Rais Magufuli kwa miaka yote mitano sukari tu imemshinda

Rais Magufuli kwa miaka yote mitano sukari tu imemshinda

na tatizo linapokuja kipindi hiki cha mfungo tu kila mara tunahisi kama ni mpango maalum kwa ajili ya kutatiza swaumu za wanaofunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati anaingia madarakani, sukari ilikuwa imetulia kwenye 1,800 - 2,000 kwa kilo. Tena ilitulia haswaa, wala haikuwa ishu. Sasa Magu na kiherehere chake, sukari iikapanda hadi 6,000 kwa kilo. Baadae ika-settle 2,600 kwa kilo. Hapo akasikika akidanganya kuwa alikuta sukari inauzwa 5,000!
Hii naikumbuka vyema baada ya hali kutulia wapambe wake wajinga wajinga ni kweli walisema huo ujinga. P
 
Najiuliza ni nini tatizo?

Rais Magufuli alipoingia ikulu mgogoro namba moja aliouanzisha ni sukari. Sukari ghafla ikapanda bei, ikapotea mitaani.

Ilifikia hatua akatoa vitisho kuwa ataliruhusu jeshi likamate sukari iliyofichwa liigawe bure. Nakumbuka hii kauli wapiga zumari waliishangilia sana ila ilikopotelea anakujua mwenyewe.

Kwa miaka yote mitano ya utawala wake sukari haijawahi kupata suluhu na sasa imepotea tena sokoni. Nini tatizo? Mbona huu mgogoro kama una kitu nyuma ya pazia?

Sasa kama kwa miaka yote mitano sukari tu kashindwa kuipatia ufumbuzi, sijagusia sarakasi zake za makinikia? Inakuwaje hili la Corona?
Sukari ilimkaribisha Hivo imekuja kumuaga tena.Next year tutakuwa na tz mpya
 
Leo nimezunguka sehemu kibao kutafuta sukari hakuna. Watawala hawajui demand and supply? Hata kama Serikali inatakiwa kuingilia ila sio kurukia.
This look like failed state, serikali inaongozwa na mabumunda?
Hawazalishi ila wanalazimisha bei elekezi.
Sitaki kuonge sana but we are doomed.

Lawama zote kwa JK na Mkapa. Na pia TISS tutawalaumu mpaka kufa.
 
Bila kupepesa macho, kwenye sukari kuna udhaifu mkubwa Sana, karibu serikali zote hasa majira ya mwezi mtukufu, kuna nini?

Je mawaziri huwa wanaweka mikono Yao hapo? Hili la sukari ukweli ni janga haswa, ukweli usemwe, Serikali imechemka
Suala la sukari ni tatizo la kimfumo tu, Unataka kusema kwamba Bodi ya Sukari hawajui mwarobaini wa tatizo la sukari . ?
 
Unazungumzia miaka mitano wakati ameshindwa kuimudu ndoa yake yenye miaka 40!!!
Achana na ndoa, hivi unajua kwa miaka zaidi ya ishirini iliyopita hakuna kiwanda kipya cha sukari Tanzania . ?

Ni vile vile tangu enzi ya mwalimu, waulize sababu utawasikia wanavyo kukuruka
 
na tatizo linapokuja kipindi hiki cha mfungo tu kila mara tunahisi kama ni mpango maalum kwa ajili ya kutatiza swaumu za wanaofunga

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulivyompumbavu unadhani sukari imeadimika kwajili ya kuwakomoa walioko kwenye mfungo.

Hili tatizo limekuwepo toka awamu ya tano imeingia madarakani kila kitu kimekuwa cha kubahatisha bahatisha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda Mlimani City duka la Game bei tshs 2950 kwa kilo
Mkuu, hapa Mimi ni mshabiki wa JPM Sana!! Ila katika hili, sipepesi macho mkuu, hapana, mbona sukari ni tatizo na hakuna maelezo? Ina maana watu wote wa Dar wawe wanaenda kununua sukar ShopRite mlimani siyo?
 
Back
Top Bottom