Gusa usukumani usikie kelele?
Uko very sana tena hujakosea.Cha kwanza utasikia kutoka kwa Wenye Makofia.Tangazo linaanzaga hivi.Sikia ee na uelewe ee mambo yanavyokwenda.
Ni marufuku kwa mtu yeyote ku.......Sisi(Wenye mkofia) tutawachukuli hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwapeleka mahakamani (utadhani wao ndio wanajua sana sheria).
Kuna mtu mmoja humu amezungumza kuhusu Corona na Lumumba.Duuuu mzee wamebweka kama simba mzee nikajiuliza mbona hivi,nikakumbuka jamaa yangu aliniambiaga mgao wanaopata kutoka kwa bosi wao Kijani kwa kufanya hivyo si mdogo.Basi nikaelewa.Ukilipwa vizuri fanya kazi kwa bidii.Nilisikiaga book mbili vijana wakisema.
Haki huinua taifa bali
(dhuluma,ugandamizaji,unyanyasaji,ubaguzi,uuaji,utekaji,ubambikiaji wa kesi nk.) ni dhambi tena ni aibu kwa taifa.
Wachagga poleni.Mnajua kuchapa kazi,nyie hata njaa ikija hamsubiri unga wa serikali,mnajua thamani ya elimu,mnajituma,mnasaidiana,mnajali kwenu,mnajali kazi za makanisa na misikiti kwa michango,mwezi 12 mpo Moshi na famili zenu kwenye maboma yenu mkitokea Dar,Chato,Mwz,Tabora,Shinyanga,Bukoba,Kahama,Nairobi,Kampala kila kona (Kila mmoja na gari lake huko mgombani,kweli raha,nani anawaweza sasa) mpo kila mahali Tanzania mpaka pale Chato nimewakuta.Mwisho wa siku faida yote mnayochuma huko inarudi Moshi kwa maendeleo ya vijiji vyao.(Kwani si mnajua)
Kumbuka huu msemo kwa tofauti kidogo,mvua inanyesha nje mchagga yupo ndani,ile mvua haimzuii kuchapa usingizi wake.
Waacheni waendelee kuhangaika iko siku watakoma.Endeleeni kumtii Mungu kwa sala na maombezi.Majibu ni hapa hapa au Pantaleo unasemaje wewe