Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 11,936
- 15,196
Nikiri kwamba mimi ni muislamu kwa kuzaliwa.
Ukiwa mpenda haki lazima uwe na uwezo wa kusimama katikati na kusema kweli.
Iliripotiwa kwamba kuna mtumishi mmoja kachana MASAHAF Huko Morogoro.
Hatua zilizochukuliwa dhidi yake ni kama ameua yaani mwamposa aliyekusanya watu na kusababisha wakanyagane akaonekana katenda jambo dogo kweli kuliko la kuchana MASAHAF.
Kama tunakumbuka vizuri hapa jukwaani kuna mtu aliitwa DIBAGULA. Huyu bwana alitokea huko huko Morogoro. yeye alisema YESU SIO MUNGU. Hukumu ya case yake inajulikana ukweli ni kwamba alishinda?
Leo kuna mzalendo mmoja huko Kigamboni amemfukuza huyu bwana kazi. Ni amma hajui sheria, kanuni na taratibu za utumishi au ni mihemko tu ya kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Nitaeleza:
1) Kwanza jamaa hajapewa nafasi ya kusikilizwa. Hapo anashinda mchana kweupe, hakuna mashtaka yoyote ya kiutumishi yaliyofunguliwa dhidi yake. Mkuu wa nchi kaingia chaka.
2) Imani yake haiamini kwenye utukufu wa qurani, yeye mkristo, unaposema kitabu kitakatifu sio kwake
3) Kosa alilofanya halimuathiri mwajiri wake kwa namna yeyote ile, amelifanya nje ya kazi zake.
Tujifunze kuheshimu Sheria