Rais Magufuli ni lazima atetewe kwa nguvu zote dhidi ya udhalimu wowote

Mbona yeye alisema serikali zilizopita hamna walichofanya,lakini juzi tumeorodheshea Mambo ya maana yayozidi yake?Tena yanayogusa maisha ya Mtz moja kwa moja?
 
Ok, safi kabisa! Tuanzie hapo, haya kitu gani kipya kimefanywa ili tuweze kuwapinga kwa hoja?
 
Kwa maana nyingine Wananchi wa Nchi zifuatazo hawakuwa Wazalendo
1.Waganda kutomtetea Idd Amin
2.Wakongo kutomtetea Mobutu
3.Wasudan kutomtetea El Bashir
4.Afrika ya Kati kumtosa Bokasa
 
Mi namtetea kwenye haya unamwonea tu.
Kweli hawezi kuwa Malaika.

Ila Kama anajitahidi.
Tunamsuport kiaina upinzani mda mwingine inazingua.
Huwezi kupinga kila kitu.

Vingine fanya Kama huvioni.

Ni kutuzinguua wanachi tu[emoji4]
Natamani wangepotea ndugu zako mkaturudishia Ben saa8, azory nk
 
Ok, safi kabisa! Tuanzie hapo, haya kitu gani kipya kimefanywa ili tuweze kuwapinga kwa hoja?
Elly Mshana, urewedi avae.

Kumpima Rais na serikali yake unaangalia ni mambo gani yamefanyika katika kipindi chake.

Kwanza unaweza kuona ongezeko kubwa la ukusanyaji wa kodi. Jambo la kwanza Rais alilofanya ni kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato na kuongeza nguvu katika ukusanyaji. Kutoka bilioni 900 kwa mwezi mpaka wastani was yrilioni 1.3 - 1.6. Pesa hizi ndio zinazofumika kulipa mishahara na kufanya shughuli za maendeleo.

Tunamtetea Rais na serikali yake kwasababu ameonesha kwa vitendo Nia yake ya kufufua shirika la ndege. Watu wabapinga na kuwaaminisha wengine kuwa hilo sio jambo la kipaumbele. Utawasikia " ndege zinamsaidia nini bibi yangu aliyepo nanyumbu?". Ukweli Ni kuwa ili uimarishe shughuli za uchumi basi ni muhimu kwanza uhakikishe urahisi wa safari za ndani. Wafanyabiashara was ndani na wawekezaji pamoja na watumishi wa umma wanaweza kutimiza majukumu yao vizuri na kwa haraka. Hii inamaana sana kiuchumi japoninahitaji utulivu wa akili kliona hili. Uimarishaji wa usafiri wa anga umehusika pakubwa kuvutia watalii.

Kama haitoshi, Tanzania ni moja ya nchi chache duniani yenye vivutio vingi sana vya utalii. Utalii ni sekta ambayo ikiimarishwa vizuri inaongeza sana pato la taifa. Rais anakuza sekta hii kwa weledi mkubwa. Manunuzi ya ndege zetu binafsi sio tuu inakuza sekta hii bali inatuhakikishia ulinzi na ajira kwa watu wetu. Huduma za ATCL pamoja na mapungufu ya hapa na pale ni nzuri. Binafsi ni mtumiaji mzuri wa huduma zake.

Njoo kwenye ujenzi wa stiglers gorge. Hii ikikamilika itasaidoa sana uhakika na wingi wa umeme. Kimkakati, hii itaboresha maisha ya watu kwa kuhakikisha nishati hiyo inafika sehemu nyingi zaidi na kwa gharama nafuu. Isitoshe viwanda vitapata nishati ya uhakika zaidi kwa gharama nafuu na kupunguza gharama za uzalsihaji.

Mradi wa stiglers gorge unapingwa na maadui si wa nje tuu bali na wa ndani pia. Hapa kwanini tisimtetee Rais kwa kuzungumza ukweli kwa kupinga propaganda mufilisi?

Nadhani Elly Mshana umeelewa. Karibu tumtetee Rais pamoja na serikali yake. Tuhakikishe tunamlinda kwa maombi na kumtia moyo. Zaidi sana kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuweka uzalendo mbele.
 
Basi sawa
 
Kwa maana nyingine Wananchi wa Nchi zifuatazo hawakuwa Wazalendo
1.Waganda kutomtetea Idd Amin
2.Wakongo kutomtetea Mobutu
3.Wasudan kutomtetea El Bashir
4.Afrika ya Kati kumtosa Bokasa
Ndugu Bila Bila kwa mara nyingine tena unatoka bila bila.

Amin, Bokassa, Mobutu na Al Bashir hawa wote hawana sifa hata moja ya kuwalinganisha na Magufuli. Tafuta mfano mwingine. Hii ni mada ambayo ukitaka tunaweza kuichambua siku nyingine. Toa shaka mimi ni mwanahistoria mzuri.

Jenga hoja yako? Nini sio sahihi katika hili bandiko langu? Ungana nasi kumtetea Rais na serikali yake. Hii sio kwa manufaa yako binafsi. Fanya kama unafanya kwa nchi yako.

Karibu kwetu, sisi ni kundi kubwa, kundi la ushindi
 
Mtu kashindwa kuajiri kwa kipindi cha miaka 5 pamoja na kupandisha watumishi madaraja, alaf unadai ametenda mambo makubwa?
 
Sijsoma content ya ndani ila siwezi kupoteza muda kumtetea LIFUGUMA.
 
Sijakuelewa mkuu
Ungekuwa na akili ya kufuatilia mambo ungeelewa ila kwakuwa wewe ni zuzu la kusifia hutaelewa kamwe. Ni wapi uliwahi kusafiri wakakuambia kuwa una bahati kumpata Magufuli?
 
mbele ya hukumu yoyote ambayo si ya kimahakama, mtetezi ni matendo na maneno ya mlengwa mwenyewe.

wanaojiita watetezi ambao muanzisha uzi anawalenga ni wapambe tu wenye maslahi binafsi... hawa hata wanayejifanya kumtetea anapofanya baya au kosa kwao linabaki kuwa zuri tu.
 
Siku akitoka madarakani tutapewa takwimu aliteka wangapi, alitupa viroba vingapi na aliwapoteza wangapi. Hatutasubiri takwimu wakati wa maombolezo.
 
"Uthubuti sio kwenye biashara tuu, ni kwenye kila jambo"

Kwa kunukuu kipande hapo juu kilichopo ndani mada yako, mbona hakina ukweli wowote ndani yake. Kidogo ungedadavua zaidi, wapi ambapo unasimamia hasa, uthubutu wenye uelekeo chanya ama hasi na hata kuweza kuleta matokeo yenye tija.

Ilikuwa ni uthubutu wenye uelekeo na matokeo hasi kwa kutoa fomu moja ili kwa makusudi kukwepa kupambana na mtia nia mwingine. Uthubutu hasi huu ulianza mapema kwa kumfuta uanachama mtu tishio ktk nafasi ya uongozi unayoikalia.

Hapo hujagusia hujuma za wazi kwa viongozi wa vyama vya upinzani kuendesha shughuli zao halali za kisiasa kwa mujibu wa katiba na sheria. Uthubutu wa kukubali kukosolewa kupitia vyombo huru vya habari.
 
Ukimtetea mgomvi asiye na nguvu mnapigwa wote
 
Kwenye kilimo amegusa nini?

#YNWA
Liverpool, what a nice name.

Kilimo ndio sekta iliyoajiri asilimia kubwa ya watanzania, zaidi ya 70%. Hivyo uwekezaji kwenye kilimo ni kuwekeza kwa watanzania wengi. Utakubaliana nami kuwa kilimo ni eneo lenye changamoto nyingi na uwekezaji wake pia unahitaji pesa, utaalamu na umakini mkubwa.

Pamoja na kuwa bado kuna mengi ya kufanya, Rais Magufuli na serikali yake wamejitahidi sana.
Uimarishaji wa miundombinu ya barabara ni hatua nzuri katika kuwezesha usafirishaji wa pembejeo na mazao kwa gharama nafuu.
Utatuzi wa migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.
Kujitahidi kuondoa vishoka na kuhakikisha mkulima anapata walau bei nzuri
Kuimarisha tafiti za kilimo
Uwepo wa soko la uhakika wa bidhaa za kilimo kwa uanzishwaji wa viwanda vinavyotumia bidhaa za kilimo

Mambo ni mengi ila natambua kuwa bado Rais na serikali yake wanayo mengi y kufanya kwenye sekta hii
cc: Bashe et al
 
Wewe wasema
 
Come on guys, kuna mtu atakuja ajenge angalau hoja moja tuu? Mbona mmekuwa wepesi sana?

Ukweli una tabia moja, hata ukiupinga machoni moyoni unaukiri. Tokeni huko gizani, njooni huku tushirikiane kujenga Tanzania mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…