Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Mkuu, hapana jamaa ana logic, mishahara matumizi yake ni kukidhi gharama za maisha ya kila siku ambazo tayari zinabebwa na bajeti ya kila mwaka. Katiba pia imemhakikishia kuishi hata baada ya kuongoza, sasa mshahara wa nini???
Ili ujue uzito wa kazi yake na anastahili zaidi ya huo mshahara, watu wenye njaa wanamlalamikia wao kuwa wana njaa, wakulima wanamlalamikia yeye kuhusu mazao, vijana wanamlalamikia yeye kuhusu ajira, wagonjwa kulala chini wanamlalamikia yeye, pesa kupotea ktk mzunguko watu wanamlalamikia yeye, nk.
Unajua kwa nini hawa watu wote wanamlalamikia yeye? Ana majukumu mazito zaidi ya udhaniavyo.
 
Unajua mkuu, kwanza kufikiri ina-cost energy, pili wengi wetu humu akili zimeamia kwenye vidole, hivyo wazia zitoke vidoleni ziende kwenye cpu kichwani inakuwa kazi kweli...πŸ˜‰
 
mkuu binafsi sipingani na jitihada za rais, namkubali sana magufuli, linapo kuja swala la mshahara kwa mtu kama rais sioni ni wa nini,kwasababu tunapo mpa kila hitaji lake mpaka kiwembe au wa kumkata kucha kabisa tukamlipa ili kumuwezesha afanye shughuli zake kwa wepesi, ukiongeza malipo ya mshahara kwa kutaja kiasi chochote sioni kama nirealistic.
 
Baada ya watu kutaka kujua yeye anapokea sh.ngapi awapigia simu clouds tv na kujibu swali hilo kuwa yeye anapokea sh.9.500.000 kwa mwezi na akimaliza likizo atatoa ufafanuzi wote

Source clouds Tv
Fools Day ----sikukuu ya wajinga 1/4/2016 mradi taarifa itolewe kabla ya saa nne asubuhi.
 

Hawawezi kulitungia sheria; ni mpaka wabadili Katiba. Na mchakato wa kubadili Katiba sidhani kama utakuwa rahisi kivile kwa jambo moja isipokuwa kama wanataka kufanya kwa ujumla
 
Tuzipage na akili zetu nafasi za kufikiri jamani.
 
ndugu ukumbuke huyu mtu tunamuwezesha kwa kila kitu ili apate urahisi wa kazi zake hata za binafsi, ukitaja kiasi hicho kuwa ndo mshahara wake hautakuwa realistic.
 
Duuh mbona mdogo sana!!!!
wengine mbona tunaambiwa wanalipwa mil 36.
ina maana ni mabosi wa raisi?
 
ndugu ukumbuke huyu mtu tunamuwezesha kwa kila kitu ili apate urahisi wa kazi zake hata za binafsi, ukitaja kiasi hicho kuwa ndo mshahara wake hautakuwa realistic.
Wewe unaweza fanya kazi bila kulipwa? Sio yeye tu anayewezeshwa, hata majeneral wa jeshi wamewezeshwa.
Kwa hiyo akitaka jenga nyumba ya mama yake na nyumba ya baba yake unamwezeshaje?
 
Sio mbaya maana amepunguza maneno maneno ya Akina Kabwela na Tundu Maneno. Hivi kwenye ule mpango ya kupunguza posho kwa wabunge Tundu Maneno alikuwa upande gani!!!!!
 
Wewe unaweza fanya kazi bila kulipwa? Sio yeye tu anayewezeshwa, hata majeneral wa jeshi wamewezeshwa.
Kwa hiyo akitaka jenga nyumba ya mama yake na nyumba ya baba yake unamwezeshaje?
Kuna watu huwa wanaamua kuwa upande wa ubishi bila sababu yoyote. Hata mtoto mdogo anayepewa huduma zote bado anahitaji uhuru wa kuwa na nguvu ya fedha. Kwangu mimi rais wa nchi lkama Tanzania hata kama atalipwa milioni 30 kwa mwezi ni reasonable kabisa.
 
Hawawezi kulitungia sheria; ni mpaka wabadili Katiba. Na mchakato wa kubadili Katiba sidhani kama utakuwa rahisi kivile kwa jambo moja isipokuwa kama wanataka kufanya kwa ujumla

..Raisi ni ccm.

..spika ccm.

..majority ya wabunge ni ccm.

..sasa Nani atawazuia hata kama wakiamua kubadili katiba?
 
Aya sawa!!!
Raisi analipwa kidogo kuliko wakurugenzi wa mashirika ya umma sawaa!!
Ila katika kubana matumizi kama vipi adake milioni mbili tuπŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰

Happy fools day
Kwa kazi yote anayoifanya kama kiongozi wa nchi,alipwe 2m au sasa mnataka kumfanya afisa mtendaji wa kijiji na sio raisi tena,tuanze basi na pensheni ya ''aliye jiuzuru''
 
Wewe unaweza fanya kazi bila kulipwa? Sio yeye tu anayewezeshwa, hata majeneral wa jeshi wamewezeshwa.
Kwa hiyo akitaka jenga nyumba ya mama yake na nyumba ya baba yake unamwezeshaje?
ndugu yangu ingawa mimi siyo mkatoliki niliwahi kusikia kitu kama hiki, naomba uchukulie kama mfano, mapadri wa kikatoliki hawalipwi mishahara ila husaidia sana familia zao!. Mimi nipo tayari kufanya kazi "bila malipo" kama ntapewa kila kitu cha kuniwezesha kuhishi na kunihakikishia maisha baada ya kustaafu hadi kufa kwangu. Neno bila malipo hapo juu nime liweka kwenye inverted comma kwani si sahii kusema silipwi wakati napewa kila kitu! na hicho kitu nitakacho pewa ndo ujira wenyewe!!!!, kwahiyo ndugu yangu mshahara wa rais ni jumla ya gharama zoote anazo gharamiwa na selekali kwa mwezi + na hizo miloni tisa na nusu.
 
Muvi yetu imefika epsode ya ngapi?

#Ngoma ikivuma sana mwisho hupasuka.
 

.. William Lukuvi alidai gharama za kumtunza Raisi ni sawa na bajeti ya mikoa mitano.

..madai hayo aliyatoa wakati akipinga hoja ya serikali 3 ktk hotuba ili maarufu aliyoitoa kanisani.

...lazima sasa tupate ufafanuzi wa kina na uwazi kuhusu matumizi ya serikali, ikiwemo mishahara, posho, na marupurupu, ya watumishi wote wa serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…