Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema mshahara wake ambao yeye ameukuta na ambao analipwa ni Milioni 9 na laki 5. Rais Dkt.Magufuli amelazimika kuyasema hayo wakati wa uchambuzi wa magazeti katika kipindi cha Clouds360. Akizungumza na mtangazaji wa kipindi hicho Hudson Kamoga ameahidi akirudi kutoka likizo yupo tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake.
Baada ya kusema mshahara wa juu uwe angalau Milioni 15 kumbe yeye hata Milioni 10 hajafikisha
Na pumba juu MKUUHiyo ni wivu class A mkuu
Pumba[emoji107]..millions 9.5 za nini wakati serikali inamgharimia kila kitu hata kuanzia chakula, makazi, hata luku halipii.
..zaidi ya hiyo millioni 9.5 kuna posho anapokea. Sasa Kama ni mkweli aeleze anapokea kiasi gani.
..pia akistaafu anajengewa nyumba na kuendelea kutunzwa yeye na familia yake.
..Huu ndiyo tunaita UNYONYAJI.
Mmmh bado siamini
Hivi zito na lisu huwa swaelewa na wao wanalialia kimoyoyo hakuna posho za kijinga wameanza kujiuzuru,hawa jamaa hawataki kusema ukweli kwa watanzania kuwa jaman maisha yamebadilika siku hiz fedha hakuna wanaanza kumshambulia rais et taja mshahara.kuna baadhi ya wanasiasa nishaachaga kuwasikila kwasababu niwanafiki ni baraa wakibanwa wanaongea vingne kufikisha ujumbe nawaomba watulie sindano ziingie vizuri.
Wewe ni kubwa jinga hujitambwi umebaki kuropoka tu.anakula bure, analindwa bure, nashauri apunguziwe na kulipwa laki nne kwa mwezi, vinginevyo naye mnafiki tu
Hivi heshima ya rais ni kucheza na media muda wote? Magufuli hajui kuwa kuna mambo ya kujibu yeye kama rais na mambo ya kujibiwa na vyombo husika? Kwa heshima ya ofisi ya rais wa nchi yoyote kufahamu lipi lijibiwe na wakkati gani na nani nijambo la muhimu sana. Vinginevyo ni udhaifu mkubwa sana kwa taasisi husika.Leo wakati nasikiliza Kunani Tanzania Magazetini Clouds TV kipindi, Gazeti la Nipashe nileandika taarifa kuhusu Zitto na Tundu Lissu kumtaka Raisi Magufuli kutaja mshahara wake ili wajue kiasi cha kodi anacholipa!
Haikuchukua muda, taarifa ya Breaking News ikasomwa na Mtangazaji Baby kuwa, Mh. Rais kapiga simu na kuwatajia kiwango cha mshahara wake na kuwa atakapotoka rikizo fupi aliyonayo atawaletea risiti ya mshahara wake! Mh. Rais ametaja kuwa Mshahara wake ni Milioni tisa na Laki tano (Tsh. 9,500,000/-)
Chanzo: Clouds TV, Kunani magazetini!
NyumbuWajinga wa lumumba eti hiyo ni uzalendo si apokee tu kama ya mwalimu laki 5 tujue ni mzalendo? Si anakula bure malazi bure!!! Na miposho kibao? Mlaji ni mlaji sio lazima ataje mshahara wake wajinga ndo waliwao
pengine huo unaweza kuwa ndo mshahara mdogo kuliko wa rais yeyote yule duniani..................sasa sijui kama kuna ukweli au vipi ila ngoja movie iendeleee iko siku tutafika tuRais Dkt. John Pombe Magufuli ametaja mshahara wake kuwa ni Tsh mil 9.5, huku akiahidi atatoa Salary slip zake punde akitoka mapumzikoni Chato.
Hiyo imetokea wakati wa kipindi cha magazeti leo tarehe 01/04/2016 ambapo watangazaji walisoma habari iliyoandikwa na gazeti la nipashe kuwa Zitto na Lissu waomba ataje Mshahara wake na ukatwe kodi.
Wakiwa katika mjadala huo, walipokea taarifa kuwa Rais kawasikia na katuma taarifa ofisi za Clouds kujuza mshahara wake kuwa ni mil 9.5 na atatoa stakabadhi zake akirudi Dar.
Huo ndio mshahara alioukuta na hata Rais Kikwete alikuwa akilipwa kiasi hicho pia.
Chanzo: Clouds 360 Asubuhi hii.
9500000 per year 114,000,000
9500000 per 5 years 570,000,000
9500000 per 10 years 1,140,000,000
HAPA KAZI TU.
Upungue kwa sasa hivi. Uchumi ukiimarika ataongezewa. Hana matumizi nazo zaidi ya kupeleka kwa wahitaji. Elimu ni bure, kula, kulala na hata wardrobe yake na ya mama yetu vianagharamiwa na kodi zetu. Wote tuwe wazalendo. Hii habari ni ya kweli lakini?Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametaja mshahara wake kuwa ni Tsh mil 9.5, huku akiahidi atatoa Salary slip zake punde akitoka mapumzikoni Chato.
Hiyo imetokea wakati wa kipindi cha magazeti leo tarehe 01/04/2016 ambapo watangazaji walisoma habari iliyoandikwa na gazeti la nipashe kuwa Zitto na Lissu waomba ataje Mshahara wake na ukatwe kodi.
Wakiwa katika mjadala huo, walipokea taarifa kuwa Rais kawasikia na katuma taarifa ofisi za Clouds kujuza mshahara wake kuwa ni mil 9.5 na atatoa stakabadhi zake akirudi Dar.
Huo ndio mshahara alioukuta na hata Rais Kikwete alikuwa akilipwa kiasi hicho pia.
Chanzo: Clouds 360 Asubuhi hii.
Nilivyoelewa kasema huo ndo mshahara aliokuta ina maana hata msoga alikuwa anapokea hiyo 9.5 leo kweli siku ya wajinga hata kama habari haihusiani na siku ya wajingaYa kweli haya?! yule jamaa yetu wa msoga yeye alikuwa anakunja 192m us dollar kwa mwaka sawa 36 m tsh kwa mwezi!. basi magufuli ni mzalendo