta awamu hii...watanzania tuseme AMINA.
 
Nimekutapeli nini ?Mimi nikitaka kitu huwa sishindwi. Ningetaka uteuzi kutoka kwa Magufuli ningeshaupa tokea 2015.

Kwa vigezo vipi labda, kama ni kwa kujipendekeza hapo sawa. Lakini kama ni kujipendekeza mstari nao ni mrefu sana, maana mpaka Paskali Mayalla yuko kwenye mstari, unapataje ww kwa mfano?
 
View attachment 1637307

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Wabunge 2 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Humphrey Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

View attachment 1637284
Polepole anaenda pewa wizara. Jembe!
 
Nathubutu kusema, polepole anafaa kuandaliwa kuwa rais wa nchi hii au waziri mkuu..
Hutaki acha! Safari ya kumuandaa kuelekea huko imeanza
 
Ila Polepole kujipendekeza kumemsaidia kutoka. Jamaa mbishi na king'ang'anizi. Alikuwa anashinda na kulala channel 10, 2015 kumponda Lowassa tu.

Nafasi yake sasa hivi apewe Joti ama Mpoki
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3][emoji3]wazo zuri Sana
 
Back
Top Bottom