Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Tumendesha harambee ya Ujenzi wa Msikiti wa Chamwino katika Misa Takatifu na uzinduzi wa Kanisa, Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Ibada ya Misa Takatifu iliongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya

Kwenye michango tuliyochangisha hapa Kanisani kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti Chamwino, Dodoma tumepata jumla ya Tsh.Million 48 na Elfu 21,mifuko 48 ya cement na Lori 5 za mchanga, Rostam amechanga Mil. 20, Boss wa CRDB Nsekela Milioni 10, pia CAG Kichere, Antony Mavunde, RC Dodoma ni miongoni mwa waliochangia, nawashukuru wote waliochangia.

Mungu Ibariki Tanzania [emoji1241][emoji419]

“Nakuomba Baba Askofu kama utaniruhusu na kama sitokukwaza basi tutumie siku ya leo pia tuchange angalau tuanze kujenga Msikiti wa Ndugu zetu Waislamu ambao Msikiti wao kwa sasa ni mdogo nao wapo pale kwa ajili ya kumtukuza Mungu” -JPM kwenye Uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino Dodoma

“Mimi baadhi ya Wasaidizi wangu wengine ni Waislamu, nataka niwatajie mmoja tu kuna Al-haji huyu ameshaenda kuhiji ila ni msaidizi wangu ninapoingia humu Kanisani lazima aingie lakini ikifika siku yake Msikiti wake mdogo,Baba Askofu niruhusu nichukue kikapu tuchangie Msikiti”-JPM

“Nachukua kikapu hapa Kanisani ili tuchangie ujenzi wa Msikiti baadaye Baba Paroko atazipeleka kwa Sheikh ili Chamwino iwe ni ya Watu wa Ibada, tumejenga Kanisa Katoliki tunalizindua leo, tujenge Msikiti, kisha tutaendelea kujenga Makanisa ya Madhehebu

mengine nk” -JPM

.
 
Waislam wamesikitishwa sana wanasema wamezalilishwa kuchangiwa pesa na makafiri tena mimbarini.
 
Wewe ni afisa upelelezi wa serikali au unaongea kwa sababu una mahaba na ccm?
Mwambieni jamaa yenu aende mahakamani na asaidie polisi upeleleziii. Vinginevyo tutambana atuambie nani kampigaaaa. Mahakamani papo aende kusaidia upeleleziii.
 
Huu ni mwanzo tu itafikia utakuja kutuambia ulisimama upande upi wa wakati wa kushuti na bashite pekee alikupa mafao ya tsh ngapi na kisha kamongo wa burigi akakupa ngapi muuaji mkubwa weye
Mwambieni jamaaa yenu aende mahakamaniii. Afungue kes
 
Usiposali unamkomoa nani ? Unasali kwa faida ya nani ? Pole sana kwa kutokupambanua dini na siasa.
Uwe na uelewa, kusali sio lazima uende madhabahuni. Unyenyekevu wako kwa Mungu huku ukiiishi imani yako pasi na shaka na matendo yakireflect unyenyekevu wako, hiyo inatosha.
 
Kama wao ambavyo wasingeweza kuchangia kwa ajili ya Kanisa😕
 
Polisi wanashindwa nini kumuhoji?
Polisi hawatafuti kesi polisi wanaletewa malalamikooo. Kama kweli jamaa yenu anataka haki itendekee aende kulipoti mahakamaniiii. Lakini akumbuke yeye ndo mtu wakwanza kusaidia upeleleziii. Asiogopee aende na dereva wake wakaisaidie polisi upelelezi. Kwani nini hataki kwenda kuripoti?
 
Ni undugu wa damu umeonyeshwa na kanisa.wakristo na waisilamu wote ni ndugu.Adam ndo baba yetu.
Kafiri hana udugu katu na mwislamu. Mfano angalia nini anachokifanya Zanzibar. Majeshi ,mapolisi,watu wasiojulikana wamejaa kila mtaa
 
Ni lini wewe ukamjua Mungu sawasawa? Sadaka ni sadaka na Wala haiji kwako aisee
 
Nimeona kwenye vyombo mbalimbali vya habari vikisema rais amezindua kanisa huko dodoma. Huu ni uvivu wa kutafiti wa wanahabari wetu. Anayeweza kuzindua kanisa katoliki ni askofu tu, rais anaweza kushiriki tu sherehe za uzinduzi. Acheni kuandika bila kutafiti
 
Alikosea sana kuamuru Lissu achapwe zile mvua za risasi mchana kweupe, imani yetu kwake ilikoma tangu siku hiyo.
 
Ungesoma jiwe lililowekwa limeandikwaje kabla ya kuleta huu uandishi wako
 
Dikteta Nduli Jiwe, KATIBA YA WANANCHI, Haki za binadamu, utawala bora na demokrasia AMEVIWEKA MFUKONI katika muda wake wote wa miaka mitano.
 

Pesa za wizi na mariba hazifai kujenga msikiti.
 
Pokeeni hiyo swadaka tu haina shida maana nasikia hata BAKWATA ilianzishwa na wakristo.
 
Hivi nikuulize swali leo hii umekutwa umekufa polisi hawatachunguza kwasababu ndugu zako hawajaripoti mahakamani?

Wacheni hoja za kijinga na za kipuuzi. Kwanza hao polisi walishasema wanachunguza hilo shambulizi lakini mpaka leo hatuambiwi wamefikia wapi.walisema anasubiri Lissu haya amekuja lakini bado kimyaa. Huoni hii inatia mashaka kuwa wahusika ni serikali? Hilo bichwa usifugie nywele 'just think"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…