Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Dkt.John Magufuli amechangisha mchango kwaajili ya ujenzi wa Msikiti wakati aliposhiriki Ibada katika Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Agosti 23, 2020.

ITV Tanzania

Huku mkiendelea 'Kunichukia' GENTAMYCINE nawashaurini sana 'Wanasisa' acheni Kucheza na Imani za Watu na Kuwachokoza kiasi hiki ni hatari.

Huyu mzee Lissu anamchanganya sana. Hizi kick haziwezi kumsaidia chochote.
Screenshot_20200823-105744_Chrome.jpg
 
Rais Ametoa pongezi wa waumini wote na watu wasio waamini wa dini ya kikristo kwa ufadhili wa ujenzi wa kanisa hilo la Roma Chamwino Dodoma, amesema yeye alichangia kidogo kulingana na uwezo wake ila wapo waliochangia zaidi kwa kiashi kikubwa na kidogo lakini wote walishiriki kwa pamoja kulijenga kanisa hilo.

Amesema Parokia ya Chamwino ina upendo mkubwa na ni mahali salama na hapo kweli uwepo wa Mungu upo, amesema kwa kuwa hapo ni makao makuu lazima pazungukwe na watu wanaomtukuza Mungu na sio wa dhehebu moja tu bali wa madhehebu mbalimbali

Ameomba ruhusa kutoka Kwa Askofu wa kanisa hilo wachangie hela wawajengee waislam Msikiti kwa kuwa waislam wana msikiti mdogo , amtoa sabau kuwa wao pia wanahitaji kumtukuza Mungu na hata baadhi ya wasaidizi wake wengine ni waislam. ameomba ruhusa achukue kikapu achangishe fedha za ujenzi wa msikiti na Baba askofu aziwasilishe kwa Shehe wa msikiti huo.

Katika hilo Baba askofu ametoa ruhusa na yeye kuchangia kiasi cha sh. laki mbili. na wengine waliendelea na uchangiaji wa msikiti huo.
Waislamu tusikubali tutasimangwa Sana na wakiristo
 
Kosa sio la rais kosa ni kwamba kanisa limetoa nafasi kuchezewa, wacha pichezewe!

IGP na TUME YA UCHAGUZI,

kuchangisha FEDHA KANISANI za kujengea MSIKITI siyo KAMPENI?

Je, WAISLAMU waliwaomba WAKRISTO msaada wa kujengea MSIKITI?
 
Zamani , marehemu Mzee Moi kila siku ya ibada ndiyo ilikuwa habari kuu kwa jirani zetu. Leo yametukuta.

Nakumbuka Moi alikuwa mtawala wa mkono wa chuma. Hii ya kwetu sijui ni ya mkono shaba. Mungu awasaidie WaTz kuvuka ktk kipindi hiki cha kusifu na kuabudu
Mtukufu moi
 
Sio mwanasiasa na siasa sijui.kila mtu ja imani..kuita wakatoliki waovyo ni upumbavu..utajisikiaje ukiskia uislamu ni dini ya ovyo
Mimi ni mkatoliki niliyebatizwa na kupata kipaimara na askofu. Nasema hivi katoliki ya leo ni ya hovyo hasa hii ya tanzania.
 
Siyo mbaya kwa wenzetu Wakristo kutuchangia, lakini kwa uwelewa wangu finyu nadhani hii haiko sawa. Hawa tunaowaita makafiri watajengaje nyumba yetu ya ibada?

Mh.Rais Magufuli amechangisha fedha za kujenga msikiti huko chamwino Dodoma akiwa katika ibada ya Jumapili leo tarehe 23/8/2020.
 
Back
Top Bottom