Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Huu ulikuwa mpango maalum wa kurudisha imani ya wananchi kwenye serikali yao ambayo imepoteza mvuto kwa kiwango kikubwa, hiyo ndio miujiza inayo fanywa hapa tz, TWAWEZA walipotoa utafiti unao lenga ukweli na hali halisi yule bwana alishambuliwa vibaya mno.
 
Ndugu yangu hao wote waliandaliwa kwajili yakujaribu kuwarejesha wananchi imani iliyokwishapotea. Lkn pia limegonga mwamba.
 

Wakaleta na watoto wa Sekondari ili na wenyewe washriki mdahalo , mtoto mmoja akasema eti tunahitaji Magufuli kama watatu hivi wafuatane ili tuweze kuendelea, kimoyomoyo nikasema Child you don't know what you are talking about! hahahaha
 
Jambo lolote likimuhusisha jiwe utengemee janga tu...sikuwa hata na muda wa kufuatilia nilijua upuuzi tu
 
Hayo ni mawazo yako mtoa post na hukatazwi kuyawaza.

Acha ukweli ujitenge na uongo.

Rais anafanya kazi kubwa na anastahili pongezi za dhati na wala si kana kwamba walikuwa wanamsifia.
 
So touching
 
jamani, Magufuli kajitahidi san, tumpe haki yake
Aliteuliwa kufanya nini? Je alichotakiwa kukifanya kimeshakamilika na amefanya ziada ya matarajio kustahili bonus ya sifa na pongezi? Just thinking aloud!
 
Kitu cha msingi katika kongamano lolote ni kumpa Rais idea za kuliokoa hili taifa,ukimsifia sana ata yeye atafahamu unamsifia, ila ukimpa nafasi ya upeo wako nini kifanyike katika lile analofanya ili mambo yawe bora lazima atashukuru ndani ya roho yake.Ukileta dharau hakika utapata tabu..sasa watu ni waoga wanaogopa kumpa mpango wanahisi ataikataa (Kitu ambacho si kweli).Mtu AKIKUSIFIA SANA inabidi UMCHUNGUZE hivyo hivyo Mtu AKIKUKASHIFU inabidi umchunguze
 
Kutumia jeshi kujenga ukuta Marerani ni kukiri kwamba kampuni au taasisi za kiraia za ujenzi zina kasoro hazifai. Solution sio kutumia jeshi, ni kurekebisha kasoro. Ili kulinda au kukuza ajira.
 
yale ndiyo yalikuwa malengo ya baraza lile la kahawa.
ona namna yule mwanafunzi alivyojipanga. ati anaulizia upatikanaji wa MAGUFULI kwamba hakukuwa na mtu aloandaliwa / succession planning ye kajuaje? kwamba asitokee mtu akagombea na kuharibu mipango ya MAGUFULI, hii imetokana na yale makelelee ya twende na membe 2020 hapo wiki iliyopita! anakwenda anasema waje MAGUFULI wengine watatu mbele. huyu ni amma anawandaa wananchi kisaikolojia au anawatisha washindani wake kisiasa
 
Kila siku anasema yaleyale kama unafatilia utagundua hotuba yake hiyo kila siku anizungumza .watumishi hewa. Bodi ya mikopo.strigls .barabara na reli.safari xa nje na posho hana lingine
Maigizo yamechina. Ulimwona Prof Kabundi, msanii wa makinikia akiwa na Prince Makonda waalivyokuwa wanashangilia kwa pamoja kutupwa kwa katiba mpya?
 
Ndicho tulichotarajia wengi kwani baada ya kuona majina ya wale ma-prof. tukajua ni mwendo wa kusifias mwanzo mwisho na ukweli hautasemwa!
Kwa taarifa tu ni kuwa Ethiopia wana miundo mbinu bora na ma-fly over kila eneo lkn wananchi wake kila kukicha wanakimbia nchi yao kutokana na utawala.
 

Mkuu wangu sasa hivi ni mwendo wa kusifu na kuabudu, PhD tupa kuleeeeeeeeeee!!!!
 
Niltegemea Hoja kuhusu uwanja wa ndege wa chatu, rushwa kubwa za vyeo vya ubunge na udiwani,double standard hewa kuhusu bomoabomoa ajira,watu wasiojulikana kuwa na nguvu kuliko dola.nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…