Sidhani kama ni hoja muhimu kujadili mshahara wa Raisi. Matatizo ya watanzania sioni kama mojawapo ni mshahara wa Raisi kwamba ama mdogo au mkubwa.maana raisi ni kila kitu na kwamba kama ataamua hata Ku acha mshahara akaanza kutumia ikulu kwa maslahi binafsi basi dili moja tu linaweza Ku cover mshahara wa kipindi chote cha utumishi na pengine pesa yake itaweza kutosha kula maisha yake yote na ukoo wake mzima.
Ni vema tukakumbushana kwamba ilifikia Wakati tulihitaji raisi wa aina hii ambaye hata wapinzani ahadi zao ilikuwa kuinyoosha nchi. Je wangewezaje kuinyoosha pasipo kuumiza baadhi ya watu. Ukinyoosha maana yake lazima u-strain na kwa kufanya hivyo lazima Kuwe na maumivu.
Kumbuka kuwa tunazungumzia kunyoosha na sio kurekebisha. Maana ukitekebisha unaweza ukawa unapita mlemle. Hatutaki hilo.
Ni ukweli kwamba maisha yamepanda gharama. Unga, sukari, maharage, MAFUTA, nk lakini ukiwa kwenye mpito lazima mtikisiko utokee. Naamini katika mafanikio. Jpm atatufanikishia hata kama tunapitia magumu.