Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Tumendesha harambee ya Ujenzi wa Msikiti wa Chamwino katika Misa Takatifu na uzinduzi wa Kanisa, Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Ibada ya Misa Takatifu iliongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya

Kwenye michango tuliyochangisha hapa Kanisani kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti Chamwino, Dodoma tumepata jumla ya Tsh.Million 48 na Elfu 21,mifuko 48 ya cement na Lori 5 za mchanga, Rostam amechanga Mil. 20, Boss wa CRDB Nsekela Milioni 10, pia CAG Kichere, Antony Mavunde, RC Dodoma ni miongoni mwa waliochangia, nawashukuru wote waliochangia.

Mungu Ibariki Tanzania [emoji1241][emoji419]

“Nakuomba Baba Askofu kama utaniruhusu na kama sitokukwaza basi tutumie siku ya leo pia tuchange angalau tuanze kujenga Msikiti wa Ndugu zetu Waislamu ambao Msikiti wao kwa sasa ni mdogo nao wapo pale kwa ajili ya kumtukuza Mungu” -JPM kwenye Uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino Dodoma

“Mimi baadhi ya Wasaidizi wangu wengine ni Waislamu, nataka niwatajie mmoja tu kuna Al-haji huyu ameshaenda kuhiji ila ni msaidizi wangu ninapoingia humu Kanisani lazima aingie lakini ikifika siku yake Msikiti wake mdogo,Baba Askofu niruhusu nichukue kikapu tuchangie Msikiti”-JPM

“Nachukua kikapu hapa Kanisani ili tuchangie ujenzi wa Msikiti baadaye Baba Paroko atazipeleka kwa Sheikh ili Chamwino iwe ni ya Watu wa Ibada, tumejenga Kanisa Katoliki tunalizindua leo, tujenge Msikiti, kisha tutaendelea kujenga Makanisa ya Madhehebu

mengine nk” -JPM

.
IMG_20200823_132958_993.jpg
IMG_20200823_130041_749.jpg
 
Waislam wamesikitishwa sana wanasema wamezalilishwa kuchangiwa pesa na makafiri tena mimbarini.
 
Wewe ni afisa upelelezi wa serikali au unaongea kwa sababu una mahaba na ccm?
Mwambieni jamaa yenu aende mahakamani na asaidie polisi upeleleziii. Vinginevyo tutambana atuambie nani kampigaaaa. Mahakamani papo aende kusaidia upeleleziii.
 
Huu ni mwanzo tu itafikia utakuja kutuambia ulisimama upande upi wa wakati wa kushuti na bashite pekee alikupa mafao ya tsh ngapi na kisha kamongo wa burigi akakupa ngapi muuaji mkubwa weye
Mwambieni jamaaa yenu aende mahakamaniii. Afungue kes
 
Usiposali unamkomoa nani ? Unasali kwa faida ya nani ? Pole sana kwa kutokupambanua dini na siasa.
Uwe na uelewa, kusali sio lazima uende madhabahuni. Unyenyekevu wako kwa Mungu huku ukiiishi imani yako pasi na shaka na matendo yakireflect unyenyekevu wako, hiyo inatosha.
 
Mungu wa "israeli" hachangamani na "miungu baali"

Hayo ni maigizo ya kisiasa, kuwin both sides lakini hiyo ni ibada ya kipagani.

Mtawajua kwa matendo yao, huwezi mjengea baali madhabahu na wakati huo huo ukamwamini YESU, pande hizo mbili hazichangamani, never!
Kama wao ambavyo wasingeweza kuchangia kwa ajili ya Kanisa😕
 
Polisi wanashindwa nini kumuhoji?
Polisi hawatafuti kesi polisi wanaletewa malalamikooo. Kama kweli jamaa yenu anataka haki itendekee aende kulipoti mahakamaniiii. Lakini akumbuke yeye ndo mtu wakwanza kusaidia upeleleziii. Asiogopee aende na dereva wake wakaisaidie polisi upelelezi. Kwani nini hataki kwenda kuripoti?
 
Ni undugu wa damu umeonyeshwa na kanisa.wakristo na waisilamu wote ni ndugu.Adam ndo baba yetu.
Kafiri hana udugu katu na mwislamu. Mfano angalia nini anachokifanya Zanzibar. Majeshi ,mapolisi,watu wasiojulikana wamejaa kila mtaa
 
Masheikh mumwambie Mh Rais ukweli kuhusu hili suala.la kupokea huu mchango wa kanisa kwa kujengea msikiti. Ikiwa mutapokea hizi fedha jee aiku akija kwenye makongamano yenu, akochangisha ujenzi wa kanisa mutachangia? Ni suala la wazi kuwa waislamu wanaamini kuwa ibada ya kanisani ni kufuru na kwa maana hiyo ni haramu na sheria ya waislamu hairuhusu kupokea ama kuchangia kitu kinachotokana na kupelekea kufuru.

Jee masheikh munakanusha kuwa waislamu wamekatazwa hata kula mnyama aliyechinjwa na mkristo? Jee masheikh mutakanusha kuwa waislamu wamekatazwa kushirikiana na wakristo katika baadhi ya mambo yakiwemo ya ibada?

Kwa ufupi Uislamu hau encourage ubaguzi na ni dini yenye tolerance ikifatwa according to the book lakini inasisitiza sana to keep distance na kutoingiliana kwenye mambo ya ibada kwa vile kila mtu atahukumiwa kutokana na matendo yake mwenyewe. Kwa matukio kama haya ndio Mtume Muhammad akashushiwa aya "Nyinyi muna dini yenu na sisi tuna dini yetu" Haya mambo ya kuingiliana kwenye ibada yatasababisha msuguano zaidi ya muungano. Jirani anabakia kuwa jirani mwema lakini atakapoanza kukuletea chakula nyumbani kwa mama watoto upike kwa kukuhisi huna uwezo hapo utaona ni dharau na ndio uadui utakapoanza.

Ahsante sana Mheshimiwa Rais kwa nia njema lakini masheikh musiwache kueleza.ukweli kuhusu hili.
Ni lini wewe ukamjua Mungu sawasawa? Sadaka ni sadaka na Wala haiji kwako aisee
 
Nimeona kwenye vyombo mbalimbali vya habari vikisema rais amezindua kanisa huko dodoma. Huu ni uvivu wa kutafiti wa wanahabari wetu. Anayeweza kuzindua kanisa katoliki ni askofu tu, rais anaweza kushiriki tu sherehe za uzinduzi. Acheni kuandika bila kutafiti
 
Rais Magufuli amehudhuria misa takatifu ya uzinduzi wa Kanisa la parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino jijini Dodoma.

Misa hii inarushwa mubashara TBC na Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
=========

Baba askofu mkuu amewataka waumini kuzusha macho kuuona uzuri wa kanisa na kuwaasa uzuri wa kwanza ni roho hivyo waumini watamani roho zao zipendeze kama kanisa lao, Baba askofu mkuu amemkaribisha Rais Magufuli ili awamegee busara zake.

Rais Magufuli: Matokeo ya ujenzi wa kanisa hili umefanywa na wakristo wote, wakati wa ujenzi kila mmoja alitoa alichokuwa nacho. Nakumbuka katika siku hiyo mama mzee mmoja alitoa 5,000 yote aliyokuwa nayo katika ujenzi wa kanisa hili, ujenzi umefanywa na waumini wote wa kanisa hili.

Nawashukuru wananchi wengine mbalimbali siku hiyo tukitoa mchango hapa nilikuwa napigiwa simu na baadhi ya watu wengine waislamu nakumbuka nilipigiwa na mtu mmoja kutoka Dar es Salaam na akaja kukabidhi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hili, wadau ni wengi waliojitolea na mimi nawashukuru sana kwa niaba yenu.

Nawashukuru wasimamizi ambao fedha tulizozichanga hawakuzila na shetani alikimbia mbali kuhubiri roho zao kuzila fedha hizi, tunawashukuru wajenzi hawakupoteza muda chini ya uongozi wa mkuu wa JKT na vijana wake, walikuja na kushiriki katika ujenzi huu. Vijana walioshiriki ujenzi huu si wakristo tu, walikuwepo Waislamu wamejenga, Roman, Wasabato, KKKT, Anglingana na waliookoka wamejenga.

Kikosi cha JKT nilichokiomba tukawapa fedha zilizokuwa zimechangwa na ninyi na zimechangwa na wananchi wengi napenda kuwapongeza kwa niaba yenu kwa sababu wamefanya kazi nzuri sana na huu ndio umoja wa watanzania.

Mhasham baba Askofu mkuu ndio maana mimi nilisita sana kuambiwa mimi ndie mfadhili mkuu kwa sababu ninaamini waliofadhili kanisa hili na kushiriki kwa njia moja au nyingine kukamilisha. Nilisita kubeba heshima hiyo ambayo sistahili, mimi nilitoa mapendekezo nikachangia kidogo nilichokua nacho lakini kimechangiwa kingi na wale walioshiriki kwa hiyo pongezi ni kwetu sisi sote.

Nimefurahi kumuona father Kitima, huyu ni rafiki yangu wa siku nyingi. Alikuwa ndio vice chancellor wa St. Augustine, chuo kikuu cha kule Mwanza na baadae akateuliwa kuwa katibu mkuu wa baraza la maaskofu na leo nimefurahi kuja hapa. Yale mengine mengine maviporo viporo yanayobaki kule na kwa kuwa wewe ndie katibu mkuu wa maaskofu wote, hata hili la fence linaweza likakugusagusa kidogo. Ukaangalia angalia yale yanayobaki huko ili utusaidie sisi.

Parokia ya Chamwino ina raha yake, ina upendo mkubwa hata nyimbo mnaona zinavyogusa na uwepo wa Mungu upo, kwa ruhusa yako baba askofu ilikuwa niombe kitu kimoja. Kanisa hili wameshiriki watu wa madhehebu mbalimbali kulijenga na kiukweli mahali ambako ni makao makuu panatakiwa kuzungukwa na watu wanaomtukuza Mungu. Sio wa dhehebu moja bali yote kadri muda utavyokuwa unaenda, makao makuu lazima paende na uwepo wa Mungu.

Kama utaniruhusu, tutumie siku ya leo pia tuchange angalau tuanze kujenga msikiti wa ndugu zetu waislamu ambao msikiti wao ni mdogo nao wapo pale kwa ajili ya kumtukuza Mungu na baadhi ya wasaidizi wangu wengine ni waislamu na nataka niwatajie mmoja tu, kuna Alhaji, ameshaenda kuhiji mpaka Makka lakini ni msaidizi wangu. Ninapoingia humu inabidi lazima aingie humu kanisani lakini inapofika siku ya kwenda kumtukuza Mola wake, nimeambiwa ule msikiti bado haujawa mkubwa vizuri.

Baba Askofu, uniruhusu leo nichukue kikapu ili kama sitachukua muda wako mwingi niwaombe wakristo wenzangu tuanze kuchangie, tutamuomba baba Paroko akaziwasilishe kwa shekhe kwenye msikiti wetu na tutajipanga taratibu namna tutakavyoweza kuukarabati.

Tukimaliza hivyo tutaendelea tena katika kanisa jingine kama ni Anglikana, KKKT, Wasabato ili utukufu wa Chamwino katika kumtukuza Mungu ukasimame.
======

Rais Magufuli amechukua kikapu na mtu wa kwanza kuchangia ni baba Askofu ambae ametoa laki mbili na msaidizi wake ambae ni Alhaji atachangia lakini tatu.

Katibu mkuu wa baraza la maaskofu nae kachangia laki moja na ameeleza amemfahamu Rais tangu mwaka 2001 na alikuwa karibu sana na maaskofu na amemfahamu kupitia kwao hata leo anachokifanya inaonyesha namna gani anawapenda watanzania na amefanya vingi vinavyofanya nchi iende mbele kama rushwa iliyokuwa inaelekea kutushida,a anasema ukipita kila mahali wanasema tupeni sisi Rais Magufuli.

Jumla ya fedha zilizochangwa ni 48,021,000/= Mifuko ya simenti 48 na lori tano za mchanga.
Alikosea sana kuamuru Lissu achapwe zile mvua za risasi mchana kweupe, imani yetu kwake ilikoma tangu siku hiyo.
 
Ungesoma jiwe lililowekwa limeandikwaje kabla ya kuleta huu uandishi wako
 
Tumendesha harambee ya Ujenzi wa Msikiti wa Chamwino katika Misa Takatifu na uzinduzi wa Kanisa, Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Ibada ya Misa Takatifu iliongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya

Kwenye michango tuliyochangisha hapa Kanisani kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti Chamwino, Dodoma tumepata jumla ya Tsh.Million 48 na Elfu 21,mifuko 48 ya cement na Lori 5 za mchanga, Rostam amechanga Mil. 20, Boss wa CRDB Nsekela Milioni 10, pia CAG Kichere, Antony Mavunde, RC Dodoma ni miongoni mwa waliochangia, nawashukuru wote waliochangia.

Mungu Ibariki Tanzania [emoji1241][emoji419]

“Nakuomba Baba Askofu kama utaniruhusu na kama sitokukwaza basi tutumie siku ya leo pia tuchange angalau tuanze kujenga Msikiti wa Ndugu zetu Waislamu ambao Msikiti wao kwa sasa ni mdogo nao wapo pale kwa ajili ya kumtukuza Mungu” -JPM kwenye Uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino Dodoma

“Mimi baadhi ya Wasaidizi wangu wengine ni Waislamu, nataka niwatajie mmoja tu kuna Al-haji huyu ameshaenda kuhiji ila ni msaidizi wangu ninapoingia humu Kanisani lazima aingie lakini ikifika siku yake Msikiti wake mdogo,Baba Askofu niruhusu nichukue kikapu tuchangie Msikiti”-JPM

“Nachukua kikapu hapa Kanisani ili tuchangie ujenzi wa Msikiti baadaye Baba Paroko atazipeleka kwa Sheikh ili Chamwino iwe ni ya Watu wa Ibada, tumejenga Kanisa Katoliki tunalizindua leo, tujenge Msikiti, kisha tutaendelea kujenga Makanisa ya Madhehebu mengine nk” -JPM.View attachment 1545823View attachment 1545824
Dikteta Nduli Jiwe, KATIBA YA WANANCHI, Haki za binadamu, utawala bora na demokrasia AMEVIWEKA MFUKONI katika muda wake wote wa miaka mitano.
 
Pesa za wizi na mariba hazifai kujenga msikiti.
 
Pokeeni hiyo swadaka tu haina shida maana nasikia hata BAKWATA ilianzishwa na wakristo.
 
Polisi hawatafuti kesi polisi wanaletewa malalamikooo. Kama kweli jamaa yenu anataka haki itendekee aende kulipoti mahakamaniiii. Lakini akumbuke yeye ndo mtu wakwanza kusaidia upeleleziii. Asiogopee aende na dereva wake wakaisaidie polisi upelelezi. Kwani nini hataki kwenda kuripoti?
Hivi nikuulize swali leo hii umekutwa umekufa polisi hawatachunguza kwasababu ndugu zako hawajaripoti mahakamani?

Wacheni hoja za kijinga na za kipuuzi. Kwanza hao polisi walishasema wanachunguza hilo shambulizi lakini mpaka leo hatuambiwi wamefikia wapi.walisema anasubiri Lissu haya amekuja lakini bado kimyaa. Huoni hii inatia mashaka kuwa wahusika ni serikali? Hilo bichwa usifugie nywele 'just think"
 
Back
Top Bottom