Rais Magufuli; ubanaji matumizi; na kujichanganya [contradict]

Mtu akitaka likes za kufa mtu kutoka kwa Wachaga ili ajisikie vizuri hakuna kinachosaidia kama Magufuli bashing!
inawezekana wachaga wanamchukia Magufuli. Lakini kuna sababu gani ya kumpenda mtu ambaye anaamini kwamba palipo na "wachaga" wengi anabomoa nyumba bila fidia tena kwa ubabe na ukatili wa hali ya juu. huko Mwanza ambapo japo wachaga wapo, lakini ni "kwao Magufuli", anasema hawa msiwabomolee, walinichagua. Wana sababu gani ya kumpenda mtu ambaye anaonekana kuwaandama kila kukicha na kila mahali, na akionekana kabisa kwamba anataka "kuwashughulikia"?
Yeye mwenyewe ndiye ameleta haya mambo ya kikabila. Nyerere alishughulika na "Chaga issue" kwa kujenga na siyo kwa kubomoa kama Magufuli.

Lakini pia si kweli kwamba wanao-mbash Magufuli ni wachaga tu. tupo wengi tu ambao siyo wachaga. Magufuli ameumiza watanzania wengi. wangapi wametumbuliwa? familia zao, ndugu zao, marafiki zao? wakulima wa mahindi kwa ujumla hawana hamu na Magufuli. Wafanyabiashara hawana hamu na magufuli. Watumishi wa serikali hawana hamu na Magufuli. Watanzania wengi tu hawana hamu naye. hivyo usipotoshe kudai kwamba ni wachaga tu
 
Hapo ndipo hali ya maisha itakuwa ngumu sana sina uhakika km madeni ya ndani yamelipwa yote Kulipa madeni ya ndani huchochea mzunguko wa pesa kuto lipa madeni ya ndani ni kudumaza uchumi wa nchi
 
Umesahau jambo muhimu la kutumia hela ya umma kuleta biashara ya kitumwa ya kununua binadamu
 
Hoja ya ukatikati wa Dodoma haina mashiko tena. Zama zimebadilika.

Unless labda tuwe hatuendi na wakati.
 
Tunahamia dodoma -gharama

Tunajenga express road from kimara to kibaha-gharama

Tunanunua midege mchanyato for cash-gharama

Tunajenga ma fly over at the same time -gharama.

Tunarudi uchaguzi kila baada ya miezi kadhaa-gharama.

Tunajenga stigler goji-gharama

Tunajenga standadi geji -gharama

Elimu bure-gharama

Aisee vyote hivi vikitimia barabara! Ndani huo muda basi naweza anko naniliu apewe sifa-ameeen!! Apewe sifa-ameen

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ndio ukweli kuhusu kutumia vibaya pesa za umma au walipa kodi, sehemu nyingine ambayo mimi naona ni pale alipohamua kununua wapinzani na changuzi za kila siku ni mabilioni mengi ya pesa yamekwenda katika chaguzi hizi. Sikuona haja ya mradi huo kama umeleta tija kwa wananchi na kuonyesha hivyo ndiyo maana watu wameishia kutokwenda kwenye vituo na kuchagua tena.
Mradi mwingine wa matumizi mabaya ya kodi ni huu alioanza na bado kanogewa wa kununua ndege. Sawa tulihitaji kulifufua shirika letu lakini kwanza tulipoanza tulihitaji kupata soko na route za kutosha ili tukiruka kweli tunarudisha faida. Na hii ya kujenga uwanja wa ndege Chato ni hasara tupu. Chato na Mwanza siyo mbali, kwa hiyo mradi huu ungependeza kama ilikuwa ni kupanua uwanja wa mwanza kuwa uwanja wa kimataifa
 

Nyani Ngabu wewe umejitambulisha kama muumini mkubwa wa magufulu na umekua ukimsifia kwa kila jambo na kuwakebehi wanaomkosoa. malalamiko na hoja za kuonesha ubovu wa magufuli na uongozi wake umekua ukiyapuuza sana. imekuwaje mkuu leo unaona mtukufu amekua na makosa
 
Hoja ya ukatikati wa Dodoma haina mashiko tena. Zama zimebadilika.

Unless labda tuwe hatuendi na wakati.

..hata mimi sioni ulazima wa mji mkuu kuwa katikati ya nchi.

..kuna mataifa mengi, USA ni mojawapo, yameendelea, lakini miji yao mikuu haiko katikati ya mataifa hayo.
 
standard Gauge Railway inaondoa ulazima wa kuhamia Dodoma kwani unaweza kulala Dar. na kufanyakazi Dodoma hivyo utafika kabla ya anayetoka Kunduchi kwenda Gongo la Mboto.
 
Duh chuki kwa Magu ni kubwa sana. Bila shaka inatokana na utendaji wake. Nyerere hadi anaondoka madarakani hakubadilisha nia ya kuhamia Dodoma, bado watu kwa macho makavu mnadanganya Nyerere asingefurahia kuhamia Dodoma, kisa! Magufuli kaweza, chuki kwa Magufuli inalazimisha kugeuzwa msimamo wa Nyerere!
 
Makao makuu lazima na maofisi yawe huko??
Katika mambo ambayo siyaelewi mojawapo ni hili. Hivi makao Makuu ni lazima kila kitu kiwe huko? Yaani Makao Makuu ya nchi humaanishwa Bunge, Mahakam na Ikulu. Sasa ni lazima na Tannesco nayo ihamie huko pia, kuna umuhimu gani Ofisi za mifuko ya Hifadhi ya jamii nayo kuhamia dodoma?

Usije ukashangaa na Mamlaka ya Bandari nayo inahamishia makao yake Makuu Dodoma!
 

Hata mimi nawashangaa!
 
Jambo jingine, ni kasi ya kwenda Dodoma. Kwa utaratibu wa sasa kama ungetumiwa na viongozi waliopita bila shaka Serikali ingehamia huko zamani sana, lakini walikuwa wanataka watu wahamie kwa utaratibu pamoja na familia Zao.

Kinachotokea saa hizi ni watu kuhamia nusu nusu tu. Ofisi hazitoshi, nyumba za makazi hazitoshi, huduma za kijamii kama shule hazitoshi na Kutatokea janga kubwa la familia na ndoa kuvunjika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…