Rais Magufuli; ubanaji matumizi; na kujichanganya [contradict]

Rais Magufuli; ubanaji matumizi; na kujichanganya [contradict]

Wala sikujua nani amepost. Mimi nilijikita kwenye content tu, na nikaona nitoe hizo facts ambazo nilijua mwandishi amezi-overlook. Hata hivyo, mada zako kama zikinigusa kama ilivyonigusa hii nitaendelea kuchagia, na wewe ukijisikia endelea kutukana tu kama ambavyo huwa unatukna siku zote!

Msseenge wewe.

Eti hukujua nani ameposti wakati umenikwoti na kunitaja kabisa!!

Wakati unanitaja hukujua unamtaja nani?
 
South Africa waliamua kila muhimili wa dola kuwa na mji wake mfano ni mji wa Cape Town ni makao ya Bunge Parliament of the Republic of South Africa - Parliament of South Africa , mji wa Pretoria makao ya Serikali Pretoria is proposed as the new capital of ZAR na mji wa Bloemfontein ni makao ya Mahakama Home. Na hiyo ni miaka (miongo) mingini ya nyuma.

Tukirudi hapa Tanzania ni uoga wa serikali ya awamu ya 5 kuona Bunge lipo mbali na serikali iliyopo Dar es Salaam na pia kujitakia sifa zisizo na mashiko zilizopitwa na sayansi /teknolojia ya karne hii kama wachangiaji wanavyohoji gharama na mantiki ya kulazimisha kuhamisha kila kitu Dodoma.
Sawa mku mimi sijakataa. Pendekeza ulitakaje? Mji wa Mahakama uwe wapi Morogoro? Bunge lingebaki Dodoma sio? Alafu makao ya Serikali wapi Singida au Mwanza?
Sasa hapo pangekua patamu kama una Document unaichukua Wizarani( Mji wa Serikali) uirudishe Mahakamani na urudi Bungeni nako ni mji mwingine. Pesa yako yote itaishia kwenye mabasi.
 
Sawa mku mimi sijakataa. Pendekeza ulitakaje? Mji wa Mahakama uwe wapi Morogoro? Bunge lingebaki Dodoma sio? Alafu makao ya Serikali wapi Singida au Mwanza?
Sasa hapo pangekua patamu kama una Document unaichukua Wizarani( Mji wa Serikali) uirudishe Mahakamani na urudi Bungeni nako ni mji mwingine. Pesa yako yote itaishia kwenye mabasi.

Serikali kuu ibaki Dar es Salaam huku Bunge likiwa makao yake Dodoma na labda Mahakama za Rufaa /Mahakama Kuu kuhamia ofisi za Kesi za Umoja wa Mataifa (Genocide) jijini Arusha The ICTR in Brief | United Nations International Criminal Tribunal for Rwanda.

Hii ingewezesha mihimili ya dola kuwa huru zaidi na viongozi wake Mahakama / Bunge kutohudhuria sherehe za kila siku Ikulu kama ilivyo sasa awamu ya 5, nia ya awamu ya 5 ni kuua 'uhuru' wa viongozi wakuu wa mihimili ya Mahakama na Bunge kuwatoa ofisini na kushinda Ikulu ktk hafla Kibao zisizo na mashiko .
 
Alipoingia madarakani aliingia kwa kasi na mbwembwe za kutaka kubana matumizi.

Akawakoromea wabunge kuhusu pesa za tafrija zao huko Dodoma, akaamuru kusiwepo na sherehe/ shamrashamra za sikukuu ya muungano, na kadhalika.

Baadhi yetu tukayaafiki hayo maamuzi. Tukaona ni mwanzo mzuri maana mabilioni ya pesa yalikuwa yakitumika kiholela tu kwa sherehe za masaa machache wakati kuna mambo mengine yaliyo ya muhimu ambapo hayo mabilioni yangeweza kutumika.

Baadaye kidogo akaja na hizi habari za serikali kuhamia Dodoma.

Sikuelewa! Nikajikuna kichwa.

Nikajiukiza, kama kweli mtu anayechukia mambo ya kutumia hovyo pesa za walipa kodi, inawezekanaje mtu huyo huyo ndo akawa mstari wa mbele katika kutaka kufanikisha jambo ambalo litagharimu mabilioni [kama siyo matrilioni] ya pesa za walipa kodi?

Nikajaribu kutafuta sababu iliyo ya lazima kuendelea na huo mpango wa kuifanya Dodoma ndo iwe mji mkuu, nikakosa!

Wazo lililokuwa na maana miaka ya 70 huko leo hii si lazima liwe na maana tena.

Leo hii sioni sababu ya kuingia migharama mikubwa kuhamisha makao makuu ya nchi.

Hapo ndipo napoona Rais Magufuli hayupo consistent kivile katika maamuzi mazuri ya matumizi ya pesa za walipa kodi.

Anabana matumizi huku lakini anaenda anatumia vibaya kule.

Mwisho wa siku inakuwa ni kazi bure tu! Inakuwa hujabana chochote!!

Ndo kujichanganya kwenyewe huko.

Heri ya 2019.

Wenu daima,

Nyani Ngabu au ukipenda, niite NN.
Ukiongeza na ile Tshs. 1.5T ndo kwisha kabisaa
 
Usalama gani?

Hadi hivi sasa tumeathirikaje na Dar kuwa mji mkuu?
DSM ni makao yaliyo chagukiwa na wakoloni Kwa sababu walizo nazo wao ikiwa pamoja na urahisi wa usafiriji bidhaa na watu. Lakini Kwa dunia ya leo, location ya huo mji haufai kuweka serikali, Kwanza gharama za kulinda ukanda mrefu katika bahari ya Hindi ni kubwa sana kuliko kuhamia Dodoma. Hata maswala ya tabia nchi sio rafiki kwetu kama tunavyoona mlolongo tsunami zinakumbwa fukwe za nchi nyingi duniani.
 
DSM ni makao yaliyo chagukiwa na wakoloni Kwa sababu walizo nazo wao ikiwa pamoja na urahisi wa usafiriji bidhaa na watu. Lakini Kwa dunia ya leo, location ya huo mji haufai kuweka serikali, Kwanza gharama za kulinda ukanda mrefu katika bahari ya Hindi ni kubwa sana kuliko kuhamia Dodoma. Hata maswala ya tabia nchi sio rafiki kwetu kama tunavyoona mlolongo tsunami zinakumbwa fukwe za nchi nyingi duniani.

Lame reasons.
 
Wazo la kuhamisha makao makuu lilianza wakati wa ukoloni wa Wajerumani hasa wakati wa vita ya kwanza ya dunia walipohamishia makao Tabora kwa muda mnamo mwaka 1916. Mwaka 1959 Kupitia LEGCO Waingereza walipendekeza makao yahamie Dodoma lakini hatua hazikuchukuliwa kutokana na gharama kuwa kubwa. Mwaka 1966 Joseph Nyerere mdogo wake Mwalimu alipeleka muswada binafsi bungeni kuhusu serikali kuhamia Dodoma kwa awamu, lakini pia haikufanikiwa kupitishwa. Mwaka 1972 kamati kuu ya TANU ilifikia maamuzi ya kuhamishia makao makuu ya TANU Dodoma kwa sababu kuu tatu.

Mosi, Kwa kuwa Dodoma ni katikati na inaweza kufikiwa kirahisi tokea pande zote za Tanzania.

Pili, kutokana na kuwa nyuma kimaendeleo na kuwa kwa kuhamishia makao ya chama kungechangamsha uchumi, na

Tatu. Ni kwa ajili ya Usalama kwa kuwa bara kulionekana kuwa salama kuliko ukanda wa pwani

Mwaka huohuo serikali pia ilichagua kampuni tatu za kataifa ili kupendekeza sehemu na master plan ya mji mkuu wa nchi. Uamuzi wa kuhamisha mji mkuu ulifikiwa katika mkutano mkuu maalum wa TANU Oktoba 1973. Na baadae Mwalimu alitangaza kupitia redio kuwa serikali na chama vitahamia Dodoma katika kipindi cha miaka 10


Serikali ilichukua hatua kadhaa. Kwanza ni kwa kuunda Wizara ya Maendeleo ya mji mkuu Chini yaOfisi ya Rais na pia kuunda Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) .Waziri wa kwanza akiwa Chifu Adam Sapi Mkwawa na Mkurugenzi mkuu wa CDA wa kwanza akiwa Sir George.

Majukumu ya kwanza ya Mamlaka ilikuwa ni:

Mosi, Kutafuta wana Mipango miji (Master planners) ambapo waliitisha tenda na kampuni kutoka Canada; Project Planning Associates ilichaguliwa

Pili, Ku recruit wafanyakazi wa mamlaka ampapo Sir George alianzisha kurugenzi tisa na kila kurugenzi ikiwa na Mkurugenzi na timu yake.


Kazi nyingine ilikuwa ni kuainisha eneo ambapo mji mkuu utajengwa na waliainisha maeneo sita tofauti na hatimaye wakachagua eneo moja karibu na mji wa zamani.


Kazi ya kutengeneza Master plan ilichukua miaka miwili na jopo la majaji likiongozwa na mtaalam Sir John Overal aliyekuwa Mkurugenzi wa Australian National Capital Development Commission walipitisha master plan mnamo Februali 1975. Master plan ilikuwa imegawanywa katika maeneo 4 yakiwemo Eneo la mjini (Downtown) ambapo pangekuwa na ofisi za serikali, bunge, mahakama na maeneo ya biashara

,Eneo la makazi ambapo makazi yalipangwa kwa mujibu wa mtindo wa TANU wa nyumba kumi. Eneo la tatu ilikiwa Maeneo ya wazi na bustani za kupumzikia na Eneo jingine ilikuwa miundombinu ya usafirishaji.


Mwalimu alipendezwa sana na mpango huo uliokuwa ukiakisi siasa ya ujamaa.


Ilikuwa imekadiriwa kuwa ujenzi utachukua miaka 10 kuanzia mwaka 1976 hadi 1986 na ungegharimu shilingi bilioni 3.6 au dola za Marekani milioni 53


CDA Pia ilikuwa na jukumu la kuweka miundombinu kama maji, barabara nk.


Pamoja na malengo mazuri hali ya uchumi baada ya hapo haikuwa nzuri kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta, Vita vya Kagera nk. CDA ikaambulia kupata 10% tu ya makadirio ya gharama hata hivyo walifanikiwa kujenga baadhi ya miundombinu ikiwemo barabara pamoja na mfumo wa maji machafu na salama. Pia walijenga ikulu ya Chamwino na baadhi ya ofisi za serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma ilani ya uchaguzi ya CCM ndiyo utaelewa. Mie nadhani JPM hapaswi kulaumiwa, yeye anatekeleza maagizo ya chama chake kilichompa dhamana ya kuwa Raisi. Mengina mnayoandika ni porojo tu. Uncle Magu endelea na moto huu huu.
 
Lame reasons.
So far you've lost merit of your argument, Kwanza hujafanya utafiti kuona ni kiasi gani kitatugharimu kuhamia Dodoma zaidi ya kuweka hisia tu. DAR ikiwa only 55m above sea level vs 1,120m za Dodona sijuwi wapi unajiona salama. Au unataka siku moja watu waogele na mafaili ya serikali ndio uanze kujiuliza tulikuwa wapi?
 
Ahsante NN,
Sio wewe peke yako, wapiga vigelegele wenzio wote wameanza kurejewa na akili zao!!

Ni kitambo kidogo tu wote tutaongea lugha moja!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kusikia kwa kenge mpk..............
Naona sasa hivi NN anaanza kuchuruzika damu masikioni mwake.
Ila kwa kua yupo nchini kwa sasa ataona uhalisia wa kile alichokua anakipigania.
manengelo njoo huku uunge mkono juhudi za Nyani Ngabu

Sent from my GT-P5200 using Tapatalk
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kusikia kwa kenge mpk..............
Naona sasa hivi NN anaanza kuchuruzika damu masikioni mwake.
Ila kwa kua yupo nchini kwa sasa ataona uhalisia wa kile alichokua anakipigania.
manengelo njoo huku uunge mkono juhudi za Nyani Ngabu

Sent from my GT-P5200 using Tapatalk


😂😂😂 leo ameyatema?ngoja nimsome..mm kila siku ninaunga juhudi za mheshimiwa Rais..na ile kauli yake anataka kila mkoa uwe na viwanda 100 kila mkoa naona inafanikiwa kwa kasi...
only in Tz!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] leo ameyatema?ngoja nimsome..mm kila siku ninaunga juhudi za mheshimiwa Rais..na ile kauli yake anataka kila mkoa uwe na viwanda 100 kila mkoa naona inafanikiwa kwa kasi...
only in Tz!
Kenge zote sasa hivi taraibu zinaanza kusikia nasubiri zamu ya barbarosa ifike.

Sent from my GT-P5200 using Tapatalk
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kusikia kwa kenge mpk..............
Naona sasa hivi NN anaanza kuchuruzika damu masikioni mwake.
Ila kwa kua yupo nchini kwa sasa ataona uhalisia wa kile alichokua anakipigania.
manengelo njoo huku uunge mkono juhudi za Nyani Ngabu

Sent from my GT-P5200 using Tapatalk

Miaka yote nimekuwa nikipinga kuhamia Dodoma.

Sijaanza jana wala leo.

Au labda wewe umeanza kunisoma lini?
 
Kenge zote sasa hivi taraibu zinaanza kusikia nasubiri zamu ya barbarosa ifike.

Sent from my GT-P5200 using Tapatalk
😂😂😂 kuna kenge 1 ina upara ilisalenda baadaye ikaja geuka..ile inaipenda san cdm inaogopa tu kujiweka wazi...hyo kenge uloitaja hyo inalamba makalio daily ya mkulu
 
Hii Serikali inatumia mabilioni bila sababu.
Kujenga ofisi za wizara na idara Dodoma wakati Dar es salaam kuna ofisi ,kwa nchi masikini hatukutakiwa kufanya hivyo.
Kufanya chaguzi ndogo za madiwani na wabunge bila sababu,Nina amini kabisa hakukuwa sababu za uchaguzi kama maendeleo hayana chama hakukuwa sababu ya kuwahonga wabunge na madiwani wa upinzani ili wahamie CCM.
Wakati yeye anamnanga Kikwete kwamba hela nyingi zilipotea kwa wapiga dili awamu ya nne,rais wa awamu ya sita atamnanga yeye kuwa hela nyingi zilipotea kwa kufanya chaguzi za hovyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
ndo maana wanahangaika kichinichini asiondoke,huu siku akitoka utafumuliwa uvundo wa ajabu sana
 
Miaka yote nimekuwa nikipinga kuhamia Dodoma.

Sijaanza jana wala leo.

Au labda wewe umeanza kunisoma lini?
Nmekusoma kwa muda mrefu sana ila nilikua sitaki kukulaumu kwa sababu ya mambo mkuu mawili.
1) Nnajamaa zangu wengi wapo nje ya nchi wao mara nyingi sana huko walipo ni watu wa kusifia na kuunga mkono juhudi, ilifikia baadhi wakawa mpk wananikashifu kwa kuniita mimi ni mpiga dili, ila wengi walio bahatika kuja nchini na kukaa kwa muda mchache tu kwa waliyoyaona hapa wamekiri wenyewe ni tofauti kabisa na jinsi walivyokua wanafikiria wao kabla ya kujionea hali halisi ilivyo.
2)Kawaida (damu ni nzito kuliko maji) hili nadhani unalifahamu maana nlikua nakwambia mara kwa mara hivyo haina haja ya maelezo mengi.

Sent from my GT-P5200 using Tapatalk
 
- Kuhamia Dodoma
- Siasa za hovyo ("kuunga mkono juhudi") zinazotufanya turudie chaguzi za wabunge (hili partly ana share lawama na wahamaji)
- Kununua madege mengi tena kwa cash
- Uwanja wa ndege wa Chato (katika maamuzi ya hovyo kwangu ni namba moja)
- Ametengeneza "woga" kwa watumishi wa umma na mihimili mingine ya dola....hili lina gharama kubwa sana ambazo haziwezi kuonekana moja kwa moja.

Nk nk

Hatukatai, kuna mengi tu anafanya mazuri kwa nchi yetu.
 
Back
Top Bottom