Rais Magufuli: Kazi ya Serikali sio kulisha watu, sitatoa chakula cha bure kwa wataokumbwa na njaa

Rais Magufuli: Kazi ya Serikali sio kulisha watu, sitatoa chakula cha bure kwa wataokumbwa na njaa

Lakini haya ni mambo ya ajabu.

Ni wapi serikali ilipowahi kuwagawia wananchi wake chakula wakati palikuwepo na mvua za kutosha kwa wananchi kujilisha wenyewe!

Kuna mfano wowote mtu yeyote anayeweza kuuweka hapa kuthibitisha kwamba serikali iliwahi kuwagawia wananchi wake waliokuwa wanakufa kwa njaa kwa uzembe wao tu kwa kutolima chakula wakati hali ya hewa ilipokuwa inawaruhusu kufanya hivyo?

Mbona anakomalia mambo ambayo hayajawahi kutokea hata mara moja!

Watu wanakosa chakula wakati wa majanga, na hapo ni wajibu wa serikali kote duniani kusaidia raia zake majanga yanapotokea.
 
Roho ya kimaskini na ya kichawi, wakati huo huo anachota trillions za walipa kodi bila idhini ya Bunge kufanyia miradi ya kipuuzi kijijini chato, kununua wanasiasa malaya etc. Huyo anayejiita mwendawazimu kwa akili yake pesa za walipa kodi ni pesa zake!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewaagiza Watanzania kutumia mvua zinazonyesha kipindi hiki kulima mazao ya chakula na biashara ili kuepukana na janga la njaa, na endapo eneo lolote litakumbwa na njaa serikali haitokuwa tayari kupeleka chakula.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa Wilayani Bahi mkoani Dodoma wakati akielekea jijini humo akitokea Tabora, amesema kuwa maeneo ambayo hayatafanya kazi kwa uzembe wao hatovumilia viongozi wa maeneo husika.

“Sitatoa chakula kwenye Wilaya yoyote, hakuna chakula cha bure kama mlivyozoea huko nyuma, usipofanya kazi usile na usipokula kufa, lazima tuambiane ukweli, Watu wafanye kazi, walime, na asiyefanya kazi asile”, amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa, “Wilaya itakayopata njaa DC ataondoka na Viongozi wengine wanaostahili kuhamasisha Wananchi kufanya kazi wataondoka, tunataka pesa tunayopata ifanye kazi nyingine, tunatoa Elimu bure, tunajenga SGR ndio kazi za Serikali, sio kukulisha".
 
Ni kweli. Siyo mara zote njaa inaletwa na watu kuzembea kufanya kazi. Hata maeneo yenye wachapa kazi wazuri sana njaa inaweza kutokea kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao. Hapo ndipo inabidi serikali ifanye kazi yake (tukumbuke moja ya kazi za serikali ni kutoa huduma wakati wa vipindi kama hivi)
Wakati mwingine Watanzania ni wavivu sana wanalizika haraka, mfano nimelima mashamba yangu huko maeneo ya manyara, sasahivi nimetangaza palizi kwa eka sh elfu 30000)lakini akuna anayejitokeza kisa wanachakula ndani, lakini Wakati wa njaa hiyo eka wanapalilia kwa elfu 15000) Watanzania kwa ujumla ni wavivu sana.
 
Sijawahi juta kumkataa Magufuli
Lakini unakula vyakula vya wanaolima.. tena labda kwa kukopa.. nenda kalime.. tabu upinzani koko kila kitu mnapinga.. ukweli ndio huyo.. penda sana Rais wetu woteeee bila kujali itikadi.. yani Rais wako pia anajua kutupa vya uso.. imekuuma.. kalime ule.. ukikosa sehemu nifate hapa kijijini tulime tule.. Organic Food ya kiwango cha juuu
 
Raisi wangu kwa uchaguzi gani unaostahili kuitwa uchaguzi? Tusichoshane bure.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewaagiza Watanzania kutumia mvua zinazonyesha kipindi hiki kulima mazao ya chakula na biashara ili kuepukana na janga la njaa, na endapo eneo lolote litakumbwa na njaa serikali haitokuwa tayari kupeleka chakula.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa Wilayani Bahi mkoani Dodoma wakati akielekea jijini humo akitokea Tabora, amesema kuwa maeneo ambayo hayatafanya kazi kwa uzembe wao hatovumilia viongozi wa maeneo husika.

“Sitatoa chakula kwenye Wilaya yoyote, hakuna chakula cha bure kama mlivyozoea huko nyuma, usipofanya kazi usile na usipokula kufa, lazima tuambiane ukweli, Watu wafanye kazi, walime, na asiyefanya kazi asile”, amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa, “Wilaya itakayopata njaa DC ataondoka na Viongozi wengine wanaostahili kuhamasisha Wananchi kufanya kazi wataondoka, tunataka pesa tunayopata ifanye kazi nyingine, tunatoa Elimu bure, tunajenga SGR ndio kazi za Serikali, sio kukulisha".
Yeye anatoa chakula kama nani ? Chakula kinatolewa na serikali sio yeye .
 
Wakati mwingine Watanzania ni wavivu sana wanalizika haraka, mfano nimelima mashamba yangu huko maeneo ya manyara, sasahivi nimetangaza palizi kwa eka sh elfu 30000)lakini akuna anayejitokeza kisa wanachakula ndani, lakini Wakati wa njaa hiyo eka wanapalilia kwa elfu 15000) Watanzania kwa ujumla ni wavivu sana.
Kama unadhani hiyo 30,000 ni worth Sana peleka ndugu zako watumikishe afu walipe hiyo pesa watakushukuru sana
 
Kama unadhani hiyo 30,000 ni worth Sana peleka ndugu zako watumikishe afu walipe hiyo pesa watakushukuru sana
Ndio maana Magufuli kawaambia wasipotumia furusa wakalima na kujitafutia chakula,wasije kulia njaa,me sina shida tajiri anuniwi mkuu.
 
Sawa kamua baba serikali kazi ni kuwajengea watu miundo mbinu afya na usalama wa mali zao sio kuwaletea chakula wavivu!
Kuna food banks ulaya,jk alitoa ruzuku kwenye mbolea tukawa tunanunua mfuko wa 50kg sh 20000,yeye kafuta ruzuku,tunanunua 70000,kuna hifadhi ya chakula ya serikali,kinahifadhiwa kwa malengo gani?..tz inauza chakula nje,hulima serikali mpaka awasimange watu!!?
 
Inawezekana hiki kilicho kwenye hifadhi ndo kinatolewa msaada kule nchumbiji na kingine kupelekwa kule jimbabwe, sisi watanzania wanyonge tunajibeba.
 
Hayo maneno yana ukweli ndani yake lazima tufanye kazi, ila akumbuke zinaweza nyesha mvua zikapitiliza mazao yakaharaibika, hapo asiache kutupa msaada (nimekumbuka Kagera)
Sawa kabisa,
Kanda ya ziwa mvua kuna sehemu, zimeondoka na vitalu vya mipunga, na iliyopandikizwa ikafukiwa na mchanga, na mvua ukipishana nazo ndiyo basi,

Napo itasemwa hawa watu wavivu ndiyo maana hawajavuna?

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Sikia wewe mbumbumbu! Magufuli yuko sahihi! Nenda kalime usikae tu mjini unapiga domo ukitegemea njaa ikitokea utapata chakula cha bure
Na yeye chakula anachokula anakilipia? Au kinatokana na lile fungu lisilo hojiwa pale Bungeni? By the way, tangu alipoingia madarakani, ni lini aliwahi kuwapa Watanzania hicho chakula chake cha bure?

Maana nyinyi Mataga hamjawahi kuhoji!! Kazi yenu ni kukatika tu viuno kwa kila akisemacho mwenyekiti wenu.
 
Kama I
Jamani huko mliko, hasa wakulima, kweli Rais Magufuli anaweza kumshauri au kumwelekeza Mkulima yeyote nchini alime nini, wakati gani au atumie mbinu gani? Wakulima wetu wanajua nini cha kufanya, wakati gani ili wapate mavuno mengi kwa chakula cha familia zao na ziada kwa ajili ya kuuza wapate pesa kwa mahitaji mengine muhimu kama kusomesha, kununua pembejeo, kuboresha nyumba, kulipa kodi na mahitaji mengine ya kila siku ya nyumbani kama sukari, mafuta, chumvi vyama, Michele nk.

Awamu ya Tano haijawahi kuwa na mpango wowote wa Kilimo kama Awamu zilizopita kulikuwa na Ukulima wa Kisasa, Kilimo Bora, Kilimo cha Kufa na Kupona, Siasa ni Kilimo (Nyerere), Kilimo cha Kupona (Mwinyi), Kilimo Kwanza (Kikwete) nk. Toka Uhuru, wakulima wetu hawajawahi kuomba chakula chao toka kwa Rais yeyote, hata na yeye, wala Serikali ya Awamu yoyote kwa sababu wanajua namna ya kupata na kuhifadhi chakula chao hata katika mazingira magumu kama ukame, mafuriko, wadudu waharibifu nk.

Wanaoweza kukabiliwa na uhaba wa chakula ni wale wasiyo Wakulima ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wake, wafanyabiashara na wengine ambao chakula chao lazima wanunue, wengi wao wakiwa wanaishi mijini.
 
Nilimchagua kwa sababu alipiga push up jukwaani

IMG-20210131-WA0002.jpg
 
Back
Top Bottom