Nikiri kwamba mimi ni muislamu kwa kuzaliwa.
Ukiwa mpenda haki lazima uwe na uwezo wa kusimama katikati na kusema kweli.
Iliripotiwa kwamba kuna mtumishi mmoja kachana MASAHAF Huko Morogoro.
Hatua zilizochukuliwa dhidi yake ni kama ameua yaani mwamposa aliyekusanya watu na kusababisha wakanyagane akaonekana katenda jambo dogo kweli kuliko la kuchana MASAHAF.
Kama tunakumbuka vizuri hapa jukwaani kuna mtu aliitwa DIBAGULA. Huyu bwana alitokea huko huko Morogoro. yeye alisema YESU SIO MUNGU. Hukumu ya case yake inajulikana ukweli ni kwamba alishinda?
Leo kuna mzalendo mmoja huko Kigamboni amemfukuza huyu bwana kazi. Ni amma hajui sheria, kanuni na taratibu za utumishi au ni mihemko tu ya kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Nitaeleza:
1) Kwanza jamaa hajapewa nafasi ya kusikilizwa. Hapo anashinda mchana kweupe, hakuna mashtaka yoyote ya kiutumishi yaliyofunguliwa dhidi yake. Mkuu wa nchi kaingia chaka.
2) Imani yake haiamini kwenye utukufu wa qurani, yeye mkristo, unaposema kitabu kitakatifu sio kwake
3) Kosa alilofanya halimuathiri mwajiri wake kwa namna yeyote ile, amelifanya nje ya kazi zake.
Tujifunze kuheshimu Sheria
1. Tena ikithibitika alikuwa yuko "mbwiii" na kilevi, hata hahitaji kuweka hata wakili, anaachiliwa asubuhi tu na hakuna cha "upelelezi haujakamilika" wala nini....
2. Halafu mimi nashangaa sana watu na serikali yenyewe inavyolikuza jambo hili unnecessarily kabisa. Kwanza hebu tujiulize tangu lini "kitabu chochote cha makaratasi tu yanayoweza kuchanika, kuungua moto ama kuchanwa na mlevi barabarani, iwe Biblia ama Korani kiwe kitakatifu??"
Makaratasi yapo kwa ajili ya kutunza kumbukumbu tu za maandishi lakini hatuwezi kuziita "takatifu". Hayo maandishi yakisomwa na kukaa ndani ya moyo ama nafsi ya mtu yakatenda kazi kusudiwa, ndipo yanakuwa na maana. Ukishamaliza kusoma, waweza hata kutupa chooni kitabu hicho kwa sababu utakuwa umepakua na ku - install ndani ya moyo kila kitu...
Kama Yesu Kristo atarudi leo kuchukua watu wake, hatauliza ama kuwataka watu waoneshe " the so called - Biblia ama Korani takatifu" ndiyo iwe tiketi yako ya kuingia mbinguni. HAKUNA!!
3. Mimi ni Mkristo 100%. Lakini akitokea mtu ambaye anapesa zake zimekosa kazi ya kufanya na akaamua kwenda kununua Biblia zote madukani na kuzipeleka dampo kule Pugu na kuzitupa ama kuzichoma moto, nakuhakikishia kabisa SITAJALI LOLOTE!!...Why?
4. Kwa sababu Mungu yeye ndiye Mtakatifu na kamwe haishi kwenye makaratasi yanayoitwa "Biblia" au "Korani". Mungu anaishi ndani ya Roho ama Mioyo na Nafsi za WATU haishi kwenye makaratasi yanayochanika ama kuchomeka na moto ama kulowa na maji....!!
5. Ukichana makaratasi hayo yanayoitwa leo " matakatifu", haiwezi kuwa umemchoma au kumchanachana Mungu. Mungu Mtakatifu hachanwi wala haunguzwi na moto kana kwamba yeye amekuwa ni karatasi!!
6. Mtu anayeweza kuamushiwa hii inayoitwa "hisia ama hasira zake" na eti kutaka naye kulipiza kisasi eti kwa sababu makaratasi yaliyopachikwa na binadamu jina la "kitabu kitakatifu" yanechanwa au kuchomwa moto na mlevi fulani, hakika huyo mtu hapana jina jema linalomfaa kuitwa zaidi kuwa a useless chicken head, mtu asiyemjua Mungu Mtakatifu wala namna anavyotenda kazi katika maisha ya watu...!!
7. Umesema kweli, kuwa, kile ambacho ni kitakatifu kwako siyo lazima kiwe kitakatifu kwangu....