Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

THX PM
 

Attachments

  • 545bc1e6-f51c-44e8-aeac-73cce900fe77-360x220.jpeg
    545bc1e6-f51c-44e8-aeac-73cce900fe77-360x220.jpeg
    9.8 KB · Views: 1
Hili ni janga, Marekani walipoona maisha yao yanachezewa na mtu mmoja wakapiga chini. Wapambe wakajitokeza kulazimisha, wenye busara wakasema uhai wetu ni MUHIMU kuliko mtu mmoja. Bila kumtupa YONA Baharini tutakwisha.
Safi
 
Yeye ndo aliongoza kuzodoa watu wanaovaa Barakoa kila mkutano aliohudhuria. Mfariji mkuu anapokuwa mzodoaji mkuu unategemea faraja hapo? Wewe ifike jioni kuna baridi mtoto wako mmoja avae sweta watatu waendelee kucheza kifua wazi , unapotokea unamzodoa aliyevaa sweta na kuwasifu wanaotamba kifua wazi. Kesho wakiugua Pneumonia umlaumu aliyevaa Sweta au watoto waliocheza vifua wazi?
Kwa mtu yotote mwenye akili hakupaswa kumfatiliza au kusubiri tamko kutoka kwake, unakuta mtu mzima na akili zake na elimu yake eti anasubiri Rais atoe tamko la kuvaa barakoa..
Corona haijaanza Leo na tahadhari zote tunazijua..tulipaswa kuchukua tahadhari sisi wenyewe kabla ya kusubiri kuambiwa.
 
Ofcourse Serikali ni vigumu kuzuia mtu (Ingawa kule Moshi kuna mtu ambaye yupo Serikalini aliwaambia watu wazivue)..., pili dhihaka na yeye kusifu watu ambao hawajavaa ni msimamo tosha wakufanya watu wanaovaa waonekane ni wa ajabu.

Pia tujihadhari na Barakoa tu zinazotoka nje ?... Je vipi mitumba, Misaada, Magari, TV, Electronics, Simu, Madawa, Mafuta, Sukari, n.k. Hivyo ni Salama (au ndio kuzua taharuki ?)

Hivi TBS na Taasisi zote zinafanya nini ? Kwanini zisizuie vitu ambavyo sio salama au kuvipiga marufuku ?, Mimi mteja mtaani ninayenunua nina vipimo au ninajuaje kwamba hiki sio salama ?, Au ndio mwanzo wa Trade Wars na kusema kila kinachotoka nje ni sumu ? (Kama ndivyo hio ingefanikiwa tu iwapo tungekuwa tunajitosheleza kwa quality na quantity) unless otherwise ni kuzidisha taharuki na sintofahamu kwa wananchi.. (watu wataogopa kutumia oil wakidhani in Corona)
TBS wenyewe hawajitoshelezi ki technology baadh ya vitu hawajui na hawana taaluma hiyo Cha kufanya tumwombe Mungu na Yona atupwe baharin
 
Kwahiyo hiyo vita ya kiuchumi anapigana Tanzania pekee??

Hao USA, Italy, France hawana hizo vita??

Mambo mengine ni ya kukaa kimya, yanashusha credibility yako tu.
 
Hahaha watanzania tuna shida kubwa sana..walitaka waambiwe "vaeni" ...
Sasa hivi roho zao nyeupe..kesho utaona kila mtu na barakoa yake na mandoo ya kunawa mikono kila sehemu
 
Back
Top Bottom