Rais Magufuli jitahidi uache uvunjaji wa sheria! Let justice take its natural course!

Rais Magufuli jitahidi uache uvunjaji wa sheria! Let justice take its natural course!

Sasa kosa la yule jamaa liko wapi jamani mbona mwamposa bado yuko kiataa anasubiri kupandishwa daraja kuwa level za akina TB joshua
 
Kuwa mkristo au moslem haikupi right ya kuchana vitabu vya dini ,hata kama haukiamini ,amini kwa Allah au Mungu lakini usikashifu vitu vya wengine
Umesema vema kabisa. Maan kuna wengine, huvuta upande wao na kuona wengine hawana haki. Kama tukio hili lingefanywa kinyume, kungekuwa kimya kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa hiyo kwa kuchana kitabu cha kuruani ni kuonesha chuki kwa kikundi cha jamii flani, lakini kusema Yesu si Mungu (kuna jamii inaamini kuwa Yesu ni Mungu) si kuonesha chuki dhidi ya hiyo jamii?

Sheria ilivyo kukosea tu taratibu za kumtoa kazini huyo jamaa, tayari ni kukiuka taratibu za kisheria na hiyo ni sababu tosha ya kushindwa kesi

Mhe. mwenyewe anajua Serikali itashindwa kesi, maana alisema "aondolewe kazini hata kama atashinda kesi"
Kinoamiguu,
1:Cha kwanza acha unafiki wa kijinga ww siyo muislam,muislamu hawezi kumtetea mtu aliye kidharirisha kitabu ambacho anaamimi ni kitukufu.
2:Kwa hiyo kumbe siku hizi ukiua au ukiiba nje ya kituo chako cha kazi ni halali?unapo onesha kitendo chochote kisicho faa ndani ya jamii haufai kuwa kiongozi au mtumishi.
3:Kitendo alicho fanya huyu jamaa ni inshara tosha ya chuki yake dhidi ya uislam na waislam, kwa mujibu wa sheria ni kosa kuonesha chuki hadharani dhidi ya jamii yeyote haijalishi unakubaliana na maono yake au la.
4: huyo aliye sema yesu sio mungu hana kosa kwa sababu yeye alitoa maoni yake jambo ambalo limeruhusiwa na katiba, ya kwamba unaruhusiwa kuamini chochote kwa imani yako Lakini usingilie au kukiharibu anacho amini mwenzio eti kwa sababu hukubaliani nacho,na ndio maana serikali imeruhusu midaharo mbali mbali kati ya dini tofauti hata hapa jf kuna jukwaa la dini.
5:kingine muajili wako ndio mwenye uwezo wa kukwambia sikuhitaji kwa sababu ndio kakuajili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa hiyo kwa kuchana kitabu cha kuruani ni kuonesha chuki kwa kikundi cha jamii flani, lakini kusema Yesu si Mungu (kuna jamii inaamini kuwa Yesu ni Mungu) si kuonesha chuki dhidi ya hiyo jamii?

Sheria ilivyo kukosea tu taratibu za kumtoa kazini huyo jamaa, tayari ni kukiuka taratibu za kisheria na hiyo ni sababu tosha ya kushindwa kesi

Mhe. mwenyewe anajua Serikali itashindwa kesi, maana alisema "aondolewe kazini hata kama atashinda kesi"

Sent using Jamii Forums mobile app

Kusema Yesu siyo Mungu imo kwenye Qur'an.

Ni mtizamo tofauti wa kitheolojia na ni wa kale sana baina ya Waislamu na Wakiristo,

Mkiristo akisema Yesu ni Mungu haimaanishi kuwa anamkasirisha muislam, na hivyohivyo Muislamu akisema Yesu siyo Mungu anamkasirisha Mkiristo.

Ila ikifikia hatua ya mtu kuichanachana Biblia au Quran na kuikanyagakanyaga sasa hapo unakuwa umevuka mipaka.
 
Hakuna namna ya kumtetea mtumishi yule vinginevyo idhibitishwe pasipo shaka kwamba alirukwa na akili. Na akisharukwa na akili tayari hatoshi kuendelea na kazi vinginevyo pia idhibitishwe pasipo shaka kuwa sasa akili zimemrudia tena kichwani.
 
Wanafanya hayo au yanayofanana na hayo mara kadhaa... na wakristu tunawapotezeaga tu.. umewahi fika kwenye mihadhara yao..?? Yaani hawa watu hata misiba ya kiislamu huwa waziba barabara... hata wakiwa na sherehe huwa wanaweka maturubai kuziba barabara..!! Tunavumiliaga sana...

Wewe umekatazwa kuziba barabara ukiwa na shughuli kwani [emoji23][emoji23][emoji23] wp wamevunja sheria !
Tatizo lenu nyinyi mnakaa mashambani huko nje ya mji sasa unaona ni vitu vya ajabu hapa mjini..
Kwa taarifa yako mambo hayo yapo miaka na miaka kabla hamjaja mjini kutoka huko mashambani kwenu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
View attachment 1354837

Hizo pia ni beer ukinywa inaacha harufu mdomoni kama bia zingine isipokuwa hazina kilevi ndani yake.

Mie sijui sana mambo ya dini na aya zake; hila kama wewe unaishi nje ya nchi tafuta maduka ya wasomali au waarabu ambayo hata sigara awauzi na muuza duka swala tano utakutana na hizo beer katika baadhi ya maduka.

Sio wote wanatumia hata hizo zisizo na vilevi hila wenyewe wanasema sio dhambi, kulewa ndio dhambi. Ndio maana wanauza alcohol free; haya gani za Quran zinasema ivyo sijui my knowledge is limited.
Nimetaja pombe na pombe lazima iwe na kilevi, hizo ni kama grand malt tu usitumie kutetea hoja yako ya kupotosha. Eti kutumia ulevi ruksa
 
Rais kama muajiri mkuu wa Serikali na aliyechana Quran ni muajiriwa wa Serikali na serikali imeweka viwango vya nidhamu na maadili ambavyo vingine vipo nje ya sheria ila ndani ya mamlaka ya ajira, kumfukuza mtu aliyefanya hivi si kosa.

Mahakàmà itaangalia kosa kwa upànde wa kisheria na serikali imeangalia kosa kwa upànde wa maadili na si makosa yote ya kimaadili yanavunja sheria, mengine yanavunja taratibu za kazi na za kiutumishi.

Mfano mtu kaenda kazini kalewa, hilo ni kosa la kimaadili ambalo sheria haiwezi kumkuta na kosa.

Rais hajavunja sheria yeyote ila katekeleza wajibu kama muajiri mkuu na msimamzi wa maadili wa watumishi wote wa umma
kazi yake na kosa lake vinahusiana VIP, wangeachiwa wale mashehe waliobambikiziwa kesi kama anawajali,kutafuta sifa kupitia mwendawazimu aliyewehuka in utoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana kweli ametenda kosa kuchana Qurani, amewaudhi wengine, Lakini

1. Kuna taratibu tumejiwekea za kushughulka na watu kama hao wanaoamsha hasira za wengine! Uliapa kulinda katiba na sheria zitokanazo na katiba hiyo. Kunatartibu! Wewe huna mamlaka ya kisheria kumwajibisha. Mihemko ya nini? Niwie radhi kuwa this is cheap popularity and to win the Islamic community!

2. Umeshaidharau mahakama kwa kusema ashinde asishinde nimeshamfukuza kazi! Matamshi kama hayo ni ya kidictator katika nchi ambayo ni lawlessness. Unajipa ukuu wa kuwa juu ya mahakama na sheria maana unaapa kutoisikiliza mahakama in case anakwenda mahakamani na kushinda!

3. Hili siyo tukio la kwanza Nakuwekea kesi ya Dibagula uone how such issues are handled in a law abiding regime!
Mzee kasome hukumu ya court of appeal baina ya urouch wa chama cha walim tanzania dhidi ya katibu mkuu utumishi wa uma.

Rais ndo mwenye mamraka yakufukuza mtumishi wa uma kazi.

Kwahiyo Rais alisema hivyo akimaanisha sheria ndo imempa nguvu.
 
Wewe umekatazwa kuziba barabara ukiwa na shughuli kwani [emoji23][emoji23][emoji23] wp wamevunja sheria !
Tatizo lenu nyinyi mnakaa mashambani huko nje ya mji sasa unaona ni vitu vya ajabu hapa mjini..
Kwa taarifa yako mambo hayo yapo miaka na miaka kabla hamjaja mjini kutoka huko mashambani kwenu

Sent from my iPhone using JamiiForums
What is your point then..!!! Mashambani ndo wapi? Asumptions zako za mashambani basi hazina hoja ya kwanini uzibe barabara kisa eti unaishi mjini..!!!
 
What is your point then..!!! Mashambani ndo wapi? Asumptions zako za mashambani basi hazina hoja ya kwanini uzibe barabara kisa eti unaishi mjini..!!!

Nijambo la kawaida lipo miaka na miaka pengine kabla wewe ujazaliwa ..
Panapokua na jambo la kukusanya watu either msiba au harusi ni kitu kinachoruhusiwa Sasa kama wewe unashangaa ndio maana nakwambia labda umetoka mashambani

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Rais kama muajiri mkuu wa Serikali na aliyechana Quran ni muajiriwa wa Serikali na serikali imeweka viwango vya nidhamu na maadili ambavyo vingine vipo nje ya sheria ila ndani ya mamlaka ya ajira, kumfukuza mtu aliyefanya hivi si kosa.

Mahakàmà itaangalia kosa kwa upànde wa kisheria na serikali imeangalia kosa kwa upànde wa maadili na si makosa yote ya kimaadili yanavunja sheria, mengine yanavunja taratibu za kazi na za kiutumishi.

Mfano mtu kaenda kazini kalewa, hilo ni kosa la kimaadili ambalo sheria haiwezi kumkuta na kosa.

Rais hajavunja sheria yeyote ila katekeleza wajibu kama muajiri mkuu na msimamzi wa maadili wa watumishi wote wa umma
Halafu licha ya kuwa ni rais ni muajiri mkuu kuna suala la maadili ya mtu binafsi.

Ukilea mpumbavu mmoja akafanya upumbavu hadharani kesho ataibuka mpumbavu mwingine atafanya upumbavu mwingine.

Yule dogo imekula kwake mazima.
 
..kwanza, nalaani kitendo alichofanya huyo kijana cha kudhalilisha QURAN.

..Lakini hiki ulichoandika ni UONGO.

..Mkapa aliwahi kufukuza watumishi kimakosa na serikali ilishindwa kesi mahakamani.

..Raisi hayuko juu ya sheria kama ulivyodanganya hapo juu.
Rais ni mwajiri mkuu, anaweza kukufuta kazi au kupendekeza upandishwe cheo muda wowote ule.

Kiongozi mkuu wa serikali ni rais, huyo pimbi wa huko Kilosa ni muajiriwa wa serikali.
 
Rais kwa mamlaka yake ni muajiri mkuu wa Serikali hivyo ana mamlaka yote ya kumuajiri na kumfukuza yeyote ndani ya JMT kwa sababu yoyote bila kumtaarifu yoyote juu ya ukomo wako wa ajira.

Hata kama ni ngumu kuwatoa baadhi ya watumishi kama CAG na majaji lakini katiba imesema hapana kama Rais hatoweza kuwaondoa hao dhanà nzima ya muajiri mkuu inapotea ndio maana kawekewa utaratibu wa kumtoa na anaweza kumtoa.

Kwa hiyo Rais anaposema Fulani atoke hakihitajiki kingine zaidi ya kutangazwa nafasi ipo wazi na mtu anajazwa
Ficha ujinga wako wewe, muajiri mkuu ndio nini? Watu wote wameajiriwa na taratibu za ajira zipo wazi.

Sio mtu akiamka tu anafukuza mtu kazi. Hii tabia hata wakuu wa wilaya na mikoa walianza kufanya kipindi fulani.

Acha sheria ifuate mkondo wake. Taratibu za ajira zipo wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulia mzee. Mbona unashindwa handle mazungumzi unajaaa jazba, unadhidi ku prove na kuonyesha, busara ili hama kambi yako.

Hakuna sehem imesemwa hapo juu na mimi kupongeza wala kutetea tukio.

Nimeongelea ufinyu wa hoja zako na Double standard.

Unashida kisaikolojia hamtaki kosolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja zipi ulizo ongea zaidi ya pumba hapo siku zote mtu anaye endekeza chuki ni mpumbavu tu hana akili na wewe unaye tetea upumbavu na wewe pia ni mpumbavu,samahani kwa kukuita mpumbavu ila sioni jina lingine zaidi ya hilo kwa mtu anaye palilia chuki kama wewe.
 
Back
Top Bottom