Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Hivi presidaa anapata muda wa kuaangalia international news km CNN kweli kupata exposure? na atakuwa anajibu hadi maswali ya redioni? Hadi lini! Ila anyway labda ndo uzalendo! Jk alikuwa akiandaliwa birthday na redio watu wanaponda !
 
Siku zote watanzania tumekuwa ni watu ambao ukisikiliza stori za serikali iliyoko madarakani imekuwa ni shida sana na hasa pale unavyoona kuwa ubepari umejaa serikalini na pia watu wanajiendeleza wenyewe tu, lakini kiukweli hilo halipo sasa hivi na hii imesaidiwa kwa kumpata mzalendo wa kweli.

Binafsi siiamini CCM ninayemwamini ni Magufuli kwa kuwa ameishi katika kipindi kichafu na yeye kuonesha usafi wake mwanzo mwisho.
Imefika kipindi skendo ya rais aionekani mpaka wanaanza kumuuliza mshahara wakati miaka yoote hawakuuliza.

Ukiangalia trend ya uongozi ni kushuka na kupanda manake moja anatengeneza anaefata anaaribu na anaefata anatengeneza
Kiukweli nchi ilifikia pabaya kweli kiasi kwamba mtu akiiponda serikali anakuwa maarufu na kweli anaponda vitu vya kweli.

Lakini sasa hivi upinzani inabidi watengeneze new plan na sii kuponda tu, upepo umebadrika na inabidi waende kasi kuliko kasi ya rais na hapo ndo watashika akili za watu wanaojielewa.

Nawakubali sana wapinzani na nataka upinzani uendelee kuwepo ili iwe kama Marekani kwa mfano, ingewezekana kukawa na vyama viwili tu au vitatu tu ingependeza sana.

CHADEMA ni chama kizuri ila ukweli bila ushabiki wa kijinga inabidi watengeneze system yao ili iwe ya kidemokrasia zaidi kuliko kupendeleana na pia ili kujiosha wangesuka uongozi wao upya. Kimekuwa chama kikubwa na inabidi kijinusuru kuanguka.

CCM nayo haiaminiki manake mabepali yamejaa mle kiasi kwamba unaweza kuona mtu mchapakazi sana kumbe sio mzalendo bali serikali ya magufuli inakutaka uwe hivyo
cha msingi ni katiba mpya tu na hakuna kingine.

Katiba ya Tanzania inaifanya serikali ya Tanzania kuwa kivuli cha rais
Kama rais ni mbovu serikali inakuwa mbovu kama rais ni msafi serikali inakuwa safi.
 
Rais Dk john pombe magufuli ametaja mshahara wake kuwa ni Tsh mil 9.5, huku akiahidi atatoa Salary slip zake punde akitoka mapumzikoni Chato.

Hiyo imetokea wakati wa kipindi cha magazeti leo tarehe 01/04/2016 ambapo watangazaji walisoma habari iliyoandikwa na n gazeti la nipashe kuwa Zito na Lissu waomba ataje Mshahara wake na ukatwe kodi

Wakiwa katika mjadara huo, walipokea taarifa kuwa Rais kawaskia na katuma taarifa ofisi za Clouds kujuza mshahara wake kuwa ni mil 9 plus na atatoa stakabadhi zake akirudi Dar.

Source Clouds 360 Asubhi hii.
Zitto: Mshahara wa Rais wa JMT ni sh 384/= mil kwa mwaka
 
kwa kulipwa kwake mil 9.5 hakumfanyi awapunguzie wengine mishahara...
 
Hivi presidaa anapata muda wa kuaangalia international news km CNN kweli kupata exposure? na atakuwa anajibu hadi maswali ya redioni? Hadi lini! Ila anyway labda ndo uzalendo! Jk alikuwa akiandaliwa birthday na redio watu wanaponda !
Kila zama na zama zake mambo yamwbadlikaa matatizo ya nchi ni mengi usikilize ya wenzio ya nn umbea mwingne huo
 
bado mkubwa sana /
ukizingatia.
-usafiri Burr
-chakula bure
-nyumba bure
vocha bure
-
 
Wakuu nataka kujua wabunge wanalipwa mshahara,posho ,marupurupu na posho mbali mbali shilingi ngapi?
Posho za vikao wanalipwa shilingi ngapi?
Je hayo wanayolipwa wnakatwa kodi
 
Hili swali sasa ni lazima Zito kabwe na Tundu lisi wajibu.
 
Kwa maoni haya hakuna jema ambalo Rais atafanya na wewe ukalikubali...pole sana, comrade.
Ndugu yangu hii nchi ina shida kubwa sana. Hata sisi Wananchi ni tatizo. Tumekuwa malimbukeni wa siasa, kila kitu tunakosoa kwa mitazamo ya kisiasa tu. Mimi naimani humu JF kuna watu unaweza kuta ni wajuaji sana lakini ukakuta hata kuendesha maisha yao tu wameshindwa na kubaki kuilalamikia serikali kwa kila kitu.
 
Najiuliza hivi Clouds Tv ndo imekuwa Tv ya Taifa ambako mkulu anatolea taarifa? Haya mahaba ya JPM kwa clouds yametokana na nini? TBC ii wapi?? Natamani kumsikia pia Mr. Buhohela....
 
ni ile siku muhimu kwa mjinga bin mpumbavu ! sioni zaidi ya hapo !!
 
Back
Top Bottom