Rais kama muajiri mkuu wa Serikali na aliyechana Quran ni muajiriwa wa Serikali na serikali imeweka viwango vya nidhamu na maadili ambavyo vingine vipo nje ya sheria ila ndani ya mamlaka ya ajira, kumfukuza mtu aliyefanya hivi si kosa.
Mahakàmà itaangalia kosa kwa upànde wa kisheria na serikali imeangalia kosa kwa upànde wa maadili na si makosa yote ya kimaadili yanavunja sheria, mengine yanavunja taratibu za kazi na za kiutumishi.
Mfano mtu kaenda kazini kalewa, hilo ni kosa la kimaadili ambalo sheria haiwezi kumkuta na kosa.
Rais hajavunja sheria yeyote ila katekeleza wajibu kama muajiri mkuu na msimamzi wa maadili wa watumishi wote wa umma