Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,998
inawezekana wachaga wanamchukia Magufuli. Lakini kuna sababu gani ya kumpenda mtu ambaye anaamini kwamba palipo na "wachaga" wengi anabomoa nyumba bila fidia tena kwa ubabe na ukatili wa hali ya juu. huko Mwanza ambapo japo wachaga wapo, lakini ni "kwao Magufuli", anasema hawa msiwabomolee, walinichagua. Wana sababu gani ya kumpenda mtu ambaye anaonekana kuwaandama kila kukicha na kila mahali, na akionekana kabisa kwamba anataka "kuwashughulikia"?Mtu akitaka likes za kufa mtu kutoka kwa Wachaga ili ajisikie vizuri hakuna kinachosaidia kama Magufuli bashing!
Yeye mwenyewe ndiye ameleta haya mambo ya kikabila. Nyerere alishughulika na "Chaga issue" kwa kujenga na siyo kwa kubomoa kama Magufuli.
Lakini pia si kweli kwamba wanao-mbash Magufuli ni wachaga tu. tupo wengi tu ambao siyo wachaga. Magufuli ameumiza watanzania wengi. wangapi wametumbuliwa? familia zao, ndugu zao, marafiki zao? wakulima wa mahindi kwa ujumla hawana hamu na Magufuli. Wafanyabiashara hawana hamu na magufuli. Watumishi wa serikali hawana hamu na Magufuli. Watanzania wengi tu hawana hamu naye. hivyo usipotoshe kudai kwamba ni wachaga tu