Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Wanabodi,
Asalam aleikum!
Kwa muda mrefu sasa zile hisia na dhana ya Rais Magufuli kulichukia kabila hili la Wachaga sasa amedhihirisha jana.
Pamoja na kwamba alikuwa anaongea kwa utani lakini hilo ndilo liko moyoni kwake ila hakupata sehemu pa kulisemea.
Katika clip hii ambayo Mama mmoja aliyekuwa akilalamika kuwa wametapeliwa kwenye umoja wa vikoba vyao na Grace Mushi, kitu ambacho kilimfurahisha Rais kusikia aliyemtapeli ni Mchaga.
Rais alienda mbali zaidi kwa kumlaumu Mama huyu kuwa kwanini walimpa dhamana huyu dada wa Kichagga awahifadhie hela?
Pamoja na kwamba alikuwa akiongea kwa utani, lakini alionekana wazi wazi akishadadia kuwa Wachaga si watu wazuri na wakuwamini katika fedha.
Nina wasiwasi tukio hili ni la kutengeneza ili upate sehemu ya kulinanga kabila hili.
Tunaomba utuombe radhi mara moja.
WAchagga walimtesa sana pale faculty mwaka 1987, UDSm, na alitoswa mara 3 na dada Flora Ringia, tuyaache lakini anawachukia kuliko hata CORONA