Hio ndio inapaswa kuwa kauli ya kiongozi...sio kuwapa watu matumaini hewa...
Kuna Kipindi nilisema kuwa huu msemo wa HAPA KAZI TU kuna siku utakuwa kinyaa, naona yametimia haiwezekani mtu kupoteza ndugu na hana pa kulala unamwambia akafanye kaziDu! Mtu afanye kazi uku analala kichakani
Sema tutakuchangiaKuna Kitu Ningependa Kusema Kuhusu Mwonekano Mpya wa Rais,ila Sina 7m...
Acha Nifunge Bakuli Langu...
Huyu jamaa ni janga kuliko tetemeko lenyeweKwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.
Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.
Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.
Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.
Wasukuma nyodo asili yao....!!Miaka mitano tutaona Kama decade kwa mipasho utafikiri mswahili dah aseee.
Sipati picha watu wamekaa msibani ndugu kafa, nyumba imebomoka, pakulala ni Shida, watoto wameanza kupata maradhi kutokana mabadiliko ya aina ya maisha na mateso. Halafu wanasikia Rais kwa Mara ya kwanza atatoa neno hivyo wanahamu na matumaini ya kumsikia atasema nini lakini wanaishia kuambiwa "msibweteke fanyeni kazi kujinusuru serikali haiwezi kufanya yote. Tetemeko halikuletwa na Ccm"Maneno ya faraja bado yanahitajika zaidi katika jambo hili, watu wamepoteza familia zao, mali zao hivyo tuendelee kuwapa faraja.
Upo chato au kijiji gan?Na mm huku kijijini upepo umeondoa bati nasubiri serikali ije inisaidie kuezeka
Ndio baadhi yetu tulikuwa tunasema kukaa kwake kimya ilikuwa ni heri. Akifungua kinywa tu, basi kuna watu ikiwa ni pamoja na wahanga wa janga hili watakwazika. Kazi ya serikali ni nini? Kwa nini basi serikali inakusanya kodi? Ndio, watu wachangie na waliishaanza kuchangia lakini ilikuwa ni WAJIBU wa anayekusanya kodi kuwa wa kwanza ama kutangulia kutoa huduma ya kwanza na kutoa uelekeo wa kitaifa katika kipindi cha masaa 24. Itamchukua muda mtukufu kujua majukumu ya serikali.Nimemsikia akisema waathirika wa tetemeko la ardhi wafanye kazi wasikae tu kusubiria Serikali iwasaidie, tetemeko halijaletwa na Serikali
Hali mbaya na Mwenye uwezo hawezi ngoja serikaliHilo la kusema watu wajiongeze wasisubir serikal ni ukwel fulan mchungu ambao hatuwez kuukubali.
Kwa maana kuna mtu anaweza kua na ufa tu Ila akakaa kusubir....
As long as una uwezo wa kufanya kitu fulan basi uanze nacho.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Ndiyo mkuu! Kama kuna walioamini kuwa kupatwa kwa jua kuliratibiwa na serikali tukufu ya Jpm na kuamuliwa kuwa tukio hilo lifanyike Mbeya wanashindwa vipi kuamini kuwa tetemeko ni kazi ya serikali? Kama ujinga Ni mtaji basi serikali ina 99% ya share zote.