Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Wakati mitandaoni kukiwa na tafsiri nyingine kuhusu hili la kanisa kuchangia ujenzi wa msikiti, mitaani ndio habari njema na wenye Imani Yao wanaona hiyo ndio nzuri imekaa kiupendo na kuondoa dhana ya chuki iliyojengeka miongoni mwa dini hizi

Lakini pia huku mitaani kuna visima vingi vilivyojengwa na waislamu na mpaka vingine vipi jirani na makanisa, watumiaji ni watu wote, vivyohivyo kwa visima vilivyojengwa na Wakristo, tnajinywea Tu

Ni zamu ya Dunia nzima kujifunza Tanzania namna Imani inavyopaswa iwe
 
Umesoma Quran Sura ya 9 aya 17 soma kwanza halafu uchangie.
 
Pu
P
Pumzi imekata
Delete ccm Oct 28
 
MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!
Unaonekana so muislam umedandia tu hoja ili kukidhi kiu yako ya kisiasa
Uislam inaruhusu kujengewa msikiti na asie muislam au hata kupewa pesa za kujengewa msikiti
Msikiti wameombewa waislam,wewe kinakuuma Nini?
 

Hapa umeweka kisu kwenye mfupa. Halafu nilishangaa sana anasema anachangisha ili waislamu wawe na msikiti mkubwa, kwani msikiti mkubwa ndio Mungu anasikiliza zaidi sala zao? Huenda alikuwa na nia nzuri, au anasaka kura kupitia nyumba za dini, lakini alifanya jambo sahihi sehemu ambayo sio sahihi. Yaani hata uvae suti nzuri vipi, lakini huwezi kwenda kukimbia nayo marathon maana sio vazi sahihi kwa ajili ya marathon. Halafu kawadhalilisha sana waisilamu kuwa hawawezi kujenga msikiti mkubwa mpaka wajengewe na waisilamu. Yeye alitakiwa aende msikitini akaitishe hiyo harambee yake, sio kuchangusha hela kwa makafiri ili kuwajengea waisilamu msikiti mkubwa, huku akiacha matatizo ya msingi ya waislamu.
 
Na waroma wengi biashara yao Ni kitimoto hii sijui imekaaje au pesa sio Haram
 

Aende msikitini akachangishe hela za kujenga kanisa kama ataeleweka. Kaishiwa mbinu za kusaka kura huyo. Waisilamu wana matatizo ya msingi, sio kichangishiwa hela ya kujengewa msikiti mkubwa huko kanisani kwake. Shehe Ponda juzi katoa waraka, na ulibeba matatizo ya msingi ya waislamu, hakuna popote waisilamu walitaka michango ya kujengewa msikiti na wakristo. Kama ni kura tayari NEC ina idadi ya kupika ya watu 29m+, kwanini alete siasa za kudhalilisha dini nyingine huko kanisani kwake, huku tayari ana kura nyingi za kupika?
 

Wakati makonda anajenga msikiti pale dar waislamu walimuomba?
Kuna misikiti na makanisa huku watu huchangisha kwa malafiki zao ambao ni waislam na wasio waislam je huwa ni dhambi?
Lengo la Raisi ni kwamba dini zote ziwe pale chamwino ili watu wanao ishi au kufanya kazi maeneo hayo na wageni wapate sehemu yao ya kusali sasa kosa liko wapi?
Je wewe kuchangia huko kunakuuma nini mpaka uanzishe uzi hapa?
Mwisho, kuna wapiga diri na wauza madawa ya kulevya hapa nchini hujenga maisikiti na makanisa kisha kuyakabidhi kwa viongozi na ni pesa haramu, je makanisa hayona misikiti huwa ni haramu?
Nakuachia na wewe ujibu unalojua.
 
Watoe hukumu kwa masheikhe walioko mahabusu kama wana mahaba na uislam ova,
 
Mkuu, siku zote wanasiasa wasio na ushawishi wa kisiasa hutumia maeneo mengine kuziba pengo hata kama kufanya hivyo ni hatari. Kumbuka lengo la wanasiasa ni ku survive.

Kuna nyakati wanasiasa hutengeneza matatizo ili waje na solution kama hoja za umahiri wao.

Kinachosababisha haya yote ni reaction inayotoka kwa Waislam.

Kwa muda kumekuwa na some reservations kwamba kuna tatizo katika awamu hii kama utarejea Waraka wa Sheikh Ponda.Majuzi kamati kuu ya CCM imempitisha Gwajima.

Leo mitandaoni kuna clips za Gwajima si moja au mbili ni nyingi zikionyesha chuki ya wazi dhidi ya Uislam

Kamati ilichukua uamuzi wa kisiasa bila kuitazama jamii. Hili ni kosa kubwa !

CCM wanashindwa kuwaangalia Waislam machoni, huwezi kumkubali Gwajima bila kukubali ushawishi wake hasa chuki dhidi ya Waislam

Katika jitihada za kujikosha na 'uchafu' wa Gwajima ambao CCM imeukumbatia ikidhani Waislam hawaoni ndio sasa tunaona haya ya michango n.k.

Kamati kuu ilidhani hili ni la Kawe, kadri muda unavyosonga wanabaini kuwa hoja ya Gwajima imegusa jamii yote ya Waislam, na inathibitisha hoja ya Ponda na hivyo waliokuwa na wasi wasi na Ponda sasa hawana shaka tena!

Gwajima kasema na CCM imemuunga mkono na imemthibitisha
Gwajima naye kasaidia sana kuthibitisha kile Ponda alichokisema.
 
Hakuna mapenzi hayo bhana.

Hizo wanazofanya sijui kina Makonda sijui nani sijui Lowassa ni kwa maslahi yao ya kisiasa tu na sio eti kwamba wanataka waislam wapate pa kuabudia.
 
Hata mimi ningekuwepo pale kanisani wala nisingethubutu kuchanga. Maana ni kuabudu miungu wengine.
 
Na huu ndio ukweli, enzi na enzi.

Toka kipindi cha Mwalim Nyerere na mpaka sasa.

Kwa taifa makini na chama makini kinachohitaji ustawi wa jamii yake, amani na upendo kwa wanachi wake basi Gwajima hakupaswa hata kuruhusiwa kuchukua form ndani ya chama hicho.

Ila kwa vile lengo la CCM ni kumuondoa tu madarakani Halima Mdee basi kwa gharama yoyote ile hata kuhatarisha mshikamano wa wananchi wapo tayari kufanya hivyo.
 
Wakati wa Mwalimu hata waliofuata dini ilikuwa ni 'taboo'' kuizungumzia katika mazingira ya kisiasa.
Sasa hivi tunaambiwa watu wasichanganye dini na siasa, lakini wanasiasa ni haki kuchanganya na dini.

Kiti kimoja cha ubunge wa Kawe hakina sababu zozote zile za kuweka amani ya nchi katika mstari.
Hili ni kosa kubwa sana na sijui huko ndani ya CCM hakuna mwenye jicho la kuona na uthubutu wa kukemea

Kinachotokea sasa hivi, Wagombea wote wa CCM bila kujali imani zao, kila wanaposimama mbele ya jamii wanasoma nyuso za wananchi hasa Waislam zikiwa na swali moja '' Haya ya Gwajima mumeyakubali''?

CCM hawana jibu, hawawezi kumkubali Gwajima na kukataa ujumbe wake.
Kauli zimetoka kwenye kinywa cha Gwajima! Zipo mitandaoni zinasomeka, ni chuki tu iliyothibitishwa na CCM

Kibaya zaidi CCM imefungua ''floodgate'' Utakmakamata vipi Sheikh Ponda kwa uchochezi halafu umzawadie Gwajima kwa Ubunge na jamii ikuelewe!!!

Kwa maneno mengine Sheikh Ponda amepata 'natural immunity'' Atasema chochote
Ukimkamata Sheikh Ponda utaulizwa, vipi Ponda enede Ukonga , Gwajima aende Dodoma?
Kuna tatizo kubwa sana sijui kwanini CCM hawalioni!

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Wakati wa ufunguzi wa kanisa huko miaka ya nyuma kijijini Butiama Hayati Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alitangaza rasmi kuwa angependelea kuona pale kijijini Butiama panajengwa Msikiti mkubwa. Kwa maombi yake kwa kiongozi wa Libya hayati Ghaddafy fedha za kujenga msikiti huo ulipatikana na msikiti huo ulijengwa kwa usimamizi wa ofisi ya Rais huyo mstafuu. Leo kwa mheshimiwa Rais Magufuli kuchangisha fedha ya kujenga msikiti pale sio kosa.
Mwache kupotosha vitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…