Rais na Taasisi saidizi zirudi Dar es Salaam, Makamu wa Rais abaki Dodoma

tuliwaambia issue sio kuhamia dodoma, malalamiko yalikuwa kwenye uharaka na gharama itakayotumika......naona mnatema ndoano taratibu....
 
Dodoma wabaki Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, Spika aende chato bunge ataliongoza kwa WhatsApp video call
 
Mimi ningeomba kwanza kufahamishwa nisababu zipi kwa wakati wa nyerere zilipelekea dodoma kupendekezwa kuwa makao makuu ya nchi?
 
Hakuna kitu kitaniuma katika maisha yangu kama kuua habari ya Dodoma, tumeenda Dodoma, tumefika Dodoma, Dodoma imeanza kushamiri, watu wananunua viwanja. Hakika wanasiasaa ndio miungu wa dunia hii.
 
Kama tulipanga kuhamia dodoma na kulikuwa na umuhimu na priority hiyo basi tungetengeneza time frame na phases kuanzia one mpaka sita....kwa kutenga budget kila mwaka na kufanya kitu..sio ghafla bin vuu tu...
 
Huu upuuzi ndo jpm alikuwa hataki.yaan wanaloliona gumu kumbe jepesi tu.

Ukiona mtu anaeogopa kufanya maamuzi jua kichwa maji tu.

Kama sio jpm sidhani kama ikulu ingehamiaga dodoma.

Rip jpm
Hata kurudi Dar es salaam ni maamuzi pia bwashee!
 
Safari ya Dodoma hatua iliyofikia inaitwa "point of no return", fedha iliyotumika kwenye majengo + hela za kuhamisha wafanyakazi, hakuna namna wanaweza kufanya reverse.
 
Ivi BOT na Gavana waliwahi kuhamia Dodoma pia?
 
Siyo lazima kuhamia Dodoma!
 
uendeshaji wa ofis ni ghali mno wabaki Dodoma foleni hapa dar zipungue
 
Je kuhamia DDM ndio kujali hali ya wanyonge? sioni mantiki ya kauli hii. Kuhamia DDM kumeligharimu Taifa fedha nyingi bila maandalizi ya kutosha. Maraisi waliotangulia isipokua Magu wailiona ni vema kuhamia kidogokidogo bila kuumiza wananchi. Unafrees ajira, promosion zote na kupeleka budget kiduchu isipokuwa Budget ya ujenzi hii sio sawa. Nchi hujengwa kwa kuendeleza watu na sii vitu. Kwa sasa na technolojia hii unadhani kuna haja ya kuwa DDM kwa sasa?
 
Nimekuelewa sana bwashee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…